Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Wanaowabeza Polisi mitandaoni ‘kushughulikiwa’

Hakuna sheria inayolazimisha kumuonea huruma adui yako.
 
Vitisho na matamko yasiyo na kichwa wala miguu havitasaidia kurudisha heshima ya polisi kutoka kwa wanachi. Badala yake watazidi kudharaulika kila kukicha na hata mkiwafunga wanaobeza polis, mtafunga wangapi.. because no body care about police business anymore
 
Mmh napata shaka kuamini kama huyu nae ana upeo mdogo wa kufikiri..
 
tuambie watafanyaje?,weka hoja hapo. unakuta mtu kafungua email fake, namba ya simu fake kwanza alishaitupa miezi sita iliyopita, akaunt jf fake, jina lake halijulikani, uhalifu kafanyia internet cafe sio kwenye simu yake, unampataje mtuhumiwa? hawa ambao wanatapeli pesa katika makampuni kama mpesa,aitel nk hawpatikan wote,anatumia line na kutupa hawapatikani. juzi tu kuna mtu nilimwona ofisi ya vodacom anaomba msaada ametapeliwa fedha kupitia mpesa wakamwambia hawawezi kum trace mhalifu coz wanatumia line na kuzitupa ,
Usitupe mtama kwenye kuku wengi.
 
Hehe. Sasa serikali imefikia hatua ya kudhani ina mamlaka ya kutawala mpaka hisia za watu/wananchi. Kwamba sasa serikali ndiyo itatoa amri na maelekezo ya ama kufurahia au kuchukia jambo flani linapotokea. Hisia za watu/wananchi sasa hazitokani na utashi na maono ya mtu mmoja mmoja bali maelekezo yanayotolewa na serikali. Serikali imefikia hatua ya kuuliza watu kwa nini wanafurahia au kwa nini hawafurahii na kutoa adhabu kwa jinsi ambavyo watawala wanaona inafaa. Hizi ni sifa za utawala wa kiimla.
 
CHADEMA wameungana na Mafisadi kupigania maandamano badala ya kupigania maendeleo .!!!

Aliyewaambia watanzania wanahitaji maandamano na siyo maendeleo ni nani?

Shame to you all
Ninyi malaika leteni hayo maendeleo, kwani lazima myategemee majizi?

Leteni maendeleo na hayo majizi pelekeni mahakamani au yachomeni moto.

Na fikra zako kengeufu peleka kwenu.
 
Ananikumbusha korea ya kaskazini alipokufa kim jong il,pale kwenye msiba lazima ulie kwa juhudi na kuonekana una hudhuni sana,ole wako shushushu wakukute haulii,
wanakuweka kizuizini wewe na family yako yote na haurudi uraiani ng'o..
 
Wanaaonyesha Furaha? Furaha inaonyeshwaje? Inapimwaje? Watu wengine bhana
 
CHADEMA wameungana na Mafisadi kupigania maandamano badala ya kupigania maendeleo .!!!

Aliyewaambia watanzania wanahitaji maandamano na siyo maendeleo ni nani?

Shame to you all
Rudi tu kwenye mada, ili usiwe irrelevant. Sawa?
 
Mimi Kwa Maoni Yangu, Mwigulu Ni mojawapo ya watu ambao Kwa Tukio Hili wanafaa wachunguzwe, Hili tukio lina Kila dalili ya Kuwa Lilipangwa kwa siasa. Masikini Watoto wa Watu, Askari wale wanne wanaweza Kuwa walitolewa Kafara na Watu waovu sana Kisiasa. Mungu Sii Mwanadamu Ukweli Utajulikana!
Unakumbuka kijana aliyemwagiwa tindikali kule Igunga? baadae akawa mdoli wa Mwigulu anapita nae kila mahali kumuonyesha na kusema CHADEMA wamemfanya hivi!
Masikini Tanganyika.
 
Hehe. Sasa serikali imefikia hatua ya kudhani ina mamlaka ya kutawala mpaka hisia za watu/wananchi. Kwamba sasa serikali ndiyo itatoa amri na maelekezo ya ama kufurahia au kuchukia jambo flani linapotokea. Hisia za watu/wananchi sasa hazitokani na utashi na maono ya mtu mmoja mmoja bali maelekezo yanayotolewa na serikali. Serikali imefikia hatua ya kuuliza watu kwa nini wanafurahia au kwa nini hawafurahii na kutoa adhabu kwa jinsi ambavyo watawala wanaona inafaa. Hizi ni sifa za utawala wa kiimla.
Keshokutwa itakuw marufuku mtu kuvaa viatu. Watawala wamepoteza uwezo wa kufikiri kabisa.
 
sisi kina gogo la shamba tulishasema miaka hii mitano ni ya kusikia na kuona mambo mengi ya ajabu kutoka kwa viongozi tuliowategemea
 
Mbona viongozi wanatukuzatukuza kufanya mambo kiubababe?, hivi hawa wanatafuta heshima kwa umma au wanatafuta kuabudiwa?
 
Hayo ni maneno ya Waziri wa Mambo ya Ndani mh. Mwigulu Nchemba kuwa kwa wale wote watakaoonesha kufurahia jambo hili wataitwa kwenye vyombo vya sheria kujieleza.

My take: Kabla ya kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria kujieleza kwanini serikali isijiulize kwanini imefikia hatua mpaka polisi kuuawa wananchi wanashangilia?
Dah, tulipofikia ni pabaya
1. Kufurahia jambo ni hisia na wala si maamuzi, na hisia hutokana na kilichotokea kabla ya jambo linalofurahiwa....
2. Inawezekana ni muendelezo wa kusifia tu wanaotuzunguka
3. Tumezowea kusikia wasifu mzuri wa watu ila ikiwa vinginevyo tunaona haiwezekani iwe hivyo

Nadhani ingekuwa vizuri kama tungetafuta chanzo cha furaha hiyo .... maana kwenye jamii yetu kufurahia kifo cha mwenzio si kawaida...
 
Kwa mtazamo wangu Police waliouwawa wamekufa eneo lao la kazi na wakiwa na sare zao za kazi inaumiza sana moyo kwa wakuu wao,wazazi wao,familia zao na marafiki wao,,kwangu hawa ni MASHUJAA.

Mungu na awapumzishe kwa amani na Watanzania wote tuwaombee familia zao ktk kipindi hiki kigumu
 
Back
Top Bottom