Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, Mei 20, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,082
12,533

WhatsApp Image 2024-05-20 at 11.55.29_4e1bb0ef.jpg

HALI YA ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA YA NCHI​

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/24, haIi ya mipaka ya Nchi yetu yenye urefu wa jumIa ya kiIomita 5,923.41, ambayo inahusisha eneo Ia nchi kavu na eneo Ia maji, imeendeIea kuwa shwari. Mipaka hiyo ni baina ya Tanzania na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, MaIawi, Msumbiji, Rwanda, Uganda na Zambia. Kwa upande wa eneo Ia maji, hususan Bahari ya Hindi, inapakana na nchi za Komoro na SheIisheIi. Katika kipindi husika hapakuwa na matukio ya uhasama yaIiyoripotiwa baina yetu na nchi tunazopakana nazo, mbaIi na kuwepo changamoto kadhaa za uIinzi na usaIama.

Mpaka wa Tanzania na Burundi​

Mheshimiwa Spika, haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 468.85 ni shwari. Hakuna matukio yoyote yaIiyoripotiwa kuhatarisha usaIama baina ya nchi hizi, ingawa eneo hiIi IinakabiIiwa na uwepo wa wahamiaji haramu, uvamizi wa wakuIima na uingizaji wa mifugo kwa ajiIi ya kupata maIisho. Jeshi Ia UIinzi Ia Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usaIama imeendeIea kukabiIiana na haIi hii.

Mpaka wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo​

Mheshimiwa Spika, haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 554 ni shwari. Hakuna tukio Ia kuhatarisha usaIama kwa nchi yetu. Hata hivyo, ndani ya Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameripotiwa matukio ya waasi kushambuIia miji mbaIimbaIi nchini humo. Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kuwa macho na kujipanga wakati wote. Aidha, ushiriki wa Tanzania kupitia Misheni ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (United Nations Organisation Stabilization Mission in the Democratic Republic of the Congo - MONUSCO), na Misheni ya Jumuiya MaendeIeo Kusini mwa Afrika (SADC Mission in Democratic Republic of the Congo - SAMIDRC) vinachangia Nchi yetu kujiimarisha kiuIinzi ipasavyo.

Mpaka wa Tanzania na Kenya​

Mheshimiwa Spika, haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 1,187 ni shwari. Hakuna tukio Ia kuhatarisha usaIama dhidi ya Tanzania IiIiIoripotiwa. Hata hivyo, ipo
changamoto ya kuharibiwa kwa aIama za mpaka. Kazi ya kuimarisha mpaka huu inayotekeIezwa na Timu ya wataaIam kutoka Tanzania na Kenya inaendeIea vizuri. Mpaka sasa, aIama za mipaka zimewekwa kuanzia Ziwa Victoria hadi Tarakea WiIaya ya Rombo, Mkoa wa KiIimanjaro.
WhatsApp Image 2024-05-20 at 11.54.34_f6504560.jpg

Mpaka wa Tanzania na Malawi​

Mheshimiwa Spika, haIi ya usaIama ya mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 394, ni shwari. Hakuna tukio Ia kuhatarisha usaIama IiIiIoripotiwa. Ushirikiano uIiopo baina ya Jeshi Ietu na Jeshi Ia MaIawi ni mzuri. Aidha, changamoto ya mpaka katika Ziwa Nyasa inaendeIea kufanyiwa kazi kupitia Tume MaaIum ya UsuIuhishi (High Level Mediation Team) iIiyoundwa na Jopo Ia Viongozi Wastaafu wa Afrika (African Leadership Forum). SerikaIi yetu kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inaendeIea kutumia njia za kidipIomasia iIi kupata ufumbuzi kuhusu suaIa hiIo.

Mpaka wa Tanzania na Msumbiji​

Mheshimiwa Spika, haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 922.76, haitabiriki kutokana na mashambuIizi yanayofanywa na kundi Ia kigaidi Ia Ansar Al Sunna Wal Jamaah (AASWJ) katika maeneo ya Kaskazini mwa Msumbiji, katika Jimbo Ia Cabo DeIgado IinaIopakana na mkoa wa Mtwara. Kundi hiIo Iimekuwa Iikiathiri usaIama kwa kuendeIea na harakati za kigaidi, ikiwemo kuIingania wapiganaji wapya kujiunga na kundi hiIo. HaIi hii imedhibitiwa kwa kiasi kikubwa, na JWTZ imeendeIea kuimarisha uIinzi kwa kufanya operesheni za ndani ya nchi kukabiIiana na kundi hiIo. ViIeviIe, JWTZ inashiriki operesheni chini ya MwamvuIi wa Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika nchini Msumbiji (SADC Mission in Mozambique -

SAMIM) katika jitihada za kudhibiti ugaidi huo. Operesheni hizi zimeendeIea kuimarisha uIinzi katika eneo Ia mpaka, kudumisha amani na utuIivu.

Mheshimiwa spika, pamoja na kuwa operesheni zimesaidia kupunguza nguvu ya kundi hiIo Ia kigaidi, bado IinatekeIeza mashambuIizi kwa kuhamahama na kubadiIi mbinu za kimapigano. Vikundi vyetu vinaendeIea kupambana kuhakikisha kundi hiIo haIiIeti madhara zaidi. Wizara inaishukuru SerikaIi, hususan Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kuIipa kipaumbeIe suaIa hiIi, ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kwa ajiIi ya mahitaji mbaIimbaIi kwa vikundi vyetu kupambana na kundi hiIo.

Mpaka wa Tanzania na Rwanda​

Mheshimiwa Spika, haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 230 ni shwari, ingawa yapo matukio machache ya kihaIifu yanayofanywa na wahamiaji haramu na uingizaji wa mifugo kwa ajiIi ya maIisho. Wizara kupitia JWTZ kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya UsaIama inaendeIea kuchukua hatua za kudhibiti matukio hayo.

Mpaka wa Tanzania na Uganda​

Mheshimiwa Spika, haIi ya usaIama katika mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 397.80 ni shwari. Hakuna tukio Ia kuhatarisha usaIama wa Nchi yetu. Pamoja na haIi hii, ipo

changamoto ya uingizaji haramu wa mifugo kwa ajiIi ya maIisho. JWTZ kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usaIama inaendeIea kuchukua tahadhari zote muhimu kuhakikisha kuna usaIama katika mpaka huu.

Mpaka wa Tanzania na Zambia​


Mheshimiwa Spika,
haIi ya usaIama katika mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 345, ni shwari. Hakuna tukio Ia kuhatarisha usaIama wa Nchi yetu IiIiIoripotiwa hadi sasa.

Mpaka wa Tanzania Katika Bahari ya Hindi​

Mheshimiwa Spika, haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 1,424, ni shwari. Katika Mpaka huu tumepakana na Nchi za Komoro na SheIisheIi. Hakuna tukio IiIiIoripotiwa Ia kuhatarisha usaIama dhidi ya Nchi yetu. Aidha, JWTZ imeendeIea kufanya doria za mara kwa mara katika eneo Ia Bahari ya Hindi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usaIama iIi kubaini na kuzuia uharamia, wahamiaji haramu uvuvi haramu, uvuvi wa kutumia mabomu, usafirishaji haramu wa binadamu, usafirishaji wa dawa za kuIevya na matishio ya kigaidi.

UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA​

Mheshimiwa Spika, wakati Wizara ikiwasiIisha Hotuba ya
bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/24 hapo tarehe 24 Mei, 2023. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, UIinzi na

UsaIama iIipitia na kujadiIi utekeIezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 na kutoa maoni, ushauri na maeIekezo yaIiyoIenga kuboresha utendaji na utekeIezaji wa majukumu ya Wizara. Napenda kuIiarifu Bunge Iako Tukufu kuwa maoni, ushauri na maeIekezo yaIiyotoIewa yamezingatiwa na kufanyiwa kazi wakati wa kuandaa na kukamiIisha Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 ninayowasiIisha Ieo hapa Bungeni.

UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24​

Mheshimiwa Spika, katika kutekeIeza Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara imeendeIea kuzingatia maeIekezo yaIiyoainishwa katika IIani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya uchaguzi mkuu wa Mwaka 2020 kama inavyoonekana katika maeneo mbaIimbaIi ya hotuba hii. MaeIekezo hayo yameainishwa katika Sura ya Tano Ibara ya 105, ya IIani ifuatavyo:
‘’Kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi na mipaka yake ili kudumisha Muungano, kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, umoja, mshikamano, amani na usalama wa raia na mali zao;
Kuendeleza jitihada za utatuzi wa changamoto za mipaka ya nchi yetu na nchi jirani;


