Wanasayansi wagundua uwepo wa bahari katika Sayari ya Mars

Ila sasa nauli si itakuwa kubwa sana? Imagine watakaoishi huko hawafi, aisee utakuwa mtafutano kwenda huko
Jakubumba Ni Kweli nauli itakuwa ni kubwa na watako ishi huko watakuwa ni matajiri sisi Masikini hatuwezi kwenda wala kuishi huko mkuu.

Kwahiyo mwisho wa Dunia ukifika inabidi Mungu awe na Kazi mbili. Ya MARS na EARTH....ahahahaha
RGforever Mwenyeezi Mungu hawezi kuwa na kzi mbili wakati hiyo Sayari ya Mars aliyeiumba ni ndiye yeye aweje teana kuwa na kazi mbili ikifika mwisho wa hii dunia hiyo sayari
Mars pia hatokuwepo itaangamia tu kama dunia itakavyoangamia.

Mk.were atakua wa 1 kukimbilia huko after 2015 election
Angel Msoffe Atakimblia huko kwanini huyo uliye mtaja? hapa duniani anamuogopa nani?

Wana uhakika gani kuwa kule kuna maisha kwa binadamu?

Inawezekana viumbe vya kule hutumia hydrogen badala ya oxygen tutumiayo siye hapa duniani kwetu!!!!
Kwetu Iringa Mahali palipo kuwa na Maji uhai hautokosekana wapo kwenye Uchuınguzi Je Maji yapo? kama maji hakuna ina maana hakuna hapo Uhai. mkuu hutaki ndugu zako wa kihehe na majirani zako wa kjibena muende kuishi huko kwenye Sayari ya Mars Mkuu?Kamwene? Mnogage? Ulamwiko?

Du ngoja nifanye mchakato wa kwenda kule bongo longo longo kibao nikaanzishe tanzania ya mars haitakuwa na mafisadi ccm hairusiwi kwenda kule hatutaki shobo kule ni goood people only
Karibu sana Mkuu bongo yetu njoo uwasafishe Mafisadi wasiende kwenye Sayari ya Mars bigboi;

hongera zao, dunia yenye maji tele ambayo huhitaji kuhangaika sana kuayapata imetushinda kuitunza sasa hiyo yenye maji yanayo sadikika yako chini na inawezekana si kweli na haina hali ya hewa ambayo sisi binadamu tutaweza ishi kwa raha mstarehe kama duniani ndo wanahangaika nayo. Bora wangewekeza kuboresha maeneo ya dunia yanayo geuka kuwa jangwa kwasababu ya uharibifu wa mazigiara.
Lakini hongera zao.
Mkuu Bado wapo Kwenye Utafiti hawajapata bado UhakikaMzuri kuwa je wanaweza Watu kuishi huko? Tunangojea Wana Sayansi watupe Jibu lili kamili Subiri itafika siku utasikia Binadamu wanakwenda huko kutalii na kuishi huko kwenye hiyo Sayari ya Mars elmagnifico
 
Last edited by a moderator:
Mungu Hana mamlaka na sayari nyngne kwa Sabab hakuiumba
Mkuu umekosea kusema hivyo Mwenyeezi Mungu ndie Mwenye Mamlaka ya vitu vyote na ndie alivyoviumba yeye hakuna zaidi yake na ni mwenye uwezo wa kila kitu Mungu huyo huyo ndie aliyekupa wewe akili itabidi uitumie sio kusema maneno ambayo huna uwezo nayo wala huna elimu nayo samahani mkuu kama nitakukwaza. kama kitu hujuwi bora kuuliza kuliko kuropoka ovyo pasipo na elimu yoyote ile Amoeba.
 
Mkuu umekosea kusema hivyo Mwenyeezi Mungu ndie Mwenye Mamlaka ya vitu vyote na ndie alivyoviumba yeye hakuna zaidi yake na ni mwenye uwezo wa kila kitu Mungu huyo huyo ndie aliyekupa wewe akili itabidi uitumie sio kusema maneno ambayo huna uwezo nayo wala huna elimu nayo samahani mkuu kama nitakukwaza. kama kitu hujuwi bora kuuliza kuliko kuropoka ovyo pasipo na elimu yoyote ile Amoeba.

Hahahaa!
Heshima Mbele Mkuu MziziMkavu.
Twende taratibu kaka, huenda na mimi ukanielimisha; Hebu jaribu kuongea kwa evidence nitafakari.
 
