Malalamiko ya wanafunzi kozi za Afya; Barua ya wazi kwa Waziri Afya na Elimu

cokusoma

New Member
Feb 3, 2022
1
1
BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA ELIMU NA WAZIRI WA AFYA.

NAKALA: OFISI YA WAZIRI MKUU
OFISI YA KAMATI YA BUNGE HUDUMA ZA JAMII
BARAZA LA MAFUNZO YA UFUNDI (NACTE)
TAHLISO
VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA

UTANGULIZI:
Barua hii ya wazi imeandikwa mahusi na sisi wanafunzi wa Kitanzania tunaosomea fani za Afya kwa ngazi ya diploma kutoka kwenye vyuo vya serikali na vyuo binafsi. Kwa umoja wetu tumeamua kupaza sauti baada ya kuona viongozi wa idara ya mafunzo na hususani Mkurugenzi msaidizi wa mafunzo Wizara ya Afya kuzidi kutukandamiza.

Tunaamini, Wizara tajwa hapo juu kwa ngazi ya Waziri na taasisi zingine hazifahamu mambo haya yanayoendelea ambayo kwa kiwango kikubwa yanapelekea viongozi Idara ya mafunzo Wizara ya Afya kufanya maamuzi yanayotuumiza, hili limekuwa la muda sana na matatizo ni mengi pia. Tunaona ni wakati muafaka kumuomba Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano atusaidie.

Tunaona pia NACTE haitutendei haki katika kutusimamia na kututeteta kwa msingi wa kuwa hatuyaoni matatizo kama haya yakitokea katika vyuo vinavyotoa mafunzo mengine mbali na haya ya Afya. Kwa mfano, tukiuliza kwa wanafunzi wenzetu wa CBE, IFM CHUO CHA MAJI nk hatusikii mazingira magumu kwa wenzetu wanaosoma vyuo hivyo. Mara kadhaa tukiuliza baadhi ya masuala yanayotukandamiza, inaonekana yameamuliwa na wakaurigenzi wa wizara bna hayafahamiki NACTE. Hadi tunajiuliza, Je! tumefanya makosa kujiunga na fani hizi za Afya?.

Tunaona kuna shida za kiutawala katika idara ya mafunzo Wizara ya Afya, tunakuomba mheshimiwa Waziri Mkuu ikikupendeza wewe ni mzazi wetu uunde tume huru kuchunguza haya. Tunapendekeza pia barua hii ichagize kupatikana kwa hadidu za rejea. Zimekuwepo jitihada kadhaa za kusadiiwa na wakuu wetu wa vyuo na kupaza sauti ili kutatua changamoto hizi lakin bado hali ni mbaya. Tutaainisha changamoto za muda mfupi na muda mrefu zinazotukumba.


CHANGAMOTO YA KWANZA:
Kuzuiwa kufanya mitihani ya wizara mara kwa mara bila sababu ya msingi. (Barua ya Wizara ya tarehe 27/01/2022 yenye kumbukumbu namba LB.205/262/01A/96 iliyosainiwa na Dr. Fadhili Lyimo kipengele cha tano imetoa katazo la wanafunzi kuzuiwa kufanya mitihani mwezi wa tatu. Matatizo ni kama yafuatavyo (Barua imeambatanishwa);

1). Wanafunzi wa Mwaka wa pili (NTA Level 5) waliofanya mitihani mwezi wa 12/2021 na kupata Supplementary wamepewa maelekezo ya barua na Mkurugenzi msaidizi wa Wizara kuwa hawatofanya mitihani hiyo hadi mwezi wa nane (8) mwaka huu.
Sisi tunauliza, kwa nini maamuzi haya ya kikatili yanafanyika wakati ipo fursa/nafasi yakufanya mitihani hiyo mwezi wa tatu (3) mwaka huu pamoja na wenzetu? Ni kwanini tunyimwe fursa ya kuendelea na masomo? Mtaala unazungumzia kawaida kupewa mtihani (Supplementary exam) huwa ni ndani ya wiki tatu baada ya matokeo kutoka, Je? Kwa kama mwaka jana 2021 iliwezekana kufanyika mitihani hiyo ya marudio ndani ya wiki chache nini kinakwamisha mitihani hiyo kufanyika mwezi wa tatu (3) mwaka huu?
Ukizingatia kuwa mitihani ya mwezi wa 12 mwaka jana 2021 ilitungwa kwa dharula na ilifanyika bila kikwazo. Kama wanafunzi tuko tayari kufanya mitihani ni kwa nini viongozi wa idara ya mafunzo wasitutendee haki kwenye hili? Mhe Waziri, sisi tunatoka katika familia za kimaskini, muda wetu wa kusoma ni uwekezaji wetu, wa wazazi wetu na Taifa kwa ujumla. Ni kwa nini iwe kawaida kusoma muda mrefu bila sababau za msingi? TUNAIOMBA NACTE WATUPE NAMBA ZA MITIHANI ILI TURUDI KUFANYA MITIHANI YETU TUNATAMANI KWENDA HATUA NYINGINE.