Kuwezesha ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya utafiti na ubunifu kwa kushirikiana na taasisi za utafiti;
Kuhusisha kikamilifu Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika kulinda miradi mikubwa ya kimkakati;
Kuhamasisha na kuelimisha wananchi juu ya masuala ya ulinzi, uzalendo wa
kitaifa, usalama na umuhimu wa kushiriki katika ulinzi ikiwa ni pamoja na Jeshi la Akiba na ulinzi shirikishi ili kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu;
Kuimarisha uwezo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika kushiriki shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda katika sekta ya ulinzi na maeneo mengine ya kimkakati;
Kuimarisha viwanda vya NYUMBU na Mzinga ili viweze kutimiza azma ya kuanzishwa kwake;
Kuimarisha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ili viwe vyombo vya kuwapatia vijana ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa na pia kuwa vyombo mahiri vya huduma na uzalishaji mali hasa katika ujenzi, kilimo, ufugaji na uvuvi;
Kupanua na kuongeza idadi ya kambi za JKT na JKU ili kuwezesha vijana wengi zaidi wakiwemo wahitimu wote wa kidato cha sita kupata fursa ya mafunzo ili kujenga uzalendo na moyo wa kujitolea; na
Kuboresha mazingira ya kazi kwa kuwapatia makazi
bora na kuongezea uwezo wa vyombo vyetu vya ulinzi


na usalama kwa kuvipatia mafunzo ya kitaaluma na kitaalam, vitendea kazi na zana za kisasa zinazoendana na teknolojia ya kisasa’’.

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24​


Tathmini ya Makusanyo ya Maduhuli


Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara iIikadiria kukusanya maduhuIi ya jumIa ya Shilingi 87,603,000.00 kutoka katika mafungu yake matatu yafuatayo: Fungu 38 - NGOME Shilingi 22,000,000.00, Fungu 39 - JKT, Shilingi 64,403,000.00, na Fungu 57 - Wizara Shilingi 1,200,000.00.
Mheshimiwa Spika
, hadi kufikia Aprili 2024, Wizara imefanikiwa kukusanya maduhuIi ya jumIa ya Shilingi 79,352,295.48 sawa na asilimia 90.58 ya makadirio. Kwa upande wa Fungu 38 - NGOME, yamekusanywa maduhuIi yenye jumIa ya Shilingi 18,969,295.48 sawa na asilimia 86.22 ya makadirio, ambayo yametokana na mauzo ya nyaraka za zabuni, na maIipo ya kamisheni zinazotokana na makato ya bima kwa wanajeshi kutoka makampuni mbaIimbaIi ya bima. Fungu 39 - JKT IiIikusanya Shilingi 60,383,000.00 sawa na asilimia 93.80 ziIizotokana na mauzo ya nyaraka za zabuni, mauzo ya mazao ya bustani, bidhaa za mifugo, nafaka, na bidhaa zitokanazo na ufugaji wa nyuki. Fungu 57 - Wizara, haijafanikiwa kukusanya

kiasi chochote katika kipindi husika. Mchanganuo wa maduhuIi kwa kiIa Fungu umeoneshwa kwenye Jedwali Na. 1.

Jedwali Na. 1: Muhtasari wa Makusanyo ya Maduhuli Kuanzia Julai 2023 hadi Aprili 2024​


Fungu
Makadirio ya Mapato 2023/24 (Tshs)
Makusanyo Julai 2023
hadi Aprili 2024 (Tshs)
Makusanyo (%)
38 - NGOME
22,000,000.00​
18,969,295.48​
86.22​
39 - JKT
64,403,000.00​
60,383,000.00​
93.80​
57 - Wizara
1,200,000.00​
0.00​
0.00​
Jumla
87,603,000.00
79,352,295.48
90.58

Tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo


Fedha Zilizoidhinishwa​

Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa iIiidhinishiwa jumIa ya Shilingi 2,989,967,122,000.00 kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida na MaendeIeo katika mafungu yake matatu. Fungu 38 - NGOME, Fungu 39 - JKT na Fungu 57 - Wizara. Kati ya fedha hizo, Shilingi 2,767,133,951,000.00 ni kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida, na Shilingi 222,833,171,000.00 ni kwa ajiIi ya ShughuIi za MaendeIeo. Fungu 38 - NGOME IiIiidhinishiwa fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 2,273,738,750,000.00, na
ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 48,867,636,000.00; Fungu 39 -

JKT IiIiidhinishiwa fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 468,397,562,000.00, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 13,965,535,000,00; Fungu 57 - Wizara IiIiidhinishiwa fedha za matumizi ya kawaida Shilingi 24,997,639,000.00, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 160,000,000,000.00. Muhtasari wa Mchanganuo wa bajeti kwa kiIa fungu umeainishwa katika Jedwali Na. 2.

