Watafiti na ndoto za kuanzisha maisha Mars

Eugen TZA

Member
Aug 7, 2023
61
98
Kumekua na juhudi katika siku za hivi karibuni zikifanywa na binadamu kutafuta uwezekano wa kuanzisha maisha mapya katika sayari nyingine nje ya sayari ya Dunia, Elon Musk tayari ana vifaa vinavyoendelea na kazi huko Mars akitafuta namna ambayo binadamu ataweza kuishi.
-
Ripoti za hivi karibuni zimeendelea kugongea msumari tafiti iliyofanyika mwaka 2021 ambapo wanasayansi waligundua michirizi au mipasuko katika sayari ya Mars inayofanana na mipasuko ya huku Duniani hivyo huenda ilikua na maisha miaka bilioni 3.6 iliyopita kama ilivyo sasa hapa katika sayari ya Dunia.
-
Licha ya ugunduzi huo bado huenda binadamu akaishi kwa shida sana katika sayari ya Mars kutokana na sayari hiyo kuwa na kiwango cha chini sana cha baridi hasa nyakati za usiku, vimbung'a, na miyonzi hatari, Hata hivyo wazo la Elon Musk ni kutengeneza mahema ya kisasa (Dome) ambayo binadamu atakua akiishi ndani yake.
-
#PeaceOverInterest
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom