Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Mie nadhani wanapaswa kujitafakari upya! Haya wanayoyasema ni kuendelea kuukuza mgogoro. Mwenye Busara aangukapo husimama,akafuta vumbi, akaangalia kilichomwangusha, na kisha kusonga mbele! Itakuwa ni busara kama watajiuliza hii hali imetokana na nini hadi wachukiwe na wananchi, ni nini kinasababisha leo watu wafurahie maswahibu yanayowapata polisi!

Busara busara busara!
 
Ahahaha kweli,bwana anayetakiwa kukosolewa nchi hii ni UKAWA tu hasa Lowasa,Tundu,na Mbowe,na Maalim wengine wote ni kusifia tu
Jeshi letu la police linafanyakazi nzuri sana linang'aa kiutawala na linaongoza kwa kuwatishia raia wasio na silaha, wameona size yao ni raia na walipojaribu kwa majambazi walipata moto mkali ndo maana wamerudi kwa raia vibonde wao, kagera kule juzi wameuawa raia 56 na inasadikika wameuawa na askari wa Rwanda lakini kimya hadi saiv, sisi raia tusiojua hata kushika bastola tunapigiwa mazoezi kwa ving'ora na washawasha, Jeshi letu la police hoyeeeee!!
 
Raia wanaonewa bure.
Heshima inatolewa pale mtu anapojisikia kathaminiwa na kuheshimiwa.
Kwa sasa jeshi letu linathamini mtu mmoja na kupuuza haki za raia.
 
Polisi siku zote wapo sahihi. Nyie mnaowabeza mna ajenda zenu za siri

Hivi Lizaboni una nini wew? Please nipe siri yako ya wewe kuwa hivi kama hotujali. Mana naamini hata nikiona burudoza linapita juu ya katiba ntapiga makofi na roho haitauma tena
 
inabidi tuwe tunawasifia kuwa walikuwa washawadhiti ipasavyo ghafla jambazi mwenye hilizi kali akawakomboa baada ya mapigano makali sana waliweza kuua polisi woote kwani inaoonekana wana waganga wa jadi wakali kwani hata risasi zetu hazikuwapata over
 
Hivi ww unatoa kauli na bado unajua kwamba siraha hizo zitaenda kuuwa na maeneo gani?Unajisikiaje zikija uwa wazazi wako/mke wako/Dada yako/Watoto wako/ndugu zako wakaribu.Siyo sawa kuongea lugha hiyo kumbuka waliopoteza maisha wanafamilia kama wewe.Watoto wao walikuwa wanawahitaji baba zao ila maisha yao yamekatishwa kikatili.Vuta hisia ndiyo utajua si jambo la kufurahia kamwe.Samahani kama nimekukwaza.
 
Mimi nina swali lakini nsionekane kama mchochezi, kwani wananchi wa Tz kwa sasa wanaheshimu au wanaogpa jeshi la polis?
 
Wanajidharirisha wenyewe kwa kutembea na mabomu barabara kutisha raia wamekuwa kama chama cha siasa, wamaacha taruma zao na kuanza kuisaidia ccm... Na hii kitu wakiendelea nayo wanajijengea chuki kwa raia...
 
Hapo mi maoni yangu ni kwanini raia wanafurahia hii hali.Lazima tujiangalie ili tujue wapi tunakosea.
Lakini tunawapongeza kwa Nazi ngumu za ulinzi wa taifa letu.
 
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Ukweli siku zote unauma sana.
 
Wanastahili kubezwa..., show na mbwembwe zote zile kumbeeee........
 
Kwa hapa nalipongeza sana Jeshi letu la polithi kwa intelligencia hii ya kugundua kuwa kumbe wanamitandao wamelichoka.Nawaomba tu wajitahidi kuboresha hiyo INTELLIGENCIA yao iwe ina Baini na attack kama ya Jana.I salute u gayz

Unajuw maana ya neno gays au ulitaka ku mean Guys??
 
Makamanda uchwara mabomu mwili mzima kumbe hamna kitu

Mbwembwe nyingiwengi wao hawana mafunzo ya kutosha hasa vile vitoto vyao vya kupiga makofi....havina ujuzi wala experience kabisaaa
 
Tukisema ukweli tunasakwa daaah ngoja tukae cul tusije kuwa tunachochea....Time will tell.

Sheria inakulinda mkuu kuwa open na ongew chochote huyo waziri na mkuu wa mkoa wake inu hamna kabisaaaa na wanaongea vitu ambavyo havieleweki...na mwigulu hawajui haki za binadamu wakiamua kufanya kazi hicho cheo chake atakiona kibaya namshauri aache kuropoka
 
Watu mmekuwa waoga kuongea fact.....kuweni makini ila kwenye ukweli inabidi useme ukweli..
eti watawakamata wote walioshabikia kwanza watanilazimisha niwapende police??wafanye kazi waache kutumika bila sababu
 
Tanzania ndio nchi pekee duniani Mwananchi analazimishwa " kufanya mapenzi " na polisi.
 
Tukumbushane ukweli- respect is earned not given.Respect is a two way traffic- tuheshimiane.
 
Jeshi letu la polisi halifungamani na chama chochote cha siasa. Wanafanya mambo yao kwa weredi wa hali ya juu sana, Tuendelee kuwaunga mkono. Wapunguze tu matamako kwenye vyombo vya habari maana nchi yetu haina tishio lolote la usalama kama wanavyojaribu kutwambia. Nimesikitika kuona hata kampuni ya SGA ikitoa security alert kwa wateja wake, eti tarehe 1 September kutakuwa na hali tete ya usalama.... this is a big lie!
Jeshi letu la polisi halifungamani na chama chochote!hapo umesema uongo!na hilo ndo tatizo kubwa la watanzania hatupendi kusema ukweli sijui kama ni uoga au unafiki.
 
Back
Top Bottom