Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Jeshi la polisi lingefaa kubinafsishwa ningependekeza ifanyike hivyo maana haiwezekani kuwanyima watu haki kila idara.inashangaza sana badala ya ulinzi kwa RAIA limekuwa jeshi la vitisho kwa RAIA.jirekebisheni acheni kutisha watu
 
Duh, naona sheria kila siku zinatungwa na serikali on the fly.... muda si mrefu tutaambiwa marufuku kufikiri vibaya!
 
Ukiwakamata uwapeleke mahakamani. Si polisi kama mnavyofanya. Wapeleke mahakamani ili mkajieleze wote.wewe mlalamikaji na yeye mshitakiwa. Hata hivyo ni ajabu kudhani kuwa kwenye msiba watu wote watalia! Wapo watakaofurahia kufa kwako, watakaosikikitika, na ambao wapo wapo kujaza msiba. Na huwezi kuwalazimisha watu kusikitika. Hilo ni suala la hisia za moyo. Na nakuhakikishia utaishia kuwatesa tu kwenye vituo vya polisi. Hawashitakiki.
Sure!!
 
Hii serekali inawafanya wananchi wanalichukia jeshi la polisi, hii inawaweka polisi kwenye hali ngumu sana wakati wa utekelezaji wa majukumu yao! Mwigulu hajiulizi kwamba ukishawahoji ndio wananchi wataanza kulipenda na kuliheshimu jeshi la polisi?

Huwezi mlazimishi binadamu kupenda kitu nje ya utashi wake viongozi waache utoto!

Dawa ya jeshi la police kurudisha heshima yake na kupata uungwaji mkono na wananchi ni kuhakikisha jeshi la polisi halitumiki kisiasa hata kidogo!

Yaani jeshi ambalo lilitakiwa kufanya kazi zake kwa majibu wa sheria na taratibu zilizolianzisha leo linatumikia chama kimoja unadhani wanachama Wa vyama vingine ni vipofu au ni wajinga hawawezi kuona?

Ngoja tuanze kuvuna tulichopanda!
Mkuu kweli kabisa huu ni utoto wa kiwango cha juu kabisa. Huwezi kulazimisha mtu ampende asiyempenda. Mwigulu acha mawazo ya kitoto. Jiulize ni wapi kama serikali mumekosea. Kwanini hujiulizi why watu washangilie kuuwawa kwa polisi? Kuna organs ngapi za vyombo vya ulinzi na usalama? Mbona hizo organs nyingine hazichukiwi? Mbona Magereza au askari wa JWTZ akifariki kwa namna yoyote watanzania huonyesha sympathy? Why only police? Jiulize maswali hayo utapata jibu ni wapi mumekosea. Dunia ya leo haihitaji kutisha watu. Mimi ni mtu huru siyo mtumwa. Ni na uhuru wa kuchagua kwa utashi wangu nimpende nani na nimchukie nani? hayo maigizo mnayowafanya ujue unazidi kuwaweka askari polisi kwenye hali ngumu. Tatufute wapi mumekosea kabla mambo hayaja haribika sana ili mchukuwe hatua za kurekebisha kuliko kutisha watu wanaotoa maoni yao mitandaoni.
 
Hayo ni maneno ya Waziri wa Mambo ya Ndani mh. Mwigulu Nchemba kuwa kwa wale wote watakaoonesha kufurahia jambo hili wataitwa kwenye vyombo vya sheria kujieleza.

My take: Kabla ya kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria kujieleza kwanini serikali isijiulize kwanini imefikia hatua mpaka polisi kuuawa wananchi wanashangilia?
NADHANI YUKO MBIONI KUNUNUA KIFAA MAALUMU CHA KUMCHUNGUZA MWANADAMU ANAYECHUKIA POLISI KUUWAWA HONGERA SERIKALI YA MWENDO KASI
 
Hii serekali inawafanya wananchi wanalichukia jeshi la polisi, hii inawaweka polisi kwenye hali ngumu sana wakati wa utekelezaji wa majukumu yao! Mwigulu hajiulizi kwamba ukishawahoji ndio wananchi wataanza kulipenda na kuliheshimu jeshi la polisi?

Huwezi mlazimishi binadamu kupenda kitu nje ya utashi wake viongozi waache utoto!

Dawa ya jeshi la police kurudisha heshima yake na kupata uungwaji mkono na wananchi ni kuhakikisha jeshi la polisi halitumiki kisiasa hata kidogo!

Yaani jeshi ambalo lilitakiwa kufanya kazi zake kwa majibu wa sheria na taratibu zilizolianzisha leo linatumikia chama kimoja unadhani wanachama Wa vyama vingine ni vipofu au ni wajinga hawawezi kuona?

Ngoja tuanze kuvuna tulichopanda!

Jeshi la polisi ni sawa na kijiwe cha CCM. Hivi kama polisi wanapokea amri kutoka UVCCM hapo tunatarajia nini?
 
CHADEMA wameungana na Mafisadi kupigania maandamano badala ya kupigania maendeleo .!!!

Aliyewaambia watanzania wanahitaji maandamano na siyo maendeleo ni nani?

Shame to you all
Wanataka maendeleo yanayoletwa kwa misingi ya kuheshimu na kutekeleza matakwa ya katiba na sheria za nchi nje ya hapo ni matatizo makubwa.
 