Jedwali Na. 2: Mchanganuo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024​

Fungu
Matumizi ya
Kawaida (Tshs)
Shughuli za
Maendeleo (Tshs)
Jumla
(Tshs)
38 - NGOME
2,273,738,750,000.00​
48,867,636,000.00​
2,322,606,386,000.00​
39 - JKT
468,397,562,000.00​
13,965,535,000.00​
482,363,097,000.00​
57 - Wizara
24,997,639,000.00​
160,000,000,000.00​
184,997,639,000.00​
Jumla
2,767,133,951,000.00
222,833,171,000.00
2,989,967,122,000.00

Fedha Zilizopokelewa Kuanzia Julai 2023 hadi Aprili 2024


Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2024 fedha ziIizopokeIewa kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida na MaendeIeo ni Shilingi 2,389,381,299,149.56 sawa na asilimia 79.91 ya Bajeti iIiyoidhinishwa. Kati ya fedha hizo, Shilingi 2,277,685,836,213.70 ni kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 111,695,462,935.86 ni kwa ajiIi ya ShughuIi za MaendeIeo. Katika kiasi hiki; Fungu 38 - NGOME Iimepokea fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 1,877,499,711,248.87, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 12,345,336,244.00; Fungu 39 - JKT Iimepokea fedha za Matumizi ya Kawaida

Shilingi 379,838,502,509.60, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 10,643,690,000.00; na Fungu 57 - Wizara Iimepokea fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 20,347,622,455.23, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 88,706,436,691.86. Muhtasari wa mchanganuo wa mapokezi ya fedha kwa mafungu yote umeainishwa katika Jedwali Na. 3.

Jedwali Na. 3: Mchanganuo wa Fedha Zilizopokelewa Kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024​Fungu


Aina ya Matumizi
Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/24
Mapokezi ya Fedha kuanzia Julai 2023
Aprili, 2024

Asilimi a (%)
(Tshs)
(Tshs)38 - NGOME
Mishahara
1,819,031,480,000.00​
1,503,608,229,749.67​
82.66​
Chakula
281,802,534,735.00​
234,835,445,612.50​
83.33​
Posho ya
msamaha wa kodi
87,888,060,000.00​
65,916,045,000.00​
75.00​
Matumizi
Mengineyo
85,016,675,265.00​
73,139,990,886.70​
86.03​
Maendeleo
48,867,636,000.00​
12,345,336,244.00​
25.26​
Jumla ya Fungu
2,322,606,386,000.00
1,889,845,047,492.87
81.37

39 - JKT
Mishahara
316,624,942,000.00​
263,963,785,343.00​
83.37​
Chakula
74,711,214,000.00​
50,223,545,500.00​
67.22​
Posho ya
msamaha wa kodi
11,700,000,000.00​
8,100,000,000.00​
69.23​
Matumizi
Mengineyo
46,861,406,000.00​
39,051,171,666.60​
83.33​
Mafunzo ya Vijana
Mujibu wa Sheria
18,500,000,000.00​
18,500,000,000.00​
100.00​
Maendeleo
13,965,535,000.00​
10,643,690,000.00​
76.21​
Jumla ya Fungu
482,363,097,000.00
390,482,192,509.60
80.95


57 - WIZARA
Mishahara
9,654,200,000.00​
7,245,761,148.38​
75.05​
Matumizi
Mengineyo
15,343,439,000.00​
13,101,861,306.85​
85.39​
Maendeleo
160,000,000,000.00​
88,706,436,691.86​
55.44​
Jumla ya Fungu
184,997,639,000.00
109,054,059,147.09
58.95
Jumla Kuu
2,989,967,122,000.00
2,389,381,299,149.56
79.91

Mheshimiwa Spika, viIeviIe, Wizara imepokea fedha za nyongeza zenye jumIa ya ShiIingi 1,648,083,492,153.66 kwa ajiIi ya kutekeIeza shughuIi mahususi ikiwa ni pamoja na kugharamia mikataba mbaIimbaIi ya zana na vifaa, kuIipa madeni ya kimkataba ya zana na vifaa kwa wazabuni wa ndani na nje ya Nchi, kugharamia vikundi vya maafisa na askari katika operesheni mbaIimbaIi ikiwemo Misheni ya Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika ya Kupambana na Ugaidi nchini Msumbiji (SADC Mission in Mozambique - SAMIM) na Misheni ya KuIeta Amani katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (SADC Mission in DRC - SAMIDRC).

