Wanaosali Jumuiya vs wacheza pool table, kuna tofauti?

Kusali kwenyewe mnasali kama fashion tu na mazoe ila matendo yenu ni bora hata wapagani!

Tumejijengea imani ya kipuuzi sana eti kuwa kusali swala tano na kwenda Kanisani ndio tumemaliza kila kitu wakati kitakachotuhukumu ni matendo yetu.

Unatoka Kanisani au Msikitini na gari lako una mkutana kilema njiani huku mvua ikimnyeshea unampita kama humuomi?

Unatoka kwenye sala yako dakika mbili baadae unaenda kuzini!

Sisi binadamu ni wanafiki wakubwa bora hata wanyama wasiomjua mungu kuliko sisi tuliopewa akili na mungu.

Watu ni mabingwa wa kutetea imani zao lakini ni mabingwa wakubwa wa kutenda dhambi kila kikicha tena pasipo hata kujutia dhambi zao!
Mbona kama unamsema babu yako aka mzee wa harambee uliyemzungushia mikono ???

Kanisani deile halafu anatupiga marichmond ya kutosha halafu chenji inarudi kanisani na msikitini.

Kweli leo umefakamia kitu cha Arusha kwa style ya SHISHA
 
Mada mzuri mkuu ila tatizo wanaoenda jumuiya ni wavivu na wana IQ ndogo na ndio hawa wanaokushambulia hizo jumuiya zipigwe tu marufuku
ni mambo ya imani,japo naona kama hakuna logic na ni upotevu wa mda wa kiuzalisha ama kufanya mambo mengine,
maana Mungu hapatikani jumuiani,
unaweza kumwomba hata ukiwa upenuni mwa nyumba na akasikia,sio lazima kwenda jumuia,
 
Wewe kama jumuia haikuhusu ,shida yako nini? waache wanaoenda wapoteze muda, sio suala jema kumuingilia mtu imani yake. Acha ujuaji usiokuwa na maana . RESPECT.
 
Hivi hatuwezi kuishi pasipo kuwa na huu utaratibu wa kusali kwa jumuiya huku mitaani.Kusali makanisani hakutoshi mpaka tukutane kwenye majumba yetu siku za week-end na hata kila siku kwa baadhi ya maeneo kwa lengo tu la kusali kwa utaratibu huu wa Jumuiya?

Wanaocheza pool table wanatakiwa kukamatwa kwani wanapoteza muda wa kufanya kazi,je hawa wanaokutana saa 12 kila Jumamosi na kwa baadhi ya maeneo nasikia ni kila siku,huku si kupoteza muda wa kufanya kazi?

Hivi lengo la kusali Jumuiya si kukusanya sadaka tu?Nini kipya kinachofanyika katika hizi Jumuiya tofauti na makanisani kwetu?

Alafu hivi mtu unawezaje kushiriki kwenye Jumuiya hizi lakini ukashindwa kushiriki mikutano ya kijiji/mtaa kwa maendeleo ya kijiji/mtaa wako?

Kama hizi Jumuiya ni muhimu sana,kwanini adhabu hizi za kijamii tunazozitoa kwa watu wasioshiriki Jumuiya hizi pia tusizitoe kwa wale wasioshiriki mikutano ya maendeleo ya mitaa au vijiji vyetu kwani hata hii mikutano nayo ni muhimu pia?

Utaratibu huu nimeuona hapa Dar leo hii nikakumbuka na huko mikoani hali ni hiyo hiyo hivyo nikajikuta najiuliza haya maswali.Alafu katika nchi za wenzetu mambo haya yanafanyika?Nina hakika miaka ijayo haya mambo yatakuja tu kutoweka maana sioni ulazima wake.
Aaaah kiongozi nilikuwa nakuona bonge la mtu mwenye busara lakini leo umeniangusha sana! This is very, very low! Yaani jumuiya unailinganisha na wacheza pool? Very poor reasoning! Niambie ni jumuiya gani wanasali tangu saa 12 asubuhi mpaka SAA 12 jioni? Mara nyingi jumuiya zinakutana kwa SAA 1 tu! Huko shule ulienda kuondoa ujinga tu!
 
mkuu Nimekua out SMART sana.

Jumuia ni mara moja kwa juma, pia huwa ni saa kumi na mbili asubuhi mpakaa saa moja siku ya juma mosi, ni tofauti na wachaza pool!!

Pia jumuia ni swala la kiimani zaidi ni kama Waislam wanao swali kila siku asubuhi.

dah sikuwai kutegemea maneno kama haya kutoka kwa mtu kama wewe.
 
Wewe ndiyo hakuna kitu kabisa.