2). Kuna maelekezo mengine kuwa wanafunzi wote wa mkupuo wa Septemba na waliojifunza kutoka mwezi wa kumi mwaka jana (Repeat module) pamoja na wale wa marudio (supplementary exam) na walio tegemea kufanya mtihani mwezi wa tatu(3) kuzuiliwa kufanya mitihani kwa tamko la mkurugenzi msaidizi kwenda kwa Wakuu wa vyuo vyetu vya Afya kuwa mitihani hiyo itafanyika mwezi wa nane mwaka huu.

Kama mwanafunzi aliyejianda kwa mitihani na kukamilisha vigezo vyote pamoja na kulipa ada ya mitihani ni kwanini azuiliwe kufanya mitahani hiyo?, je! amekiuka sheria za mtaala?, kwanini aachwe hadi ajiandae kabisa na kuja kuzuiliwa ghafla wiki chache kabla ya mtihani? Kuna ubaya gani mwanafunzi huyu akifanya mtihani au mitihani ni michache? au mwanafunzi huyu hatakiwi kuhitimu? au kuna kitu tumewakosea waratibu wa mafunzo? Mbona hawatuonei huruma sisi na wazazi wetu wanaouza mali zao ili kutusomesha. TUNAOMBA NACTE ITUPATIE NAMBA ZA MTIHANI ILI TUFANYE MITIHANI NA TWENDE HATUA NYINGINE. Tumejiandaa na uonevu wote huu unafanywa na idara ya mafunzo ya wizara ya Afya.

HITIMISHO:
Imekuwa ni kawaida ya sisi kwa wanafunzi kuzuiliwa kufanya mitihani pasipo na sababu za msingi, tunasikitika hili linachangizwa na maamuzi ya viongozi wa wizara Afya. Kadhia hii pia hujidhihirsha kwa wasimamizi wa Wizara ambao wakija vyuoni wanatafuta sababu ya wanafunzi kutokufanya mitihani. Hata pale ambapo NACTE imetoa namba za mitihani bado wasimamizi wa wizara hutafuta sababu ya kutuzuia kufanya mtihani. Inaumiza sana. Je shida hii inatokea katika vyuo vingine visivyo vya Afya?.

CHANGAMOTO YA PILI:
Mabadiliko ya mara kwa mara ya kimaamuzi. Tunaona hakuna utulivu wa kimaamuzi husasan yanayohusu masuala ya wanafunzi na yanayofanywa na idara ya mafunzo wizara ya Afya. Hatuna uhakika wa maamuzi gani yataletwa kesho. Ushirikishwaji wetu na michango yetu ya mawazo umekuwa ni mdogo
Mifano;

1). Limetolewa tangazo la kurudi chuoni tarehe 1/2/2022. Mkurugenzi msaidizi ameagiza wanafunzi wenye mitihani ya marudio kutoendelea na masomo ya ngazi ya sita (Level six) kuanzia mwezi wa hadi wa 11 muhula mpya wa Sepetemba unapoanza.. Maamuzi haya yanatuumiza, tupo kwenye mwaka wa mwisho (Exit level) ni kwa nini tupoteze mwaka mzima nyumbani?. Kama lipo kundi la wanafunzi wanaofanya mitihani mwezi wa tatu ni kwa nini na sisi tusifanye mitihani hyo?

2). Wanafunzi waliofaulu kulazimishwa kurudi chouni na kuanza Level six kwa tangazo la chini ya wiki moja.
Sisi tunashangaa, Wizara ilikuwa na nafasi ya kupanga ratiba ya masomo mara baada ya mitihani kuisha mwezi wa 12 mwaka jana na kutoa taarifa hiyo mapema. Kama muhula unaaza kwa ghafla na wakati wazazi wetu hawajapata nafasi ya kuaanda Ada itakuwaje?. Na kama wanafunzi wanye mitihani ya marudio wanazuiliwa kuendelea je hii haraka ni ya nini huku tukiacha kundi kubwa nyuma yetu. Ukizingatia kuwa kama mzazi atachelewa kulipia Ada zaidi ya wiki mbili sitoruhusiwa kuendelea na masomo kutokana na kuchelewa kuripoti.
Ifahamike kuwa lipo darasa la Mwezi wa 4 linaloanza kwa wanafunzi wa Level ya 6 muhula wa kwanza. Darasa hili litatokana na wanafunzi wa Level ya 5 muhula wa pili wanaofnanya mithani yao mwezi wa tatu. Ikumbukwe kuwa kama darasa litanza mwezi wa pili na jingine mwezi wa nne baada ya Level 5 muhura wa pili mkupuo wa march , kufanya mitihani ya mwezi wa tatu na kuanza level six muhula wa kwanza. Je vyuo vinaweza kuendesha madarasa mawili kwa wakati mmoja yaliyopishana kwa miwezi miwili tu. Kwa maana ya kuwa mwezi wa 5 kuna vyuo vitakuwa na madarasa mawili ya Level 6 muhula wa kwanza.
Tunapendekeza wanafunzi wenye supplementary wafanye mitihani yao mwezi wa tatu na kuanza pamoja mwaka mpya Level 6 na wenzao wa Machi baada ya matokeo kutoka.Hii itasaidia kuwapa
nafasi ya maandalizi wale walio faulu, pia itapunguza mkanganganyiko wa kuwa na level six muhura wa kwanza madarasa mawili yanayopishana miezi miwili. Tunaamini ni maamuzi sahihi kuunganisha darasa la march jipya na sisi tuliopata changamoto.

3). Yapo maamuzi ya mara kwa mara ya kuwakandamiza wanafunzi mathalan kutofanya mitihani kwa kigezo cha intake kwa tofauti. TUNAOMBA NACTE ITUANGALIE KAMA INAVYOANGALIA VYUO VYENYE KOZI NYINGINE. Kama mtaala na mitihani ni ileile utofauti wa intake usiwe kigezo vya mwanafunzi kutokufanya mitihani.

CHANGAMOTO YA TATU:
MABADILIKO YA MARA KWA MARA YA KIMUOGOZO YA MITAALA. Kumekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara kiutawala na kimuongozo tutatoa mifano kadhaa.
1). MABADILIKO YA KANUNI ZA MITIHANI.Yamefanyika mabadiliko ya kanuni ya mitihani mwaka 2020 na kuanza kutumika 2021 mabadiliko haya yanachochea sana kuonekana wanafunzi wanafeli sana (Discontinue). Mtaala wa nyuma ulimruhusu mwanafunzi mwenye repeat module kufanya mitihani mara mbili ( second seat). Kwa nafasi hii kwa mwanafunzi imekatazwa. Hii inapelekea Discontinue kuwa nyingi sana vyouni. Swali ni Je! Kwa nini mwanafunzi mwenye supplementary apewe nafasi mbili na wenye repeat module apewe moja? Kama mnaamini nafasi ni muhimu katika kujifunza, kwa nini mnawanyima wanafunzi nafasi hiyo. TUNAPENDEKEZA WIZARA ILIANGALIE UPYA HILO.

2). MABADILIKO YA MIHULA YA UDAHILI NA KUSABABISHA WANAFUNZI KUSOMA MUDA MREFU. Imekuwa ni kwawaida sana kwa mwanafunzi wa Diploma kusoma mda mrefu sana vyuoni, hii inatokana na muundo wa udahili na kuchochewa na maamuzi ya wizara ya Afya kuwasubirisha wanafunzi muda mrefu majumbani ili wasifanye mitihani ya marudio. Kwa mfano, hatuoni Daktari (MD) akichukua muda mrefu kusoma .Hatuoni shida hiyo pia (Ya kuchukua muda mrefu kusoma kutokana na kusbiri mitihani ya marudio) kwa wanafunzi wanaochukua fani nyinginezo. Je! ni kwa nini iwe ni vyuo vya Afya tu?.

Kwa muda sasa hali imekuwa mbaya zaidi kwa sisi tunaosoma vyuo vya serilkali ambapo hakukuwa na March Intake .Mda wa kusoma unakuwa mrefu sana. Wizara na NACTE mtuonee huruma. Wizara ya Afya inatukatisha tamaa sana. Je mtaki tuhitimu kozi za Afya?. Kwa kuondolewa udahili wa mwezi wa tatu kadhia hii ya kusoma muda mrefu inakwenda kuwakumba wenzetu wanasoma vyuo binafsi. kimsingi kuna sheria nyingi sana zinazoibuka kila leo na zinatumika kutukandamiza wanafunzi, tuna kosa gani?



