Wanaoisema vibaya serikali mitandaoni kukiona

ok, Huyu Masauni anafahamu katiba ya Jamhuri ya muungano au anatumia katiba ya Zanzibar?

Mwambieni Masauni alikuwepo Ole Sabaya na Ally Happy wao waliapa kiwashughulia viongozi na Raia yeyote anayemsema Rais wa wakati huo vibaya, Ally Happy alienda mbali na kusema Yeye ni mtu hatari, Sasa Leo uhatari wake akafanyie huko Ukraine au Afaghanstan

Mwambieni Masauni watu hatari na wenye vitisho wanahitajika huko na Putin wakapigane mstari wa mbele dollar 7000 na mstari wa nyuma dollar 3500, Kama hana jipya kwenye uongozi apishe watu Wengine asitake kufunga watu midomo ya kuongea na Kutengeneza Taifa linalogawanyika

Mwambieni huku bara katiba inaruhusu watu kuongea wanachotaka bali wasivunje sheria, Mwambieni Zanzibar watu wa huku bara wanatubania ardhi ya kujenga

Mwambie Masauni kuna mambo ya msingi ya kuelimisha watu wake kama PGO, Atumie muda kuwaelekeza watu wake mambo ya PGO na kutenda haki

Mwambieni Masauni awe anasikiliza kauli za Rais kuwa Jeshi la polisi lishughulike na mambo yake ya msingi wasitoke kwenye lengo la kuanzisha Jeshi la polisi

Hivi watu bado hawakujifunza awamu ya tano ya JPM kuwa haya mambo yalitengeneza chuki mpaka kwa mara ya kwanza watanzania wakaanza kufurahia vifo vya viongozi wa kisiasa

Hapa JF tu watu walitoa kauli za kuombea Viongozi wafe kwa korona. Na viongozi waliokufa watu walishangilia

Angekuwa mkristu masauni ningesema kwanini Wagalatia mna roho ngumu na mmeweka pamba masikioni

Sasa huyu ustadh Masauni ameshaanza kupandisha mabega tena, Naona Masauni Mabega yameanza kupanda sasa

Tumkumbushe masauni alikuwepo Kangi Lugola yeye alivaa mpaka bendera ya Taifa na alitembea na ilani mitaani kama anaeneza injili

Hiyo wizara Kangi Lugola alishona suti zenye Rangi ya bendera ya Taifa

Ni muhimu viongozi wakakumbuka nchi imepita wakati gani

Hawa watu mambo yakiwa magumu wanaanza kuwalilia viongozi wa dini wawashauri wananchi

Masauni aache viongozi wa dini wapumzike, Tumechoka na makongamano ya Amani kila wakati na upatanisho wa kisiasa

Rais alishasema watu waongee, Yeye ameshajisahau anaingilia mamlaka ya Rais

Mwambieni Masauni mabega hayakuzidi kichwa

Mwambieni Masauni Ally Happy aliapa atawafundisha adabu akina Jakaya Kikwete na wastaafu kisa walitoa maoni yao kuhusu maoni hayapigwi Lungu

Mawaziri mjikite kwenye mambo ya msingi yenye kuleta mabadiliko, Mambo ya kufukuzana na watu wanaotoa maoni hasi kama Panya Buku huko Twitter, Clubhouse, Facebook sio lengo la Rais Samia

Kangi Lugola alitumia miaka yote kumfukuzia Kigogo wa Twitter haya sasa kigogo huyo huyo Leo ni mwana ccm kuliko Kangi Lugola, Maoni hayapigwi Lungu( By Jakaya Kikwete)

Mwambieni Masauni tunahitaji gharama alizotumia Kangi Lugola kumtafuta Kigogo wa Twitter,

Watu Wanalalamika tozo, Masauni anaongelea kuingia gharama za kuweka mifumo ya watu wanaomtania na kumsema Rais Samia

Mwambieni Masauni asitumie tozo za wananchi kwa mambo ya utani, kejeli na masihara mtandaoni ya wananchi kwa Rais wao
Tumemwambia umeharisha.
 
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh Hamad Masauni, amewaonya wale wote wanaoisema vibaya serikali ya awamu ya 6 Mitandaoni, ambapo ameliomba jeshi la polisi kuimarisha mifumo yake (ya utambuzii) kwa kushirikiana mamlaka zingine ili kukomesha jambo hilo.

Mh. Masauni amesema wanazo Taarifa kwamba kuna watu wameandaana makundi ya vijana waliopewa kazi ya kutukana serikali mitandaoni.

Mh. Waziri ameyasema hayo wakati wa kumkaribisha Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ili kufungua kikao cha viongozi wa polisi mkoani Kilimanjaro.

Kazi Iendelee.
Ukweli huwa unauma sana. Wanataka kuziba midomo watu wanasema madudu yao hadharani ili wote aanze kuwasifu kwa nyimbo na mapambio.
 
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh Hamad Masauni, amewaonya wale wote wanaoisema vibaya serikali ya awamu ya 6 Mitandaoni, ambapo ameliomba jeshi la polisi kuimarisha mifumo yake (ya utambuzii) kwa kushirikiana mamlaka zingine ili kukomesha jambo hilo.

Mh. Masauni amesema wanazo Taarifa kwamba kuna watu wameandaana makundi ya vijana waliopewa kazi ya kutukana serikali mitandaoni.

Mh. Waziri ameyasema hayo wakati wa kumkaribisha Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ili kufungua kikao cha viongozi wa polisi mkoani Kilimanjaro.

Kazi Iendelee.
Wanajistukia..
 
Mungu isaidie Tanzania ipate viongozi wenye utimamu sahihi.

Badala ya serikali kuwahimiza watendaji wake kujibu hoja za wananchi hata mitandaoni, yenyewe inajipanga kjwadhibiti wanaohoji madudu ya watendaji huku ikiwabrand wanaitukana serikali?

Hivi hawa kina Masauni wanamheshimu Rais kweli au ndo vile wamejipanga kumuangusha kiutendaji ndo waje na kauli za kipuuzi namna hii?

Mungu isaidie Tanzania
 
Serikali yoyote ile ikishindwa kuealetea maendeleo wananchi inaanza kuwabambikia kesi wananchi. Mnamkumbuka Moi na pale underground nyayo house ambapo Sasa hivi Ni museum? Je nduli? Au Lungu, Banda je?
 
Safi sana Kuna majasiri na wababe wa nyuma ya keyboard ndio tunataka tuwaone
 
Ogopa sana watu wanaoumizwa halafu wako kimya wanalilia kwenye mioyo yao. Heri wakisema wanapunguza sumu.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Wanadhani kufanya hivyo ni kuondoa tatizo.

Kumbe ni kutengeneza jingine.

Waache watu uhuru wa kuongea kila kitu itapunguza mambo mengine.

Ila wakiendelea kuwabana sana,wataingia barabarani na kitakachotokea watakumbuka kuwa bora wangewaachia waendelee kutoa maoni yao mitandaoni.
 
Back
Top Bottom