Last edited by a moderator:
ikiwa-mras.jpg
NI HATUA NZURI YA UWEZEKANO WA BINADAMU KWENDA KUISHI, DALILI ZAONYESHA KUNA VIUMBE HAI Leon Bahati WANASAYANSI wa anga kwa muda mrefu wamekuwa wakitafuta uwezekano wa maisha katika sayari nyingine, mbali na dunia.Kuna imani kuwa kwenye sayari hizo, huenda zikapatikana raslimali nyingi kwa urahisi kuliko duniani ambako binadamu wameishi mamilioni ya miaka hadi sasa. Wataalamu hao wa anga wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda sasa na moja ya mambo muhimu wanayoangalia ni upatikanaji wa maji. Popote maji yanapopatikana, wanaamini maisha yanawezekana.Moja ya sayari ambayo wamekuwa wakiichunguza kwa miaka mingi sasa ni Mars, ambayo ni ya nne kutoka kwenye jua. Dunia ni ya tatu. Sababu kuu za kuichagua sayari hii tofauti na zingine ni kwamba, hali ya hewa inatofautiana kidogo sana na ya dunia. Sayari nyingine kama Mercury na Venus, zipo karibu zaidi na jua na hali ya joto iko juu kiasi kwamba hali ya maisha inaweza kuwa taabu. Mars ambayo wanasayansi wanaipa jina la sayari nyekundu, ipo karibu na dunia, hivyo ni rahisi kufika iwapo wanasayansi watathibitisha iwapo maisha yanawezekana huko. Wanaiita sayari nyekundu kwa sababu eneo kubwa la uso wake ni wa rangi nyekundu, tofauti na nyingine zilizomo kwenye mfumo wetu wa sayari. Hakuna mwanasayansi ambaye amethubutu kusafiri hadi kwenye sayari hiyo kutokana na ugumu wa kupata vyombo vya kuaminika, vinavyoweza kusafirisha watu kutoka duniani hadi Mars na kurudi salama. Hata hivyo, hilo siyo tatizo kwa sababu wakibaini mazingira mazuri, utengenezaji wa vyombo hivyo hauwezi kuwapa taabu. Kazi ya uchunguzi imekuwa ikifanywa kwa vyombo maalumu ambavyo havina watu lakini, vina uwezo wa kuleta mawasiliano duniani. Pia wanatumia viona mbali katika mchakato huo kuchunguza hali ilivyo kwenye sayari hii, ambayo kumekuwapo na hisia kwamba huenda waliwahi kuishi viumbe hai mamilioni ya miaka iliyopita lakini baadae mazingira yakabadilika na kuwa mabaya. Uchunguzi unaonyesha kuwa, sayari hii ina mabonde mengi ambayo yanakila dalili kuwa awali yalikuwa yanatiririsha maji kama ilivyo mito hapa duniani. Kwa muda mrefu, wanasayansi wamekuwa wakiichukulia sayari hiyo kuwa na mazingira ya jangwa yanayotokana na ukame wa muda mrefu. Wagundua maji Mwezi uliopita wanasayansi hao wamekuja na maelezo kwamba sayari hiyo ina kiwango kikubwa cha maji na mengi yapo mita chache kutoka uso wake. Mmoja wa wanasayansi wanaochunguza sayari hiyo ni Profesa Jay Melosh wa Chuo Kikuu cha Purdue, nchini Marekani. Yeye anasema uchunguzi huo umewapa imani kwamba siyo tu kwamba Mars ina maji bali kuna viumbe wadogo, mfano wa jamii ya bacteria ambao wanaendelea kuishi humo hadi leo hii. Ni uchunguzi ambao wanaamini una matumaini tofauti na taarifa za uchunguzi uilizopita na kizuri zaidi pia ni kubaini moja ya miezi yake miwili, maji yapo kwa wingi zaidi. Miezi inayoizunguka sayari ya Mars ni Demos na Phobos. Phobos ndio mwezi uliogundulika kuwa na kiwango kikubwa cha maji na ndio ulio karibu zaidi na sayari hiyo. Kwa sababu hiyo, wanaamini kwamba maisha yakianza kwenye sayari ya Mars, kuna uwezekano pia wengine wakahamia kwenye mwezi huo wa Phobos. Taarifa za uwepo wa maji kwenye sayari hii zilitolewa kwenye mkutano wa wanasayansi wanaochunguza anga za mbali, uliofanyika Austria Juni mwaka huu. Moja ya dalili za uwepo wa maji ni vimondo ambavyo vimekuwa vikianguka kwa wingi kwenye uso wa sayari hiyo. Mtaalamu wa Uhandisi na Mambo ya Anga, Profesa Kathleen Howell anasema picha walizopiga maeneo ambaye vimondo vimegonga uso wa Mars, zilionyesha dalili kama za mtu aliyetupa jiwe kwenye eneo lenye tope. “Sehemu kimondo kilipoigonga sayari ya Mars, aina ya kitu kama tope kiliruka na kusambaa pembeni,” anasema Profesa Howell. Hali hiyo wakaitafsiri kuwa maji yaliyokaribu na uso wa sayari hiyo yaliruka pamoja na udongo wakati, kimondo kilipozama ndani na kusambaa pembeni. Hali hii iko je? Utafiti huo unaashiria kwamba, sayari hiyo ina bahari kubwa iliyoenea chini kwa chini kwenye miamba mita chache kuingia ndani. Milipuko ya volkano ya miaka mingi iliyopita ni kiashirio kingene kwamba, sayari hii ina maji. Uchunguzi unaonyesha kwamba mlipuko huo uliandamana na maji. Ripoti ya utafiti huo ambao umechapishwa pia na jarida la Geology, inaonyesha kuwa kiwango cha maji kilichopo Mars kinakadiriwa kuwa sawa au kimezidi kile kilichopo hapa Duniani. “Kimsingi, kiwango cha maji tunayoyazungumzia kinalingana ama ni zaidi ya kile kilichopo kwenye uso wa dunia,” Anasema Kiongozi wa Jopo la Wanasayansi hao, Profesa Francis McCubbin, ambaye pia ni Mtaalamu wa Anga Chuo Kikuu cha Mexico. “Si jambo la kushangaza kwamba, kwenye sayari hii waliwahi kuishi viumbe hai miaka iliyopita,” anasema Profesa Howell na kuongeza: “Tatizo tutakalokabiliana nalo ni iwapo tayari muda umepita sana kiasi cha kutotambua vyema hali hiyo. “Lakini, hata kama hautapatikana uthibitisho wa kisayansi wa viumbe kuwahi kuishi miaka iliyopita, jambo muhimu ni uwezekano wa kiumbe kuweza kuishi kwa sasa.” Hatari kwenye Mars Hatari iliyopo ni kwamba, ni moja ya sayari ambayo imekuwa ikigongwa mara kwa mara na vimondo vinavyoanguka. Ni vimondo vichache sana ambavyo viliwahi kutua kwenye uso wa dunia. Vinapoanguka kuelekea uso wa dunia hukabiliwa na safari ndefu na kutokana na mwendo mkali wa mwanguko, hujikuta vinapata msuguano mkali na hewa, ambao husababisha joto kali linaloimomonyoa udongo hadi inakwisha. Sayari hii ambayo ipo karibu na ukanda wa vimondo, uso wake una makovu mengi yanayoashiria athari za vimondo vyenye ukubwa tofauti vilivyotua. Vimondo hivi ndivyo vimeweka wazi dalili za kuwapo kwa maji kwenye sayari hii ambayo uso wake unaonekana kama vile jangwa, kwa kutokuwa na miti na ishara ya ukame wa muda mrefu. MWISHO
Wanasayansi wagundua bahari Sayari ya Mars
mbona hata bahari uliyosema, haijaongelewa make mimi nimeona kama tope vile pembeni mwa vimondo vinayoanguka?
 
Inaaminika huko ndiko wanakoishi (UFO) unidentified flying objects,inaaminika wako humu duniani baada ya vyombo vyao kuharibika na kushindwa kuruka kurudi walikotoka,na inaaminika wako marekani na Russia na ndiyo wanaotoa siri nyingi za kiugunduzi na sayansi katika NASA ya marekani,documentary zipo na CIA agents wamethibitisha hilo kwa kutoa hiyo documentary film baada ya kuruhusiwa na serikali ya Marekani kuitengeneza na kuitoa hadharani,mwenye kutaka kujua zaidi tafadhali itafute ushangae. inaitwa UFO.
 
Hakuna uwezekano wa mtu kuishi mars, kwa sababu hakuna atmosphere, huyo mtu atapona na baridi, inawezekana kweli kuna maji yamesalia ndani ya mars lakini yatakwisha yote. Hapo awali wanasayansi wanasema mars ilikuwa ma bahari, maziwa na mito yenye maji juu ya nchi. Tatizo lililoikumba mars inaitwa kwa kimombo 'running green house gases', inasemekana atmospheric gases zote zilipata spidi mtoroko,(escape speed) na gesi zote zikatoroka kwenda anga za mbali. Tangu hapo kumekuwa na running out vapourization ya maji, na inakadiliwa baada ya miaka 4.5 bilioni maji yote ya mars yatatoweka. Kwa hiyo ni vigumu kuishi sayari ambayo haina cycles za life essentials, kwa mfano water cycle, nitrogen cycle, carbon cycle, nk. Ili watu waishi mars nilazima wabuni mbinu za ku-cycle maji na carbon kwanza
 