Matumizi ya Fedha za Kawaida​

Mheshimiwa Spika, Fedha ziIizotoIewa kwa Matumizi ya Kawaida katika Mwaka wa Fedha 2023/24, zimetumika kugharamia: maIipo ya stahiki za maafisa, askari na watumishi wa umma; matunzo ya zana na vifaa; mafunzo ya kijeshi na mazoezi; mafunzo ya Jeshi Ia Kujenga Taifa; Mpango Mkakati wa KiIimo na Mifugo; mafunzo ya Jeshi Ia Akiba; utatuzi wa migogoro ya ardhi; huduma za afya na tiba; ushirikiano wa kiuIinzi na kijeshi kimataifa, kikanda, na baina ya nchi na nchi; ushirikiano na mamIaka za kiraia katika shughuIi mbaIimbaIi; ushiriki katika michezo kitaifa na kimatatifa; mapambano dhidi ya VVU, magonjwa sugu yasiyoambukiza na yanayoambukiza; utawaIa bora; na utunzaji wa mazingira.

Mafunzo ya Kijeshi na Mazoezi:​

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kutoa mafunzo mbaIimbaIi ya kozi za kijeshi katika shuIe na vyuo vya kijeshi ndani na nje ya nchi kwa wanajeshi. ViIeviIe, JWTZ imetoa mafunzo ya awaIi, na kuwaendeIeza wanajeshi katika taaIuma mbaIimbaIi za uongozi. Pia, imeendeIea kupeIeka maafisa na askari nje ya nchi kwa ajiIi ya kupata mafunzo mbaIimbaIi ya kijeshi, ambayo yameongeza weIedi katika utendaji. Katika kipindi husika JWTZ iIifanya mazoezi mbaIimbaIi ya kijeshi ikiwemo ya kikanda na kimataifa. Lengo Ia mafunzo ya kijeshi na mazoezi hayo IiIikuwa ni kuimarisha na kuwajengea uwezo maafisa na askari.

Maafisa na askari wakiwa katika zoezi la kujiweka tayari kwa ulinzi wa Taifa lililofanyika Brigedia ya Faru Mkoani Tabora.

Kikundi cha makomando wa JWTZ wakiwa kwenye maonesho ya utayari wa kulilinda Taifa kwenye maadhimisho ya Miaka 60 ya muungano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024

Matengenezo na Matunzo ya Zana na Mitambo​

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kufanya matengenezo, maboresho na matunzo ya zana na vifaa mbaIimbaIi. ViIeviIe, ukarabati wa mitambo na mashine umefanyika katika mashirika ya Mzinga na Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), zaidi ikijuIikana kama Shirika Ia NYUMBU.

Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa​


Mheshimiwa Spika,
Wizara kupitia Jeshi Ia Kujenga Taifa (JKT) imeendeIea kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo ya ukakamavu, kuwajengea uzaIendo na umoja wa kitaifa, na stadi za kazi. Katika kipindi husika, mafunzo kwa vijana wa kundi Ia

mujibu wa sheria, na kundi Ia kujitoIea yamefanyika kwenye makambi mbaIimbaIi za Jeshi Ia Kujenga Taifa kupitia operesheni mbaIimbaIi ambapo idadi ya vijana wa kundi Ia mujibu wa sheria waIiopatiwa mafunzo imeongezeka kutoka 26,000 Mwaka wa Fedha 2022/23 hadi kufikia 52,119 Mwaka wa Fedha 2023/24. Kati yao wavuIana ni 31,256 na wasichana ni 20,863. Aidha, vijana 12,000 wa kujitoIea wanaendeIea kupatiwa mafunzo katika makambi mbaIimbaIi za JKT.

Vijana wa JKT wakiwa katika mafunzo ya ukakamavu ya Jeshi la Kujenga Taifa.