Kuna rafiki yangu kasema akifa Mwigulu atafunga fungate kama la simba afanyavyo anasema huyo kijana ni mchawi mpenda sifa na mwuaji
 
Kiongozi mkuu wa nchi ndie mwenye kutoa taswira ya nchi, kama anapenda kusifiwa basi utaona hata taasisi zote zitahitaji kusifiwa, nimeona bandari walikanusha kuwa hakuna upungufu wa mizigo, maana yake wananchi waseme tu kumejaa, wakaja crdb, sasa polisi. Ni sifa tu vyovyote itakavokua.
Daah! Mkuu nimecheka mchana huu nahivi sijauona vizuri inabidi niwahi Kwa mamantilie anijazie ukoko wangu !! Kwamba nimwendo wakusifu tuu!? Hiyo ndo tabia original ya mwafrica ndg yangu. Hata akiwa uchi wamnyama ukimwambia Mzee nyeti zako ziko nje unalo hilo. Anataka umwambie 'Daah! Mzee hii suti umeagiza kulekule kwa Mzee Obama nini?! Imekutoa sanaaa' hapo utakula vinono vyoote vya kifalume.
 
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.

======
Duuuuuh, kazi IPO
 
Mkuu kweli kabisa huu ni utoto wa kiwango cha juu kabisa. Huwezi kulazimisha mtu ampende asiyempenda. Mwigulu acha mawazo ya kitoto. Jiulize ni wapi kama serikali mumekosea. Kwanini hujiulizi why watu washangilie kuuwawa kwa polisi? Kuna organs ngapi za vyombo vya ulinzi na usalama? Mbona hizo organs nyingine hazichukiwi? Mbona Magereza au askari wa JWTZ akifariki kwa namna yoyote watanzania huonyesha sympathy? Why only police? Jiulize maswali hayo utapata jibu ni wapi mumekosea. Dunia ya leo haihitaji kutisha watu. Mimi ni mtu huru siyo mtumwa. Ni na uhuru wa kuchagua kwa utashi wangu nimpende nani na nimchukie nani? hayo maigizo mnayowafanya ujue unazidi kuwaweka askari polisi kwenye hali ngumu. Tatufute wapi mumekosea kabla mambo hayaja haribika sana ili mchukuwe hatua za kurekebisha kuliko kutisha watu wanaotoa maoni yao mitandaoni.
Binadamu wengine ni waajabu wakipewa dhamana ya kuongoza wanadhani watakuwa madarakani milele pia hawa walimu wanadhani kila mtu ni mwanafunzi wake wanatufanyia majaribio hatutokubali (They like treating every body like a student)
 
Hii nchi kikosi nichokipenda ni JWTZ peke yake hawana maneno na wala hamuwezi kuwasikia wapo kimya kabisaa kama hawapo vile big up saana JWTZ....Nchi yetu hata police wangekuwa kama JWTZ naamini ingekuwa nchi nzuri zaidi...

Police wamekalia kila siku matamko yasiyokuwa na mpango wowote....ningependaa sana siku moja JWTZ muwafundishe adabu hawa police
 
Jeshi letu la polisi halifungamani na chama chochote cha siasa. Wanafanya mambo yao kwa weredi wa hali ya juu sana, Tuendelee kuwaunga mkono. Wapunguze tu matamako kwenye vyombo vya habari maana nchi yetu haina tishio lolote la usalama kama wanavyojaribu kutwambia. Nimesikitika kuona hata kampuni ya SGA ikitoa security alert kwa wateja wake, eti tarehe 1 September kutakuwa na hali tete ya usalama.... this is a big lie!
 
maoni mengi yaliyotolewa na wachangiaji mitandaoni yanatoa hisia ya kuwepo mahusiano duni kati ya walinzi wetu na wananchi. nilitegemea polisi wangeyatumia maoni hayo hasi dhidi yao kama changamoto badala ya lawama. ukiona adui yako anakusifia jihadhari.
 
Mkuu kweli kabisa huu ni utoto wa kiwango cha juu kabisa. Huwezi kulazimisha mtu ampende asiyempenda. Mwigulu acha mawazo ya kitoto. Jiulize ni wapi kama serikali mumekosea. Kwanini hujiulizi why watu washangilie kuuwawa kwa polisi? Kuna organs ngapi za vyombo vya ulinzi na usalama? Mbona hizo organs nyingine hazichukiwi? Mbona Magereza au askari wa JWTZ akifariki kwa namna yoyote watanzania huonyesha sympathy? Why only police? Jiulize maswali hayo utapata jibu ni wapi mumekosea. Dunia ya leo haihitaji kutisha watu. Mimi ni mtu huru siyo mtumwa. Ni na uhuru wa kuchagua kwa utashi wangu nimpende nani na nimchukie nani? hayo maigizo mnayowafanya ujue unazidi kuwaweka askari polisi kwenye hali ngumu. Tatufute wapi mumekosea kabla mambo hayaja haribika sana ili mchukuwe hatua za kurekebisha kuliko kutisha watu wanaotoa maoni yao mitandaoni.
Excellent mkuu
 
Vitisho vimezidi tutawapendaje hao police, kama mtu anatoa maoni tu anatishiwa kushtakiwa wakati ni haki yake ya kikatiba, kama police wanamfyatulia risasi raia ambaye hana silaha ya kujihami, atapendwaje huyo police? Watu wana uchungu mioyoni mwao na uchungu huu ni silaha hatari zaidi ya hayo mabomu na bunduki wanazotuonyeshea huku barabarani.
 
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.

======
Kuna mtu aliuliza swali,je wale waliocheka kimoyomoyo nao watakamatwa?nikabak kucheka tu
 
Back
Top Bottom