...Mkuu Homosapien, kirefu cha UFO ni Unidentified Flying Object - Vyombo vya anga vinavyoonekana vikiruka angani ambavyo vinakosa utambulisho wa uhakika kutoka kwa binadamu wanaoviona. Ukweli ni kwamba 'kelele' hizi za kuwepo na vyombo na viumbe vinavyokuja duniani zimekuwepo kuanzia miaka ya 1940 lakini cha ajabu ni kwamba hadi leo hii katika karne hii ya sayansi na tekinolojia imeshindikana kupata angalau picha tu isiyo na shaka ya viumbe ama vyombo hivyo, jambo ambalo litupeleka kuamini kwamba haya ni mawazo yetu tu binadamu na siku itakapotokea vyombo ama viumbe hivyo kuonekan kwa uwazi kabisa bila kificho basi hiyo itakuwa 'frony page news ya vyombo vyote vya habari ulimwenguni!! Tunapaswa kujiuliza: Mbona vyombo ama viumbe hao huelekea kuonekana huko Ulaya tu? Ia maana hata wao wameishatutambua kuwa Afrika ni bara la Giza tu? Kwa nini hakuna taarifa zisizo na shaka za kuonekana kwa viumbe ama vyombo hivyo huku Afrika bali Ulaya tu?? Ukweli ni kwamba mpaka sasa hakuna ukweli wa kuaminika usio na shaka kuwa kuna viumbe wengine kwenye sayari yetu. Badalaya yake hawa wamarekani wanaooongoza kwa 'kelele' hizo wameishia kuiachia Hollywood yake kututengenezea Sinema za kufikirika za vile wanavyoamini viumbe na vyombo hivyo vinaweza kuwa. Angalia: INdependence Day ya Will Smith, Predator ya Arnold Schwaznegger, War of the Lords ya Tom Cruise, Knowing ya Nicolas Cage,Signs ya Mel Gibson, The Day the Earth stood Still ya Keanu Reeves, Race to Witch Mountain ya Dwayne Johnson na nyingi nyinginezo. Naamini kuwa siku kikikamatwa chombo ama kiumbe kutoka Sayari nyingine tutajua tu!!!
 
Mkuu Homosapien, kirefu cha UFO ni Unidentified Flying Objects - Vyombo vya anga vinavyoonekana vikiruka angani ambavyo vinakosa utambulisho wa uhakika kutoka kwa binadamu wanaoviona. Ukweli ni kwamba 'kelele' hizi za kuwepo na vyombo na viumbe vinavyokuja duniani zimekuwepo kuanzia miaka ya 1940 lakini cha ajabu ni kwamba hadi leo hii katika karne hii ya sayansi na tekinolojia kubwa tuliyonayo binadamu bado imeshindikana kupata angalau picha tu isiyo na shaka ya viumbe ama vyombo hivyo, jambo ambalo litupeleka kuamini kwamba haya ni mawazo yetu tu binadamu na siku itakapotokea vyombo ama viumbe hivyo kuonekana kwa uwazi kabisa bila kificho basi hiyo itakuwa 'front page news ya vyombo vyote vya habari ulimwenguni!! Tunapaswa kujiuliza: Mbona vyombo ama viumbe hao huonekana huko Ulaya tu? Ina maana hata wao wameishatutambua kuwa Afrika ni bara la Giza tu? Kwa nini hakuna taarifa zisizo na shaka za kuonekana kwa viumbe ama vyombo hivyo huku Afrika kwetu?? Ukweli ni kwamba mpaka sasa hakuna ukweli wa kuaminika usio na shaka kuwa kuna viumbe wengine kwenye sayari yetu. Badalaya yake hawa wamarekani wanaoongoza kwa 'kelele' hizo wameishia kuiachia Hollywood yake kututengenezea Sinema za kufikirika za vile wanavyoamini viumbe na vyombo hivyo vinaweza kuwa. Angalia: INdependence Day ya Will Smith, Predator ya Arnold Schwaznegger, War of the Worlds ya Tom Cruise, Knowing ya Nicolas Cage,Signs ya Mel Gibson, The Day the Earth stood Still ya Keanu Reeves, Race to Witch Mountain ya Dwayne Johnson na nyingi nyinginezo. Naamini kuwa siku kikikamatwa chombo ama kiumbe kutoka Sayari nyingine tutajua tu!!!
 
Back
Top Bottom