Nyie polisi tatizo lenu mmeegemea upande mmoja wa serikali na Chama tawala, hamtendi haki, hamfanyi kazi kwa weledi.. Muheshimiwa amewapa kiburi,.. Eti mnapotubambia kesi na kutaka rushwa, mheshimiwa anasema ni hela ya kubrashia viatu,.. Tukikamatwa kwa Kosa lolote mmepewa makucha ya kutulaza chini, nanyi mkapandishwa cheo,.. Mahakama sasa haina kazi kwa raia wa kawaida, bali polisi anaweza kumaliza kila kitu.
Tangu nimezaliwa, sijawahi kusikia kamanda wa polisi akiamrisha jeshi lake "mtuhumiwa apatikane akiwa hai au MFU" kwa mara ya kwanza ni kwa awamu hii, na kama walikua wakiambiwa hivyo basi cc wananchi wa kawaida tulikua hatusikii kupitia vyombo vya habari. Mmetengeneza mpasuko mkubwa sana kati yenu na wananchi wa kawaida, mmejisahau Kuwa mpo kuwatumikia wananchi.. Matukio ya kubaka, kuwaibia wananchi, kuwapora Mali zao na kuwaua pasipo na hatia yoyote pindi migogoro inapojitokeza,.. Badala ya kutuliza na kulinda amani ya raia na Mali yake, nyie mwatumia nafasi hiyo kuleta balaa zaidi,.. Hayo yashajitokeza Arusha, Dar, Mtwara, Masasi, Tandahimba na mwanza.
Ushauri... Police msilazimishe kupendwa, lazima mujihoji kwann watu wanafurahia mnapopata matatizo? Hakuna mtu ambaye anaweza kuchukia mlinzi wake,. Tunaona hata wenye mbwa, hupenda mbwa wake kwakua anaamini humpa usalama wake na Mali yake, tena humgharamia chakula, malazi na mafunzo ili aweze kutimiza majukumu yake, Iweje kwa police tusiwapende kama wanawajibika na kutenda kwa haki? Lipo tatizo, na lazima kwanza kukubali na sio kuwatishia watu wasionyeshe hisia zao.