CHANGAMOTO YA NNE:
Kuhamishwa vituo vya kufanyia mitihani. Kutoka kwenye vyuo vyetu kwenda kwenye vyuo vingine. Wizara ya Afya kuanzia mwaka jana imeanza utaratibu wa kutuhamisha kwenda kufanya mitihani kwenye vyuo vingine. Je kua shida gani kufanyia mitihani katika vyuo vyetu. Wakati mwigine tumehamishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine.Nzega au kagera kwenda Sengerema kufanya mitihani ya wiki moja. Hii yote inatokana na nini. Changamoto za gharama tunaoingia za usafiri na malazi zinatumiza wanafunzi. Kama tuliweza kufanaya mitihani yetu ya majaribio CA katika vyuo vyetu. Je mwanafunzi ambaye hatoweza kumuda gharama ashindwe kufanya mitihani. Tunawaonea huruma wazazi wetu.

Mwisho kabisa tunapendekeza yafuatayo;
i) Tusaidiwe kufanya mitihani yetu ya marudio mwezi wa tatu ili tuendelee na Level nyingine. Kwa upande wtu tupo tayari na tumejiandaa na mitihani hiyo.

ii) Wizara ya Afya hususani idara ya mafunzo iangaliwe namna ambayo imekuwa ikifanya maamuzi yake ya kutukandamiza. Maamuzi mengi yaliyotolewa yamejikita katika kukwamisha na kuumiza wanafunzi . Tumetoka familia za kimasikini wazazi wetu wanategemea tumalize tukatumikie taifa mtuonee huruma. Hamjali Ada tunazozipata kwa shida na muda tunaotumia kusoma.

iii) Tunamumba Mzazi wetu Waziri Mkuu aunde tume huru iundwe ya kuchunguza na kutafakari changamoto zinazotukumba wanafunzi wa vyuo vya Afya. Tume hiyo ipite vyuoni kutuhoji na tuko tayari kutoa ushirikiano.

iv) Tunaiomba NACTE itutendee haki ya kutusimamia kama inavyosimamia vyuo vingine vya fani nyingine. Tukiuliza wenzetu wanaosoma kozi nyingine hawakumbwi na changamoto kama hizi. Tunaomba mtuokoe na maamuzi ya Wizara yanayotukandamiza

v) Viongozi Wizara ya Afya idara ya mafunzo wajitathmini na watafakari kama wamekuwa wanatutendea haki.

Tunaomba, viongozi wa serikari wapokee maoni na malalamiko yetu, wafanye uchunguzi wao ili kubainisha kama haya tunayoyasema ni kweli au sio kweli. Wafanye tathimini ya changamoto nyingine tunazokumbana nazo. Tunaomba kuwasilisha.

IMEANDALIWA NA WANAFUNZI WANAOSOMA KOZI WA AFYA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA VYUO BINAFSI NA SERIKARI.
NB: Tumeambatanisha nakala ya barua inayotukataza kuridi chuoni pamoja na nakala ya barua hii ya wazi
 

Attachments

  • BARUA, WAKUU WA VYUO, MATOKEO 27012022.pdf
    211.9 KB · Views: 59
  • MALALAMIKO YA WANAFUNZI KOZI ZA AFYA-BARUA YA WAZI KWA WAZIRI AFYA NA ELIMU.pdf
    389.6 KB · Views: 43
Ukiona hivyo ujue kuna shida mahali kwani kusema uwepo wa centers za mitihani ndio itasababishw isivuje?

Yani sisi bado sana nasikia kwenye mitihani askari na mabunduki wanajazana kweli bado tuko nyuma.

Kwa wenzetu huku mitihani hufanyika online na marking ni instantly bila bias.

Hapo kupitia ile mitihani kuvuja watengeneza fursa watajazana kufanya ujanja ujanja .
 
Ukiona hivyo ujue kuna shida mahali kwani kusema uwepo wa centers za mitihani ndio itasababishw isivuje?

Yani sisi bado sana nasikia kwenye mitihani askari na mabunduki wanajazana kweli bado tuko nyuma.

Kwa wenzetu huku mitihani hufanyika online na marking ni instantly bila bias.

Hapo kupitia ile mitihani kuvuja watengeneza fursa watajazana kufanya ujanja ujanja .
Inasikitisha vijana wanalalamika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom