Wanasayansi wagundua uwepo wa bahari katika Sayari ya Mars | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasayansi wagundua uwepo wa bahari katika Sayari ya Mars

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Jul 7, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,610
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]NI HATUA NZURI YA UWEZEKANO WA BINADAMU KWENDA KUISHI, DALILI ZAONYESHA KUNA VIUMBE HAI
  Leon Bahati
  WANASAYANSI wa anga kwa muda mrefu wamekuwa wakitafuta uwezekano wa maisha katika sayari nyingine, mbali na dunia.Kuna imani kuwa kwenye sayari hizo, huenda zikapatikana raslimali nyingi kwa urahisi kuliko duniani ambako binadamu wameishi mamilioni ya miaka hadi sasa.

  Wataalamu hao wa anga wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda sasa na moja ya mambo muhimu wanayoangalia ni upatikanaji wa maji. Popote maji yanapopatikana, wanaamini maisha yanawezekana.Moja ya sayari ambayo wamekuwa wakiichunguza kwa miaka mingi sasa ni Mars, ambayo ni ya nne kutoka kwenye jua. Dunia ni ya tatu.

  Sababu kuu za kuichagua sayari hii tofauti na zingine ni kwamba, hali ya hewa inatofautiana kidogo sana na ya dunia.

  Sayari nyingine kama Mercury na Venus, zipo karibu zaidi na jua na hali ya joto iko juu kiasi kwamba hali ya maisha inaweza kuwa taabu.

  Mars ambayo wanasayansi wanaipa jina la sayari nyekundu, ipo karibu na dunia, hivyo ni rahisi kufika iwapo wanasayansi watathibitisha iwapo maisha yanawezekana huko.

  Wanaiita sayari nyekundu kwa sababu eneo kubwa la uso wake ni wa rangi nyekundu, tofauti na nyingine zilizomo kwenye mfumo wetu wa sayari.

  Hakuna mwanasayansi ambaye amethubutu kusafiri hadi kwenye sayari hiyo kutokana na ugumu wa kupata vyombo vya kuaminika, vinavyoweza kusafirisha watu kutoka duniani hadi Mars na kurudi salama.

  Hata hivyo, hilo siyo tatizo kwa sababu wakibaini mazingira mazuri, utengenezaji wa vyombo hivyo hauwezi kuwapa taabu.

  Kazi ya uchunguzi imekuwa ikifanywa kwa vyombo maalumu ambavyo havina watu lakini, vina uwezo wa kuleta mawasiliano duniani.

  Pia wanatumia viona mbali katika mchakato huo kuchunguza hali ilivyo kwenye sayari hii, ambayo kumekuwapo na hisia kwamba huenda waliwahi kuishi viumbe hai mamilioni ya miaka iliyopita lakini baadae mazingira yakabadilika na kuwa mabaya.

  Uchunguzi unaonyesha kuwa, sayari hii ina mabonde mengi ambayo yanakila dalili kuwa awali yalikuwa yanatiririsha maji kama ilivyo mito hapa duniani.

  Kwa muda mrefu, wanasayansi wamekuwa wakiichukulia sayari hiyo kuwa na mazingira ya jangwa yanayotokana na ukame wa muda mrefu.

  Wagundua maji
  Mwezi uliopita wanasayansi hao wamekuja na maelezo kwamba sayari hiyo ina kiwango kikubwa cha maji na mengi yapo mita chache kutoka uso wake.

  Mmoja wa wanasayansi wanaochunguza sayari hiyo ni Profesa Jay Melosh wa Chuo Kikuu cha Purdue, nchini Marekani.

  Yeye anasema uchunguzi huo umewapa imani kwamba siyo tu kwamba Mars ina maji bali kuna viumbe wadogo, mfano wa jamii ya bacteria ambao wanaendelea kuishi humo hadi leo hii.

  Ni uchunguzi ambao wanaamini una matumaini tofauti na taarifa za uchunguzi uilizopita na kizuri zaidi pia ni kubaini moja ya miezi yake miwili, maji yapo kwa wingi zaidi.

