Kabisaaa..wapimwe akili.Kabisaa
Ushirikiano baina ya jeshi la police na raia ni lazima udumishwe. Hii itasaidia amani ya nchi kuzidi kwenda mbele.Washauriwe waache kutoa matamko yenye ladha ya kisiasa wala kuonekana kuwa na mwelekeo huo bali wawatafute na kupambana na wahalifu. Wasijenge mazingira ya kuwatishia wananchi vinginevyo watakosa ushirikiano wao katika kutekeleza wajibu wao!
Ananikumbusha korea ya kaskazini alipokufa kim jong il,pale kwenye msiba lazima ulie kwa juhudi na kuonekana una hudhuni sana,ole wako shushushu wakukute haulii,
wanakuweka kizuizini wewe na family yako yote na haurudi uraiani ng'o..
Haya mauaji ya Polisi yachunguzwe kwa kina...kuna kitu hapa...sio bure......yachunguzwe kwa makini sana
Ukiwakamata uwapeleke mahakamani. Si polisi kama mnavyofanya. Wapeleke mahakamani ili mkajieleze wote.wewe mlalamikaji na yeye mshitakiwa. Hata hivyo ni ajabu kudhani kuwa kwenye msiba watu wote watalia! Wapo watakaofurahia kufa kwako, watakaosikikitika, na ambao wapo wapo kujaza msiba. Na huwezi kuwalazimisha watu kusikitika. Hilo ni suala la hisia za moyo. Na nakuhakikishia utaishia kuwatesa tu kwenye vituo vya polisi. Hawashitakiki.
Kasema kuwahoji sio kuwahukumu,yah wataitwa kuhojiwa.ni kuhojiwa tu si kuhukumiwa.Tatizo hakuna sheria inayohukumu watu wanaocheka,kutaniana ama kutabasamu misibani,itabidi bunge lijalo itungwe.
Sasa ukitiririka kwa style hii ya kutumia jina fake na kisha kutupa line ndio unakuwa umefanya upuuzi gani????.maana unawaogopa.Tuambie watafanyaje?,weka hoja hapo. unakuta mtu kafungua email fake, namba ya simu fake kwanza alishaitupa miezi sita iliyopita, akaunt jf fake, jina lake halijulikani, uhalifu kafanyia internet cafe sio kwenye simu yake, unampataje mtuhumiwa?
Hawa ambao wanatapeli pesa katika makampuni kama mpesa,aitel nk hawpatikan wote,anatumia line na kutupa hawapatikani. juzi tu kuna mtu nilimwona ofisi ya vodacom anaomba msaada ametapeliwa fedha kupitia mpesa wakamwambia hawawezi kum trace mhalifu coz wanatumia line na kuzitupa ,
Inamaana hata km hapo Police wakifanya madudu ktk utekelezaji wa majumu yao bas tuwashangilie? Jeshi la police la Tanzania baaado saana ktk ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yao na kulinda uhuru, haki na amani katika nchi hii...Kabla ya kuogopa kutupiwa maneno au kubezwa wajiangalie kwanza kwa jicho la tatu na kujirekebisha...
Matter of fact, I got no love for them!!!!
Usishangae wakibezwa, unapaswa kijiuliza kwanini wanabezwa?, pia sina hakika kama kubeza jeshi ama hata mtu mmoja mmoja ni kosa, kama kubeza huko hakujafikia kiwango cha kuwa kashfa ama matusi.Polisi wetu wanafanya kazi nzuri sana. Nawashangaa sana wale wanaolibeza