Shamu na Gamba la Nyoka naona mpo kundi mojawapo katika makundi aliyoyasema Eng Burton ... hata hivyo kauli ya ninavykumbuka mimi, nilimsikia akionesha dosari ya katiba yetu tuliyo nayo na si kutishia wananchi wake.
Mimi shida kubwa naoiona katika muktadha wa kipimo cha ulinganifu wa sifa za Nyerere na hali duni ya Tanzania ilivyo leo. Nyerere alisifika sana kwa harakati zake za kulikomboa bara la Afrika, kupigana vita na kumng'oa madarakani dictator Idd, umoja alioujenga kwa watu wake, muungano wa Zanzibar na Tanganyika na siasa yake ya pekee duniani. Je kwanini nini leo nchi iliyojaaliwa kuwa na kiongozi mahiri na wa pekee namna hiyo leo iko chini kisiasa na kiuchumi kiasi cha kufananishwa na kichwa cha mwendawazimu? Nchi inayouza ardhi yake kwa nchi za nje! Nchi inayoruhusu ndege za kijeshi kutua nchini na kuiba wanyama hai? Nchi inayofuga ufisadi na mafisadi wakubwa bila kuchukua hatua zozte! Nchi ambayo wageni ndio matajiri na wanapenyeza katika uongozi wa nchi yetu! Je kwanini ? Haya hayakuwepo wakati wa mwalimu...
Ninavyoona ni kuwa hali hiyo ndio inayozaa maswali magumu yaliyopo sasa ndani na nje ya nchi. Lakini kama wazungumzaji wengie walivyosema, (1) huenda udhaifu wa watawala wa sasa unatafuta kisingizio cha kuficha udhaifu "failure" kubwa katika nchi. Kumbuka habari ya Adam kumsingizia Hawa, na Hawa kumsingizia nyoka ili kuficha uhusika wao kwa kosa walilotenda. (2) Kuna baadhi ya watu (wenye lengo lao) ambao uongozi wa Nyerere uliwadhibiti wao au jamaa zao (kuwagandamiza watu wa Tanganyika, wajinga na masikini), sasa wanapata fursa ya kumlaumu Nyerere kwasababu ambazo hawajaziweka wazi. Hawa watu hawawezi kuona uzuri wa nia njema ya Mwalimu na maamuzi magumu kama kutaifisha mabenki, mashule, mashamba, nk. Wao walitamani ubepari uendelee kuwapa fursa ya kushika njia kuu za uchumi ili washike uchumi wa nchi yetu kibinafsi. Na kinachoendelea sasa hivi ktk sera ya ubinafsishaji na ufisadi ni kufufuka kwa mipango ileile ya zamani.
Mwisho nasema hivi: Kama tuna dhamira safi, naomba tukosoe sera za Nyerere kwa kupendekeza sera mbadala zilizo nzuri zaidi kama zipo. Bila kufanya hivyo tutaishia kuonekana ama tuna chuki dhidi ya Nyerere au tuna sababu nyingine. Na tusisahau kuwa, Nyerere hakuiba hata cent moja ya nchi yetu, kwanini yeye ndiye awe chanzo cha kushindwa kwa nchi badala ya hao wezi waliomfuatia? Serikali ya Nyerere haikuwa na pesa nyingi sana, lakini haikuwahi kufikia uamuzi wa kuuza kipande cha ardhi yake kwa wageni, au kuingia mikataba ya kifisadi iliyopo hivi leo kwenye mali asili ya taifa. Serikali ya Nyerere haikuwahi kuruhusu wageni kujichotea maliasili yetu huku wakionesha dharau kwa wananchi wazawa kwa kuwadhalilisha na hata kuuua, rejea tukio la Merelrani, Nyamongo na sehemu zingine. Kwakweli tusifanye kazi ya kumtetea Baraba na kumhukumu Masihi mwema.
Kumbuka hata kama hakuiba hata cent moja, lakini kawafilisi WTZ kwa sababu ya sera zake za Ujamaa.
Hii quote kutoka ktk well said article ambayo inazungumzia pia kuhusu Ujamaa wa Nyerere na Udictator wake.
Three of these factors are pertinent to this discourse. Firstis the argument that the initiative to start Ujamaa villages did not comefrom rural peasants. The scheme failed to gain the necessary ideologicalacceptance among the vast majority of the peasantry. Right from the beginning,the dominant attitudes of the people ranged from skepticism and mistrustto outright resentment and opposition (Lofchie, 1978: 452). Secondly,the use of coercion to ensure mass villagization - from threats of forcedtransportation to short prison sentences under the pretext of tax arrears -militated against the effective operation of Ujamaa villages. Finally, theefforts at building Ujamaa villages were greatly constrained by bureaucratswho held out government aid as incentives to peasants to move into villages.Peasants began to perceive such "free goods" as substitutes for availablelabor resources rather than being complimentary factors for increasedproduction. Promises of official assistance resulted in an over-dependenceof the villages on government initiatives and incentives that left villagesextremely vulnerable when government assistance eventually stopped.However, perhaps the single most adverse limitation of the Ujamaa villagizationprogram was the practice which Shivji (1974) and Raikes (1975)have described as "Kulak Ujamaa". This was a practice in which a numberof rich peasants, having attained positions in Ujamaa village committees orforged links with local bureaucrats, began to use the villages to further theirown interests.
Kwa hiyo ukisoma hiyo article vizuri utagundua haya matatizo yote yalianzia wakati wa Nyerere.