Wanaotaka kuanza kusoma CPA, karibuni tushauriane

Kwa mnaotaka kuanza Review Classes for May exams, muda ni sasa wameanza tangu last week so hatujachelewa. Twendeni tukapambane hadi kieleweke wakuu🙏
 
Dada financial services Kwanza niseme nakupenda. Nakuona humu ndani ni muda sasa.
Napenda tu the way ulivyo.

Tukirudi kwenye mada CPA (T) naweza kusema kwasasa ina soko. Sasa hivi huwezi kuwa mhasibu kama hauna CPA.

Hata kama una Degree ya uhasibu bado huwezi kuwa mhasibu, ukiajiriwa Serikalini utatambulika kama afisa hesabu sio mhasibu.

Mimi nilianza kuisotea tangu 2016 bahati mbaya bado sijaipata ila nipo hatua za mwishoni kuhitimu.

Session huwa mbili kwa mwaka, Ni May na November. Pia kuna mid session ukitaka March na August Ada za Mid Session zimechangamka Pepa moja unalipia hadi laki 3. Kama upo Dar ni vizuri mimi nimesoma CPA kwa muda wote huo nikiwa mkoa wa Rukwa. Mitihani nilikuwa nafanyia Mbeya Pale Sokomatola Mkapa Hall.

Nilishawishika kusoma hii kitu baada ya boss wangu aliyenipokea mwanzo alikuwa Mhasibu Mkuu now baada ya waraka ni Afisa hesabu.

Faida za kuwa na CPA ni nyingi sana, Mosi ukiwa nayo mshahara wa kuanzia kazi TGS F then unakuwa certified in Public Muajiri ansearch jina NBAA anapata data zako kiusahihi no longolongo.

Wahasibu ni kama wanasheria now huwezi kuwa mwanasheria bila kupitia Law School.

Mungu anisaidie nipate na ACCA
Mkuu ulifanikiwa? Naona rukwa hakuna center vp ulikua unasoma online au wewe kujisomea Tu private
 
La saba huwezi kuruhusiwa kusoma CPA, hata form four kama hana ufaulu wa hesabu na English hawezi kusoma CPA. Kwa Tanzania CPA wameirahisisha sana vigezo vya kuingia, kwa nchi kama South Africa ambako inaitwa CA (Chartered Accountant) minimum entry requirement ni degree ya uhasibu tu yaani iwe uhasibu pure ambayo ni financial accounting.
Kwahyo unaeza ukawa na degree ya mambo mengne tofauti na uhasibu na ukaweza kusoma CPA kwa TZ or.?
 
Habari wakuu!

Kwa wanotaka kuanza kusoma na waliosoma CPA karibuni mtushauri lolote, kwanza kabisa nahitaji kufahamu,
1) Intake ni mara ngapi kwa mwaka, yaani unaweza anza mwezi gani? Now tunaingia mwezi June je intake nyingine inaanza lini?

2) Vigezo vya kuanza ni vipi? Najua kuna levels mfano foundation, intermediate na final, Je kwanini wengine waanzie foundation level na wengine Intermediate?

3)Je kuna favor yoyote kwa mtu aliyesoma masomo yenye uhasibu kidogo mfano Finance, Banking nk? Je atafanya mitihani mingapi ya foundation?

4) Gharama zake zipoje hasa?

5) Center ipi ni nzuri kwa Review Classes kwa Dar es Salaam na hata kwa walioko mikoani nk?

Karibu mshare na sisi lolote kuhusu CPA wakuu, tutaappreciate👏
Watafute Wexito Consulting Group, wako vizuri kwenye mambo ya CPA
 
Wakuu naombeni ushauri kidogo...mm ni mwalimu mwenye Elimu ya diploma na nmeamua kijiendeleza ki masomo na by now nasoma Accounting and finance mwaka wa mwisho...Shida yangu ni kutaka kujua ni Department gan inafanya vizur saiv kati ya Uhasibu au ukaguzi wa ndani(Internal audit) katika level ya halmashauri.
 
Kwanza hongera kwa kujiendeleza. Mimi sio mhasibu ila nitakujibu kwa nnavyozijua halmashauri..

Ukiwa mhasibu ni madra kupata posho

Ukiwa internal auditor sometimes unaweza toka nje kukagua miradi ukapata tupesa twa vocha.

Ukiwa mhasibu ni rahisi kupata hata 10% ukipitisha malipo ya mtu.

Ukiwa mhasibu utakua unapelekeshwa na DT na kama mfumo ukiwa mbovu lawama zote kwako.

Sasa kazi ni kwako kuamua!

All in all haijalishi utapangiwa wapi, kazana ukimaliza upate CPA hiki ndio cha muhimu kwako. Pia ukishapata degree au ukipata cpa hama halmashauri sio pazuri.. tafuta mashirika ya umma uhamie uko.. tarura, ruwasa, tanapa nk nk!

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kuhama kwenda kwenye mashirika process zake zinakuwaje
 
Heshimu fani za watu Mkuu.
Watu wengine kama machizi tu. Leseni yenyewe hata mtu asiejua kusoma na kuandika,hupata. Ila anateseka sana mpaka afanikiwe.

CPA ndo la saba akasomee!!!! Dah! Ila hili huweka wazi watu na akili zao. Wanaoijua,wanajua. Wengi wanataka,lakini uhakika wa kupata hawana.
Na ndo maana ukiitafuta kwa kulipwa mshahara tu,haina msaada. Kwa watu wanaoijua, huwezi kuivamia bila basics za uhasibu.
Wameifananisha na wale wanaomaliza F4,eti wanaenda kusomea kuwa wafamasia miaka 2. Mfamasia wa kweli,anajua
 
Kwani mkuu CPA inataka mtu awe na elimu gani? I mean kwa mujibu wa NBAA.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom