Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
Hivi hatuwezi kuishi pasipo kuwa na huu utaratibu wa kusali kwa jumuiya huku mitaani.Kusali makanisani hakutoshi mpaka tukutane kwenye majumba yetu siku za week-end na hata kila siku kwa baadhi ya maeneo kwa lengo tu la kusali kwa utaratibu huu wa Jumuiya?
Wanaocheza pool table wanatakiwa kukamatwa kwani wanapoteza muda wa kufanya kazi,je hawa wanaokutana saa 12 kila Jumamosi na kwa baadhi ya maeneo nasikia ni kila siku,huku si kupoteza muda wa kufanya kazi?
Hivi lengo la kusali Jumuiya si kukusanya sadaka tu?Nini kipya kinachofanyika katika hizi Jumuiya tofauti na makanisani kwetu?
Alafu hivi mtu unawezaje kushiriki kwenye Jumuiya hizi lakini ukashindwa kushiriki mikutano ya kijiji/mtaa kwa maendeleo ya kijiji/mtaa wako?
Kama hizi Jumuiya ni muhimu sana,kwanini adhabu hizi za kijamii tunazozitoa kwa watu wasioshiriki Jumuiya hizi pia tusizitoe kwa wale wasioshiriki mikutano ya maendeleo ya mitaa au vijiji vyetu kwani hata hii mikutano nayo ni muhimu pia?
Nyinyi mnaotetea Jumuiya hizi niambieni ni lini mlikutana katika Jumuiya zenu hizi na kisha mkaongozana huku mkiwa mbeba sadaka zenu na kwenda kuwahudumia wagonjwa au makelekezo sadaka zenu hizo kuhudumia yatima?
Utaratibu huu nimeuona hapa Dar leo hii nikakumbuka na huko mikoani hali ni hiyo hiyo hivyo nikajikuta najiuliza haya maswali.Alafu katika nchi za wenzetu mambo haya yanafanyika?Nina hakika miaka ijayo haya mambo yatakuja tu kutoweka maana sioni ulazima wake.
NB:Asante Baba Askofu Valentino Mokiwa umeweka wazi unafiki wetu katika imani kupitia mahubiri yako ya leo katika Ibada ya Kitaifa ya Pasaka iliyorushwa live TBC muda mfupi uliopita.
Mliokuwa mnatoka povu hapa mtandaoni naomba muitafue clip ya mahubiri ya Askofu itawasaidia kujua kwanini nasema sisi ni wanafiki sana katika swala zima la imani.