  Miezi inayoizunguka sayari ya Mars ni Demos na Phobos. Phobos ndio mwezi uliogundulika kuwa na kiwango kikubwa cha maji na ndio ulio karibu zaidi na sayari hiyo.

  Kwa sababu hiyo, wanaamini kwamba maisha yakianza kwenye sayari ya Mars, kuna uwezekano pia wengine wakahamia kwenye mwezi huo wa Phobos.

  Taarifa za uwepo wa maji kwenye sayari hii zilitolewa kwenye mkutano wa wanasayansi wanaochunguza anga za mbali, uliofanyika Austria Juni mwaka huu.

  Moja ya dalili za uwepo wa maji ni vimondo ambavyo vimekuwa vikianguka kwa wingi kwenye uso wa sayari hiyo.
  Mtaalamu wa Uhandisi na Mambo ya Anga, Profesa Kathleen Howell anasema picha walizopiga maeneo ambaye vimondo vimegonga uso wa Mars, zilionyesha dalili kama za mtu aliyetupa jiwe kwenye eneo lenye tope.

  “Sehemu kimondo kilipoigonga sayari ya Mars, aina ya kitu kama tope kiliruka na kusambaa pembeni,” anasema Profesa Howell.

  Hali hiyo wakaitafsiri kuwa maji yaliyokaribu na uso wa sayari hiyo yaliruka pamoja na udongo wakati, kimondo kilipozama ndani na kusambaa pembeni.

  Hali hii iko je?
  Utafiti huo unaashiria kwamba, sayari hiyo ina bahari kubwa iliyoenea chini kwa chini kwenye miamba mita chache kuingia ndani.

  Milipuko ya volkano ya miaka mingi iliyopita ni kiashirio kingene kwamba, sayari hii ina maji. Uchunguzi unaonyesha kwamba mlipuko huo uliandamana na maji.

  Ripoti ya utafiti huo ambao umechapishwa pia na jarida la Geology, inaonyesha kuwa kiwango cha maji kilichopo Mars kinakadiriwa kuwa sawa au kimezidi kile kilichopo hapa Duniani.

  “Kimsingi, kiwango cha maji tunayoyazungumzia kinalingana ama ni zaidi ya kile kilichopo kwenye uso wa dunia,” Anasema Kiongozi wa Jopo la Wanasayansi hao, Profesa Francis McCubbin, ambaye pia ni Mtaalamu wa Anga Chuo Kikuu cha Mexico.

  “Si jambo la kushangaza kwamba, kwenye sayari hii waliwahi kuishi viumbe hai miaka iliyopita,” anasema Profesa Howell na kuongeza:

  “Tatizo tutakalokabiliana nalo ni iwapo tayari muda umepita sana kiasi cha kutotambua vyema hali hiyo.

  “Lakini, hata kama hautapatikana uthibitisho wa kisayansi wa viumbe kuwahi kuishi miaka iliyopita, jambo muhimu ni uwezekano wa kiumbe kuweza kuishi kwa sasa.”

  Hatari kwenye Mars
  Hatari iliyopo ni kwamba, ni moja ya sayari ambayo imekuwa ikigongwa mara kwa mara na vimondo vinavyoanguka.

  Ni vimondo vichache sana ambavyo viliwahi kutua kwenye uso wa dunia. Vinapoanguka kuelekea uso wa dunia hukabiliwa na safari ndefu na kutokana na mwendo mkali wa mwanguko, hujikuta vinapata msuguano mkali na hewa, ambao husababisha joto kali linaloimomonyoa udongo hadi inakwisha.
  Sayari hii ambayo ipo karibu na ukanda wa vimondo, uso wake una makovu mengi yanayoashiria athari za vimondo vyenye ukubwa tofauti vilivyotua.

  Vimondo hivi ndivyo vimeweka wazi dalili za kuwapo kwa maji kwenye sayari hii ambayo uso wake unaonekana kama vile jangwa, kwa kutokuwa na miti na ishara ya ukame wa muda mrefu.

  MWISHO[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Wanasayansi wagundua bahari Sayari ya Mars
   
 2. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ila sasa nauli si itakuwa kubwa sana? Imagine watakaoishi huko hawafi, aisee utakuwa mtafutano kwenda huko
   
 3. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo mwisho wa Dunia ukifika inabidi Mungu awe na Kazi mbili. Ya MARS na EARTH....ahahahaha
   
 4. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  SERIKALI ITAGHARAMIA.. Hasa hasa ya Marekani.. Huku kwetu lazima tufe tu
   
 5. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Umeona eeeeee
   
 6. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi wacheni nifie hapahapa bongo
   
 7. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Binadamu yeyote
  atakayemwamini Yesu Kristo,
  ataishi milele MBINGUNI
  Anakoishi Yehova Mungu na
  Bwana wetu Yesu Kristo.
  Hakika ni kama hivo.
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mk.were atakua wa 1 kukimbilia huko after 2015 election
   
 9. m

  mariti New Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 7, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni habari njema inayoonyesha uwezo wa binadamu kuendelea kutathmini mazingira yanayoizunguka dunia. Lakini haaanishi kwamba viumbe waliopo huko (kama wapo) watafanana kimaumbile na walio dunia hii. Wanweza kuwa wajanja au wajinga zaidi yetu. Kumbuka UFOs ambao ni hadithi ya kufikirika na ndio maana kuna sehemu iitwayo Area 51 katika nchi fulani lakini Haipo katika ramani ya nchi hiyo wala kutambulika kimataifa. Si unajua tena mambo ya "classified" information. Tahadhari iliyopo ni kuleta duniani chembechembe hai kutoka huko kwani twaweza angamia sote. Ufahamu huo ni mzuri lakini tusiende huko. Tuchunguze dunia yetu zaidi kwani kuna mengi hatufahamu hasa misituni na baharini. Mfano mzuri ni "bermuda triangle" na mengi mengi yatusukumayo tufanye utafiti hapa duniani.
   
 10. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Makala imetulia sana..... MziziMkavu Mara nyingine uwe unatupa habari za sayari kama hizi
   
 11. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wana uhakika gani kuwa kule kuna maisha kwa binadamu??

  Inawezekana viumbe vya kule hutumia hydrogen badala ya oxygen tutumiayo siye hapa duniani kwetu!!!!
   
 12. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,801
  Likes Received: 2,572
  Trophy Points: 280
  Hati miliki ya ardhi mars zimeanza kutolewa?
   
 13. bigboi

  bigboi JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 80
  Du ngoja nifanye mchakato wa kwenda kule bongo longo longo kibao nikaanzishe tanzania ya mars haitakuwa na mafisadi ccm hairusiwi kwenda kule hatutaki shobo kule ni goood people only
   
 14. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hawajaanza kuuza viwanja huko!!.
   
 15. Zuia Sayayi

  Zuia Sayayi JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 834
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Naskia kuna tume ya katiba inayoundwa kushugulikia mambo ya kule,
   
 16. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  pale posta karibu na feri mbona kuna madalali wwengi tu wa viwanja vya mars...?? kama unataka nenda pale kaulizie..
   
 17. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  madalali hawaaminiki, wanaweza kuniuzia viwanja vilivyopo kwenye venus.
   
 18. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,456
  Trophy Points: 280
  hongera zao, dunia yenye maji tele ambayo huhitaji kuhangaika sana kuayapata imetushinda kuitunza sasa hiyo yenye maji yanayo sadikika yako chini na inawezekana si kweli na haina hali ya hewa ambayo sisi binadamu tutaweza ishi kwa raha mstarehe kama duniani ndo wanahangaika nayo. Bora wangewekeza kuboresha maeneo ya dunia yanayo geuka kuwa jangwa kwasababu ya uharibifu wa mazigiara.
  Lakini hongera zao.
   
 19. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,866
  Trophy Points: 280
  Itabidi Waafrica na sisi tuwahi ili ulaya ya Mars iwe yetu na wazungu wachukue Africa ya kule.:nerd:
   
 20. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Mungu Hana mamlaka na sayari nyngne kwa Sabab hakuiumba
   
Loading...