Kuna uwezekano gani wa uwepo wa viumbe wengine sayari nyingine wenye utashi lakini wasioweza kupumbazwa(mind manipulation)

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,621
46,264
Binadamu ni viumbe wa ajabu sana, anaweza kutokea mtu mmoja tu akawafanya wachukiane, wahasimiane, wawindane na kuparuana kama paka na panya au mwewe na kuku.

Halafu pia binadamu hao hao anaweza kuja mtu mwingine mmoja tena akawafanya wapendane, waheshimiane na waishi pamoja tu bila purukushani zozote kama vile mbuzi na kondoo. Hii kama glitch kubwa katika mfumo wa binadamu inayomfanya kuharibu mambo wakati mwingi

Kuna uwezekano wa viumbe wengine wenye akili na utashi kutoka sayari nyingine lakini wakiwa hawana flaw/glitch ya aina hii? Ambao haiwezekani kufanyiwa mind manipulation au kutenda mambo kwa hisia?
 
Vitu vingi tunaathiriwa na mazingira na watu wanaotuzunguka

Ni km dini ukizaliwa wazazi waislamu mkiristo una muona kafiri na viceversa is true

Hata ndoa kuna jamii ukiolewa ni heshima..kuna jamii watoto tu ndio heshima ww oa usioe utajua mwenyewe

N:B Huu utofautianaji wa mitizamo na kufikiri ndio huifanya dunia iwe bomba

Ingekuwa wote tunafwata kitu kimoja tu siku mtu akitupoteza wote dunia nzima tunaenda kombo
 
Kama kuna viumbe wengine sayari nyingine basi bila shaka watakuwa tofauti sana na binadamu wa hapa duniani kutokana na mazingira yanayowazunguka huko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom