Ushauri kwa serikali: Iandae mikakati ya kudhibiti soko la silaha na uingizaji silaha baada ya mgogoro wa Ukraine

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Mgogoro wa Russia na Ukraine umepita mwaka mmoja sasa na huenda usiishe hivi karibuni. Nchini Ukraine hivi sasa wapo watu ambao wafanya kitu chaitwa mavuno yaani kuokota silaha kwa ajili ya kuzifanyia matengenezo, kuzisafisha kwa ajli ya kuziuza baadae.

Mara nyingi silaha hizi kupitia wauzaji hawa |(arms Dealers) huishia katika mikono isiyo sahihi kama kwa makundi ya kihalifu, waasi na hata watu binafsi mwa ajili ya matumizi mbalimbali. Tangu mgogoro wa Russia na Ukraine uanze mwezi February mwaka jana Ukraine imepokea msaada wa silaha na vifaa mbalimbali vya kijeshi vyenye thamani ya mabilioni ya dola kutoka zaidi ya nchi 28 za Ulaya.

Silaha hizo ni zile kubwa kubwa na silaha ndogo ambazo ndizo lengo la mada hii kuziongelea silaha hizo.

Silaha kama UAVs huenda zikachukua muda kujifunza kuziongoza ingawa zaweza kuwa ni silaha hatari kutumiwa khasa barani Afrika.

Lakini vifaa kama "body armour/ helmets," silaha za automatic rifles, machine guns, assault rifles, sniper rifles, sub machines guns, pistols na amo zake, ni mfano dhahiri kwamba silaha izi zikiingia katika eneo lolote la nchi khasa zile zenye migogoro na ghasia itapelekea kuleta maafa makubwa.

Barani Afrika sasa hivi kuna migogoro kadhaa khasa mgogoro wa majeshi ya Congo DRC na waasi wa M23, mgogoro kati ya majeshi ya Sudan na vikosi vya RSF (Rapid Support Forces), tishio la magaidi wa Al Shabab, migogoro katika eneo la Sahara khasa nchini Mali, Burkina Faso na nchini Senegal kote kuna hali ya kuwepo uwezekano wa silaha kuingizwa kwa silaha zaidi katika nchi hizo ili kuchochea vita na mauaji.

Afrika ndo eneo ambalo kwa sasa limekaliwa kooni kutokana na msimamo wake wa kutoegemea upande wowote katika mgogoro wa Russia na Ukraine. Hivyo basi silaha ambazo zimekuwa zavunwa kutoka eneo la vita nchini Ukraine kuna uwezekano mkubwa zikapelekwa kuuzwa katika maeneo mbalimbali barani Afrika na nchi zingine duniani zenye migogoro.

Ipo taarifa kuwa nchini Rwanda raisi Paul Kagame amewafukuza kazi wanajeshi wapatao 244 kwa utovu wa nidhamu. Habari hii haijawekwa sawa ingawa vyanzo kadhaa vya uhakika vya habari vimedokeza kuwa wanajeshi hao wakiwemo wakuu wa majeshi na mkuu wa idara ya ujasusi wa ndani wote wamefukuzwa kazi mara moja kwa utovu wa nidhamu.

Je, kwa nchi kama Rwanda askari hawa walofukuzwa kazi na wenye mafunzo bora kabisa kutoka vyuo mbalimbali duniani vikiwemo vyuo vya Marekani wataachiwa tu wazurure mitaani bila sababu maalum?

Sheria yasema wazi kuwa wanajeshi hao wanawajibika kusalimisha vifaa na silaha zao zote ambazo ni mali ya jeshi na pia kwa mujibu wa vyanzo vya habari raisi Kagame amesema kuwa askari hao pia wataondolewa rasmi mafao yao.

Je, wanajeshi hawa wataishi tu kama digidigi mitaani wakizurura bila kazi?

Sasa hapo nimeongelea kidogo kuhusu jeshi la Rwanda kwa mfano wa jeshi ambalo ikiwa silaha zisizo na udhibiti zitaweza kuwa zapenya na kuingia na kufikia mikono ya walokuwa askari wazoefu je, hali ya usalama katika eneo la maziwa makuu itakuwaje.