Kwanza kama hujui watu ambao huwa wanafanya ibada ndiyo pia wanaoongoza kwa kufanya kazi kwa kujituma, nidhamu na uaminifu, na wengi wao ukiwachunguza hawapo katika makindi ya wanaoshindwa kuendesha maisha yao. Anayeenda kusali saa 12 ndiye anayeamka kila siku saa 11 alfajiri. Wale waislam wanaofanya ibada saa 11 huamka saa 10 au saa 10.30 alfajiri. Muda huo watu wapuuzi kama wewe mnakuwa bado mmekumbatia shuka.

Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa watu wake kwenda kwenye ibada kabla ya kwenda kazini. Najua utashangaa kusikia hivyo lakini ndiyo ukweli.

Umeleta hoja ya kipuuzi kabisa.

Ingekuwa inawezekana ningependa watu wote kabla ya kazi wafanye ibada, na hiyo ingebadilisha sana ufanisi wa kazi.

Huo muda wa kila-week end kukutana nyumbani kwa mtu ni bora tungetenga na muda wa aina hiyo tukutane katika mitaa yetu kwa shughuli za kiuchumi au kupanga mipango ya kimaendeleo katika mitaa yetu.
 
Aaaah kiongozi nilikuwa nakuona bonge la mtu mwenye busara lakini leo umeniangusha sana! This is very, very low! Yaani jumuiya unailinganisha na wacheza pool? Very poor reasoning! Niambie ni jumuiya gani wanasali tangu saa 12 asubuhi mpaka SAA 12 jioni? Mara nyingi jumuiya zinakutana kwa SAA 1 tu! Huko shule ulienda kuondoa ujinga tu!
Kila week-end mnakutana saa 12 asubuhi lakini muda wa kulima hata bustani ya mboga za majani hapo nyumbani kwako utadai huna alafu kila siku tunalalamika maisha magumu!
 
Wewe ndiyo hakuna kitu kabisa.

Kwanza kama hujui watu ambao huwa wanafanya ibada ndiyo pia wanaoongoza kwa kufanya kazi kwa kujituma, nidhamu na uaminifu, na wengi wao ukiwachunguza hawapo katika makindi ya wanaoshindwa kuendesha maisha yao. Anayeenda kusali saa 12 ndiye anayeamka kila siku saa 11 alfajiri. Wale waislam wanaofanya ibada saa 11 huamka saa 10 au saa 10.30 alfajiri. Muda huo watu wapuuzi kama wewe mnakuwa bado mmekumbatia shuka.

Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa watu wake kwenda kwenye ibada kabla ya kwenda kazini. Najua utashangaa kusikia hivyo lakini ndiyo ukweli.

Umeleta hoja ya kipuuzi kabisa.

Ingekuwa inawezekana ningependa watu wote kabla ya kazi wafanye ibada, na hiyo ingebadilisha sana ufanisi wa kazi.
Wengi wenu mna akili za kipuuzi kuwa mtaenda mbinguni kwa kufanya ibada huku matendo yenu ya kila siku ni dhambi tupu.

Binadamu wengi wa leo tunasali kama fashion tu na ndio maana maovu yametamalaka dunia nzima licha ya nyumba za ibada kuongezeka kama uyoga.
 
Hivi hatuwezi kuishi pasipo kuwa na huu utaratibu wa kusali kwa jumuiya huku mitaani.Kusali makanisani hakutoshi mpaka tukutane kwenye majumba yetu siku za week-end na hata kila siku kwa baadhi ya maeneo kwa lengo tu la kusali kwa utaratibu huu wa Jumuiya?

Wanaocheza pool table wanatakiwa kukamatwa kwani wanapoteza muda wa kufanya kazi,je hawa wanaokutana saa 12 kila Jumamosi na kwa baadhi ya maeneo nasikia ni kila siku,huku si kupoteza muda wa kufanya kazi?

Hivi lengo la kusali Jumuiya si kukusanya sadaka tu?Nini kipya kinachofanyika katika hizi Jumuiya tofauti na makanisani kwetu?

Alafu hivi mtu unawezaje kushiriki kwenye Jumuiya hizi lakini ukashindwa kushiriki mikutano ya kijiji/mtaa kwa maendeleo ya kijiji/mtaa wako?

Kama hizi Jumuiya ni muhimu sana,kwanini adhabu hizi za kijamii tunazozitoa kwa watu wasioshiriki Jumuiya hizi pia tusizitoe kwa wale wasioshiriki mikutano ya maendeleo ya mitaa au vijiji vyetu kwani hata hii mikutano nayo ni muhimu pia?

Nyinyi mnaotetea Jumuiya hizi niambieni ni lini mlikutana katika Jumuiya zenu hizi na kisha mkaongozana huku mkiwa mbeba sadaka zenu na kwenda kuwahudumia wagonjwa au makelekezo sadaka zenu hizo kuhudumia yatima?

