Wanaosali Jumuiya vs wacheza pool table, kuna tofauti?

Wanaosali Jumuiya vs wacheza pool table, kuna tofauti?

Ngoja nikupe taratibu ya ibada mbali mbali.

Wakristu,
Kundi hili tuna RC, wasabato, anglican, waluteli na waprotestant. Wasabato wao hufanya ibada zao jumamosi, hii siku dunia nzima inajulikana kama ni siku ya MAPUMZIKO!
Kundi la Rc, waprotestant, waluteli na anglican hawa hufanya ibada zao jpili, hii nayo inajulikana kama ni sikj ya MAPUMZIKO!

Waisilamu wao hufanya ibada yao kuu ijumaa, hii si siku ya mapumziko ILA, INAHESHIMIKA na KUTAMBULIKA dunia nzima kama siku ya ibada. Na waajiri wakristu mpaka wahindu wanaitambua.

Hizi ni taratibu zipo na zinatambulika na zimeleta balance duniani ever since.

Kuhusu swala la jumuiya! Ni kukosa weredi na heshima kuingilia mipaka ya mtu kuabudu especially katika siku ya mapumziko! Argument yako ni kuwa wakafanye kazi waache kusali, siku ya jmosi ambayo ni siku ya mapumziko ni watu wangapi huwa wamelala (wamepumzika) katika muda huo.ambao wengine wanasali?! Jiulize ni wangapi wenye MAENDELEO kuliko wewe huwa wamepumzika katika siku hiyo ya jumamosi, maendeleo yako wewe ni yapi mpaka uwabeze wenzako?!

Mfano ndugu zangu waislamu, wao hutakiwa na kitabu chao kitukufu kusali swala tano kila siku (si ujumaa tu), je nao wauvunje amri hiyo kisa tu kufanya kazi?! Nchi ngapi za kiarabu wanasali hadi katikati ya muda wa kazi na wana maendeleo kutuzidi sisi ambao tunasali katika siku maarumu (jmosi, jpili na ijumaa).

Kuhusu eti huko jumuiya watu wanaenda kuchukua namba na kwenda kuvunja amri ya sita, hii ni argument ya kitoto sana!! Hayo mambo ni hulka ya mtu tu, kwani makazini watu hawachukui namba na kwenda kuivunja hiyo amri😱

Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, jifunze kuheshimu mambo ya watu wengine, si busara kupayuka katika kila jambo hata lile ambalo hauna maarifa nalo.
 
Hata Trump anapingwa na kukejeliwa kwa kusema ukweli kuhusu Waafrika lakini baadae sisi wenyewe hukaa na kutafakari maneno yake na kujikosoa kimyakimya pengine tukimshukuru kimoyomoyo.
Sioni tofauti ya kuleta mada kama hii na kucheza pool
 
Tofauti yao ni kwamba wasali jumuiya hukutana mara moja kwa wiki tena sehemu moja mtaa mzima kwa muda maalum, wakati wacheza pooltable hukutana kila siku,muda wowote,sehemu mbalimbali mtaani! Hivyo wasali jumuiya wakomaliza kusali wanamuda wa kitosha kufanya kazi zao wakati wacheza pooltable wanaweza kushinda wanacheza kutwa nzima
 
Niambienii kuna nini cha maana tunacho-achieve kama jamiii ambacho bila kukaa katija hizo Jumuiya kingeshindikana?

Nijibuni sio kutoka povu.
Wasabato ndo kawaida yenu. Hivi mlifanikiwaga kwenda kuhubiri ulaya?
 
Bange haipatikani kirahisi siku hizi. Jamaa ana arosto. Pum**v zako
 
Umeshasema wanakutana sa12. Unatambua mwisho wa kazi hasa za kiserekali ni sangapi?

Huo ni muda wao wa ziada na wapo huru kuutumia wapendavyo.

Jiwekee hazina yako mbinguni ambapo haitaharibika.
 
Nijuavyo mimi kila jumuia inautaratibu wa kukutana mara moja kwa wiki. Na ni juu yao kupanga wakutane juma ngapi na sangapi.

Mwishowe mtawasema hata wale wa swala 5.

Fanya yote ila muhimu zaidi ni kumwabudu Allah.
 
----> Huu ujinga upo sana huku Kilimanjaro..... Wanakutana Ijumaa na Jumamosi....
Kama kumwabudu Mungu ni ujinga. Tupe Weledi wako wewe tuuone.

Ulitaka wikend wasisali waende beach?
 
Huo muda wa kila-week end kukutana nyumbani kwa mtu ni bora tungetenga na muda wa aina hiyo tukutane katika mitaa yetu kwa shughuli za kiuchumi au kupanga mipango ya kimaendeleo katika mitaa yetu.
Hivi makambi yanaanza lini?
 
Kilichobaki ni ushoga tu kukubalika katika dini zetu.
Ahaaa nimekuelewa. Kumbe wewe ni SHOGA mtoto wa watuu...Mungu wetu anakataza ushoga ndo mana unamchukia yeye na wanaomwamini...basi hujachelewa ndugu usikate tamaa SAA YA UKOMBOZI NI SASA.
 
Salary Slip!! Ndugu yangu umejiacha uchi sana. Nilidhani umekaa vizuri upstairs lakini kumbe si hasa. Pole sana . Njia rahisi wewe kama ni mkristu/mkatoliki na hupendezwi na huo utaratibu unaweza tu kutafuta dhehebu jingine ambalo hutapata shida hiyo ya kijumiya. OK?
Huyu jamaa na Babu yake Slaa walihamia kwa Gwajima, mzee wa malimao. Naona Gwajima naye kawapotezea ndio unamuona anatapatapa na Imani za watu wengine
 
Kusali kwenyewe mnasali kama fashion tu na mazoe ila matendo yenu ni bora hata wapagani!

Tumejijengea imani ya kipuuzi sana eti kuwa kusali swala tano na kwenda Kanisani ndio tumemaliza kila kitu wakati kitakachotuhukumu ni matendo yetu.

Unatoka Kanisani au Msikitini na gari lako una mkutana kilema njiani huku mvua ikimnyeshea unampita kama humuomi?

Unatoka kwenye sala yako dakika mbili baadae unaenda kuzini!

Sisi binadamu ni wanafiki wakubwa bora hata wanyama wasiomjua mungu kuliko sisi tuliopewa akili na mungu.

Watu ni mabingwa wa kutetea imani zao lakini ni mabingwa wakubwa wa kutenda dhambi kila kikicha tena pasipo hata kujutia dhambi zao!
Sasa umeanza kueleweka japo bado unachanganya mambo. Ukumbuke tu kuwa njia kati ya azimio na kitendo ni ndefu na hakuna binadamu aliye mkamilifu. Hata tujitahidi vipi, matendo yetu kamwe hayatafikia ukamilifu ndo maana tukaambiwa kuwa neema pekee ndiyo itatuokoa!
 
Copenhagen DN vipi huu utaratibu upo huko kusali jumuiya!? sverige SE haupo huu.. why only Africa
Marekani niliuona kwenye evangelical churches. Kuna jumuia za wanandoa, vijana, wanaume, wanawake etc na unaweza kuunda jumuia yo yote ali mradi upate ruhusa ya viongozi wa kanisa. Sisi tulikuwa na jumuia ya wanafunzi na tulikuwa tunakutana kila Jumamosi jioni. Kuna kipindi nilipata matatizo ya ini na wanajumuia wenzangu walinisaidia sana kwa maombi, kunipeleka hospitali mpaka kunipikia. Jumuia zinaleta umoja wa kiimani na kama mkitaka mnaweza kuchangishana na kutoa msaada kwa watu wenye matatizo. Mpaka leo nikienda Marekani sina haja ya kulala hotelini kama mji ninaoenda kuna ex mwanajumuia na wao wakija Bongo nawa-host...
 
Mikutano ya mitaa/vijiji hamshiriki ila Jumuiya ndio muhimu zaidi huku kila siku tukilia umasikini.Tutafika?Kwanini hizi Jumuiya zisifanywe kimtaa wala mara moja kwa wiki kuliko kuzunguka nyumba hadi nyumba kila week-end?Tujali muda.
Hicho kitakuwa Ni kijiti cha arusha au tarime ulichopuliza leo
 
Hivi hatuwezi kuishi pasipo kuwa na huu utaratibu wa kusali kwa jumuiya huku mitaani.Kusali makanisani hakutoshi mpaka tukutane kwenye majumba yetu siku za week-end na hata kila siku kwa baadhi ya maeneo kwa lengo tu la kusali kwa utaratibu huu wa Jumuiya?

Wanaocheza pool table wanatakiwa kukamatwa kwani wanapoteza muda wa kufanya kazi,je hawa wanaokutana saa 12 kila Jumamosi na kwa baadhi ya maeneo nasikia ni kila siku,huku si kupoteza muda wa kufanya kazi?

Hivi lengo la kusali Jumuiya si kukusanya sadaka tu?Nini kipya kinachofanyika katika hizi Jumuiya tofauti na makanisani kwetu?

Alafu hivi mtu unawezaje kushiriki kwenye Jumuiya hizi lakini ukashindwa kushiriki mikutano ya kijiji/mtaa kwa maendeleo ya kijiji/mtaa wako?

Kama hizi Jumuiya ni muhimu sana,kwanini adhabu hizi za kijamii tunazozitoa kwa watu wasioshiriki Jumuiya hizi pia tusizitoe kwa wale wasioshiriki mikutano ya maendeleo ya mitaa au vijiji vyetu kwani hata hii mikutano nayo ni muhimu pia?

Nyinyi mnaotetea Jumuiya hizi niambieni ni lini mlikutana katika Jumuiya zenu hizi na kisha mkaongozana huku mkiwa mbeba sadaka zenu na kwenda kuwahudumia wagonjwa au makelekezo sadaka zenu hizo kuhudumia yatima?

Utaratibu huu nimeuona hapa Dar leo hii nikakumbuka na huko mikoani hali ni hiyo hiyo hivyo nikajikuta najiuliza haya maswali.Alafu katika nchi za wenzetu mambo haya yanafanyika?Nina hakika miaka ijayo haya mambo yatakuja tu kutoweka maana sioni ulazima wake.
Ulishawi kusali? Au shetan anakutumia!
 
Huo muda wa kila-week end kukutana nyumbani kwa mtu ni bora tungetenga na muda wa aina hiyo tukutane katika mitaa yetu kwa shughuli za kiuchumi au kupanga mipango ya kimaendeleo katika mitaa yetu.
Huna shughuli yoyote ile ni ulevi wako tu.bangi na viroba mbaya sana
 
Back
Top Bottom