Hivyo basi, ningependa kutoa ushauri kwa serikali ya Tanzania kuanza kuweka mikakati ya udhibiti hali ya usalama mipakani na kujiandaa na biashara haramu ya silaha pale zitapokuwa zikitafuta pa kuingilia ili kuwafikia wanunuzi.

Kuna kipindi wakati wa utawala wa awamu ya tano watu waliambiwa kusalimisha silaha zao kwa polisi na zoezi lile lifanyika ingawa haikujulikana ni silaha kiasi gani zilisalimiswa kwa polisi. Je, tangia wakati ule watu wale walosalimisha zilaha zile hwatakahitaji kuwa na silaha zingine ambazo ni sa kisasa zaidi?

Hivyo ni jambo la muhimu kwa serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuhakikisha hali ya mipakani na udhibiti wa silaha zisiingizwe kiholela nchini na kuwahakikisha usalama raia wa Tanzania na mali zao.
 
Nimemsikia mtu akisema "Who cares".

Najiuliza amaanisha nini.

Twaachia bandari moja ya mali (assets) za nchi kwa wageni.
Ni KICHAA kama Mimi pekee ambae naweza ingia na kuvunja mikataba ya hovyo!!

Na wala sitaogopa yeyote tena hao waarabu ndio hata unywele hauchezi!!

Kila mkataba unarudi mezani!!
 
Ni KICHAA kama Mimi pekee ambae naweza ingia na kuvunja mikataba ya hovyo!!

Na wala sitaogopa yeyote tena hao waarabu ndio hata unywele hauchezi!!

Kila mkataba unarudi mezani!!
Kwa sasa wamejipanga uzuri ni muhimu kujiandaa kwelikweli.

Jana nimeona news kuhusu walofanyiwa wamasai wa Loliondo na Amnesty International wametoa habari huko nje.

Mambo hayo (ya Loliondo yalipita kimyakimya).

Pia twaachia taarifa za kibaolojia (biometric Data) kwa wageni watutengenezee kwa kizingizio cha kutengeneza Universial ID card.

Ni wakati wa kujiandaa na silaha za AI Diana akija kama toto zuri la kizungu.
 
Kwa sasa wamejipanga uzuri ni muhimu kujiandaa kwelikweli.

Jana nimeona news kuhusu walofanyiwa wamasai wa Loliondo na Amnesty International wametoa habari huko nje.

Mambo hayo (ya Loliondo yalipita kimyakimya).
Mimi wala sitohangaika pekee yangu!!

Kama ni Baraza ala mawaziri lilipitisha mikataba ya hovyo mimi nitaitisha Baraza la usalama la taifa na nchi tuichambue mikataba upya na kufanya marekebisho na itatangazwa kuwa JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA imepitia mikataba yote na kufanya mabadiliko yenye tija KWA JAMHURI na Taifa KWA ujumla,yaani sisemi kwamba Mimi kama namba moka bali Baraza la usalama wa taifa kupitia ujasusi wa kiuchumi limeona kuna haja ya kufanya mabadiliko yenye tija kuendana na kasi ya uchumi wa SASA!!

Halafu nitajificha kwenye neno jamhuri wala SIO jina langu yaani nakuza neno JAMHURI ya MUUNGANO kama ndio kiini cha muelekeo wa mabadiliko hakuna "TANZANIA YA FULANI WALA YA FULANI"BALI JAMHURI IMEFANYA HIVI AU VILE!!
 
Hizi habari muhimu sana..

Congo Kinshasa tupo IMARA
Njia za panya, bandari zetu na viwanja vya ndege vya misituni vya "airstrip" (kwa ndege ndogo) ni sehemu ambazo ni rahisi sana kuingiza silaha.

Dunia kwa sasa ipo kwenye hali ngumu kila nchi imeanza kuangalia ndani kuna hali gani na mipakani kupo vipi kuasalama.
 
Back
Top Bottom