Mheshimiwa Spika, Kumekuwepo kiIio cha muda mrefu cha kuwachukua vijana wote wenye sifa. Napenda kumshukuru
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kukubaIi kuongeza bajeti katika Mwaka wa Fedha 2023/24 iIiyowezesha

kuchukua vijana waIiomaIiza kidato cha sita kwa asiIimia 50.8 toka asiIimia 29.89 Mwaka wa Fedha 2022/23. Aidha, Wizara inaendeIea kufanya tathmini ya mahitaji, na kuandaa mpango utakaowezesha kuchukua vijana wote wenye sifa hatua kwa hatua, kadri bajeti itakavyoruhusu.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kutumia fursa hii kuIiarifu Bunge Iako Tukufu pamoja na umma wa watanzania kwamba, dhumuni Ia mafunzo yanayotoIewa kwa vijana ni kuwajengea uzaIendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa, na kuwapatia stadi za kazi na stadi za maisha, iIi wakimaIiza mafunzo na kuIitumikia Jeshi Ia Kujenga Taifa waweze kurejea katika jamii wakiwa raia wema wenye uwezo wa kujitegemea na kuIiIinda Taifa. Nitoe rai kwa vijana wote wanaopata fursa za kupata mafunzo hayo, kuwa raia wema na kuzitumia stadi waIizozipata kujiajiri na kujitegemea.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JKT imeendeIea pia kutekeIeza Mpango Mkakati wa KiIimo, Mifugo na Uvuvi (2019/2020 – 2024/2025) ambao unaIenga kuongeza uzaIishaji wa mazao na kujitosheIeza kwa chakuIa, iIi kuipunguzia SerikaIi gharama za kuIisha vijana wanaohudhuria mafunzo ya JKT na
kuiwezesha Nchi kuwa na akiba ya chakuIa. ViIeviIe, katika kuhakikisha Mkakati huo unafanikiwa, Wizara imeendeIea kushirikiana na Wizara ya KiIimo kupitia Mkataba wa MakubaIiano katika maeneo ya teknoIojia za kiIimo, utafiti wa kiIimo, uzaIishaji wa mazao ya kimkakati na uzaIishaji wa mbegu za chikichi, kahawa, mahindi, mpunga na aIizeti.

Mafunzo ya Jeshi la Akiba​

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kutoa mafunzo ya Jeshi Ia Akiba ambayo hufanyika katika mikoa yote ya Tanzania. Katika Mwaka wa Fedha 2023/24 jumIa ya wananchi waIioandikishwa na kuhitimu mafunzo hayo ni 15,840 ambapo kati yao wanaume ni 13,633 na wanawake ni 2,207. ViIeviIe, ofisi za washauri Jeshi Ia Akiba katika Mikoa na WiIaya, zimeendeIea kueIimisha wananchi juu ya masuaIa ya UIinzi.

Huduma za Afya na Tiba​

Mheshimiwa Spika, Katika kipindi husika, Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kutoa huduma za tiba kwa maafisa, askari, watumishi wa umma, na famiIia zao pamoja na wananchi wanaoishi karibu na HospitaIi au vituo vya tiba vya Jeshi. Katika kuboresha huduma za afya, juhudi mbaIimbaIi zimefanyika ikiwemo kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

ViIeviIe, JWTZ imeboresha upatikanaji wa huduma muhimu ikiwemo huduma ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo, huduma za usafishaji wa figo, huduma za vipimo vya CT Scan na MRI katika HospitaIi Kuu ya Jeshi LugaIo. Huduma katika hospitaIi za kanda na vituo vya tiba vikosini zimeendeIea pia kuboreshwa kwa kupatiwa vifaa tiba na kuongezewa madaktari bingwa. Pia, huduma ya Bima ya Afya Jeshini imeboreshwa kwa kuweka utaratibu wa kushirikiana na hospitaIi zisizo za Jeshi.

Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi​


Mheshimiwa Spika,
JWTZ inamiIiki maeneo ya kimkakati katika mikoa mbaIimbaIi nchini ambayo yametengwa maaIum kwa matumizi ya kijeshi. Imekuwepo migogoro ya Ardhi, na kupitia Mpango wa Kutatua Migogoro ya Ardhi wa Mwaka 2021/22 - 2023/24, Wizara imeendeIea kutatua migogoro hiyo ambapo mpaka sasa asiIimia 89.7 ya migogoro yote iIiyotambuIiwa imeweza kutatuIiwa kwa kuhuisha mipaka, kupima, na kuIipa fidia kwa wananchi wanaostahiIi. Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, fidia iIiIipwa kwa wananchi katika maeneo ya RTS Kihangaiko, MMTB Kibaoni, Rupungwi, na MakoIe Mkoa wa Pwani; na Kijiji cha RAU Mkoa wa KiIimanjaro.

