Uwoga waliopandikiza kwa raia pamoja na kwamba kwa kiasi kikubwa umewasaidia sana katika utawala huu wa kiimla, wasifikiri sasa wana uwezo wa kutoa agizo lolote na likafuatwa kama lilivyo hata kama ni la kakipuuzi...!! Yaani unaanzaje kunipangia namna ya kutoa hisia zangu? eti tunawabeza!!? Hivi ni uwaledi upi wanaojivuniaga hawa mapolisi wa tanzania?
Nilishasema na nitaendelea kusema....!! Jeshi la polisi la tanzania ni dhaifu sana na halina uwezo wa kupambana na real criminals
Mara kadhaa tumekuwa tukishuudia uvamizi wa mabenki na waarifu kutokamatwa huku wakifanikiwa kuondoka na fedha na polisi kuishia kukamata suspects tu.
Askari wanapigiwa simu muda ambao tukio la uharifu linafanyika anaanza kuuliza maswali ya kipuuzi... eti wako wangapi!?,wana siraha!?... alafu wanakuja dakika 20 baada ya waarifu kuondoka..bulishiit
Yaani watu wawili wanavamia kituo cha polisi wakiwa na mapanga tu alafu wanaondoka pale wakiwa na siraha nzito tena na magazine na huku wakiacha wameua askari wanne waliokuwa na hizo siraha kwenye kituo hicho.
Sasa kwa jishi la polisi la dizaini hii, si utakuwa ni uchizi nikisema eti na mimi nilisifie kutoka moyoni!!?
Mapolisi wa tanzania kikubwa wanachoweza ni kudeal na vibaka wadogo wadogo kama wezi wa simu, kupambana na raia wema wasiokuwa na siraha huku wenyewe wakiwa wamejizatiti kwa kila namna.....!! Na pia kingine kikubwa wanachooneka kuweza sasa ni kukimbizana na watu mitandaoni waliopo hapa nchini na hii inakuwa rahisi sababu wengi wa hao askari tunashinda nao humu. Majitu yanapenda rushwa kama hayapokei mishahara, yaani mpaka imeshakuwa kawaida bila kurefusha mkono hupati msaada...Nitalieshimuje jeshi la polisi kama hili!?
HAYA NI MAONI YANGU AU HISIA ZANGU....!!
HAKUNA BINADAMU ANAYEWEZA KUNIPANGIA NIWAZE VIPI JUU YA JAMBO FLANI.