Utaratibu huu nimeuona hapa Dar leo hii nikakumbuka na huko mikoani hali ni hiyo hiyo hivyo nikajikuta najiuliza haya maswali.Alafu katika nchi za wenzetu mambo haya yanafanyika?Nina hakika miaka ijayo haya mambo yatakuja tu kutoweka maana sioni ulazima wake.
Nilikuwa nakuona bonge la "Great Thinker" kumbe PUMBA kabisa!
 
Copenhagen DN vipi huu utaratibu upo huko kusali jumuiya!? sverige SE haupo huu.. why only Africa

Kwahiyo kama Ulaya hawasali jumuiya na watanzania wasisali jumuiya?

Kazi ipo .
Kila kitu unataka kianzie ulaya ,Kikianzia Afrika kibaya.
 
Maybe kuna mtu 'amehack' ID yako sio bure! Wewe kama unadaiwa michango kwenye jumuhiya tafuta hiyo ela ulipe usisingizie muda!
 
Hivi hatuwezi kuishi pasipo kuwa na huu utaratibu wa kusali kwa jumuiya huku mitaani.Kusali makanisani hakutoshi mpaka tukutane kwenye majumba yetu siku za week-end na hata kila siku kwa baadhi ya maeneo kwa lengo tu la kusali kwa utaratibu huu wa Jumuiya?

Wanaocheza pool table wanatakiwa kukamatwa kwani wanapoteza muda wa kufanya kazi,je hawa wanaokutana saa 12 kila Jumamosi na kwa baadhi ya maeneo nasikia ni kila siku,huku si kupoteza muda wa kufanya kazi?

Hivi lengo la kusali Jumuiya si kukusanya sadaka tu?Nini kipya kinachofanyika katika hizi Jumuiya tofauti na makanisani kwetu?

Alafu hivi mtu unawezaje kushiriki kwenye Jumuiya hizi lakini ukashindwa kushiriki mikutano ya kijiji/mtaa kwa maendeleo ya kijiji/mtaa wako?

Kama hizi Jumuiya ni muhimu sana,kwanini adhabu hizi za kijamii tunazozitoa kwa watu wasioshiriki Jumuiya hizi pia tusizitoe kwa wale wasioshiriki mikutano ya maendeleo ya mitaa au vijiji vyetu kwani hata hii mikutano nayo ni muhimu pia?

Nyinyi mnaotetea Jumuiya hizi niambieni ni lini mlikutana katika Jumuiya zenu hizi na kisha mkaongozana huku mkiwa mbeba sadaka zenu na kwenda kuwahudumia wagonjwa au makelekezo sadaka zenu hizo kuhudumia yatima?

Utaratibu huu nimeuona hapa Dar leo hii nikakumbuka na huko mikoani hali ni hiyo hiyo hivyo nikajikuta najiuliza haya maswali.Alafu katika nchi za wenzetu mambo haya yanafanyika?Nina hakika miaka ijayo haya mambo yatakuja tu kutoweka maana sioni ulazima wake.
Mungu akusamehe pasaka hii
 
[
PQUOTE="Chosen generation, post: 15682212, member: 263986"]Nilikuwa nakuona bonge la "Great Thinker" kumbe PUMBA kabisa![/QUOTE]
Jumuiya za kila week-end hazitakupeleka mbinguni bali ni matendo yako.
 
Salary slip naona una shida na matatizo binafsi kuhusu jumuiya.Kama hutaki kushiriki jumuiya acha usiwakwaze wenzio
 
Linapokuja swala la imani watu huwa mbogo lakini kiukweli nyinyi binadamu ni wanafiki wakubwa.Hakuna atakaenda mbinguni kwa kutetea imani yake bali kwa kwa kuheshimu maelekezo ya mwenyezi mungu.

Tunaojifanya kutetea imani zetu ndio wazinzi wakubwa,ndio vinara wa kusaliti ndoa zatu,ndio wezi na mafisadi katika ofisi za umma,ndio wanaotumia imani hizi kuibia waumini wao,ndio wauza madawa ya kulevya n.k.

Huu utaratibu wa kusali kila week-end nyumbani kwa mtu mmoja umepitwa na wakati na ni bora kuwa na utaratibu wa kutenga eneo moja katika mtaa kwa ajili hiyo na iwe mara moja,mbili au tatu kwa mwezi na inatosha kabisa.Tuache kuishi kwa mazoea na kupoteza muda wa kufanya kazi.

Nilijua vichaa wapo milembe tu...

Ukimaliza wakatoliki utaanza na waislamu kwa nini siku nzima wanaswali swala tano

Hapa umechemka
 
Back
Top Bottom