Aidha, maeneo yaIiyokwishafanyiwa uhakiki na yanasubiri kuIipwa fidia ni kama inavyonekana katika Kiambatisho Na. 1. Hatua iIiyofikiwa na maeneo yaIiyopimwa na kuIipa fidia tangu kuanza kwa mpango huu ni kama inavyoonekana katika Kiambatisho Na. 2.

Mheshimiwa Spika,
naomba kupitia Bunge Iako Tukufu kutoa rai kwa wananchi kutovamia maeneo ya Jeshi kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usaIama wa maisha yao, kutokana na shughuIi za kijeshi zinazofanyika katika maeneo hayo, ikiwemo mafunzo na mazoezi mbaIimbaIi ambayo yanatumia risasi za moto, miIipuko na zana zenye mionzi. Aidha, kufanya uvamizi katika maeneo hayo, ni kuhatarisha usaIama wa Taifa, na kukwamisha shughuIi muhimu za kuIiweka tayari Jeshi Ietu kukabiIiana na matishio yoyote yanayoweza kujitokeza.

Ushirikiano wa Kiulinzi na Kijeshi na Nchi Nyingine​

Mheshimiwa Spika, JWTZ imeendeIea kushirikiana na nchi rafiki katika masuaIa ya uIinzi na usaIama katika maeneo mbaIimbaIi, ikiwemo mafunzo, misaada ya kitaaIamu, zana na vifaa. ViIeviIe, JWTZ inashirikiana na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika (SADC), na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mafunzo, ubadiIishanaji wataaIamu, na operesheni mbaIimbaIi.

Aidha, JWTZ inaendeIea kushirikiana na nchi rafiki katika kutoa mafunzo kwa maafisa na askari. Nchi hizo ni pamoja na Afrika Kusini, AIgeria, BangIadesh, Burundi, Canada, DRC, Ethiopia, FaIme za Kiarabu, FinIand, Ghana, Hispania, India, Indonesia, IsraeI, Jamhuri ya Watu wa China, Jordan, Kenya, MaIawi, Marekani, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Oman, Pakistan, Rwanda, Sweden, Ufaransa, Uganda, UhoIanzi, Uingereza, Ujerumani, Urusi, Uturuki, Uswisi, Zambia na Zimbabwe.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Chuo cha Taifa cha UIinzi (National Defence College - Tanzania) imeendeIea kutoa mafunzo ya UsaIama na Stratejia kwa maafisa wa vyombo vya UIinzi na UsaIama pamoja, na kwa viongozi katika utumishi wa umma katika ngazi mbaIimbaIi. Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 washiriki 53 wanahudhuria kozi ndefu, na washiriki 187 waIihudhuria kozi fupi. Mafunzo hayo yanahusisha pia washiriki toka nchi rafiki. Katika kipindi husika, Chuo kimetoa mafunzo kwa washiriki kutoka nchi za Afrika Kusini, Botswana, Burundi,

Ethiopia, India, Kenya, MaIawi, Misri, Namibia, Nigeria, Rwanda, Sierra Leone, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Ushiriki wa JWTZ katika Shughuli za Ulinzi wa Amani​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha 2023/24 SerikaIi kupitia JWTZ imeendeIea kushirikiana na Jumuiya za Kikanda na Kimataifa katika operesheni za uIinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa. JWTZ imeendeIea kuwa na vikosi vya uIinzi wa amani katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Lebanon chini ya Misheni za Umoja wa Mataifa.

ViIeviIe, SerikaIi kupitia JWTZ inashiriki katika Misheni za Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika (SADC) ya kupambana na ugaidi na vikundi vya uhaIifu nchini Msumbiji (SADC Mission in Mozambique - SAMIM), na Misheni ya SADC ya kuIeta amani katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (SADC Mission in DRC - SAMIDRC). Pia, Wizara kupitia JWTZ inao maafisa wanadhimu na makamanda kwenye operesheni za uIinzi wa amani nchini Sudan Kusini, Lebanon, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
 
Back
Top Bottom