BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,370
- 8,107
Waziri Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni ametoa agizo hilo baada ya kumalizika muda aliotoa kwa wamiliki wa Mabasi kufunga vifaa vya Mfumo wa Kufuatilia Gari (VTS) au GPS Tracker ili kudhibiti ajali.
Masauni amelitaka Jeshi la Polisi na Baraza la Taifa laUsalama Barabarani kuhakikisha wanayakamata mabasi yote yaliyokiuka utekelezaji wa agizo hilo.
Takwimu za ajali kutoka Jeshi la Polisi zinaonesha kati ya January hadi August 2022 watu 1,038 walifariki katika ajali 1,117 huku Magari ya Serikali yakiwa ni 11,5%.
=======================
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini na Baraza la Taifa na Usalama barabarani kuhakikisha wanayakamata mabasi yote yasiyo na vizibiti mwendo
Masauni amesema hayo wakati akizindua baraza la Taifa la Usalama Barabarani makao makuu ya Nchi Dodoma ambapo, amesema miongoni mwa vyanzo vya ajali Nchini ni mwendo kasi unaosababishwa na madereva wazembe wasio fuata sheria za usalama barabarani kitendo kinachopelekea ajali nyingi hapa Nchini
Pia Maasauni ameliagiza Jeshi la Polisi kuanzia l24 October kukamata mabasi yote yasiyo na vizibiti mwendo ambapo amesema kuwa tayari alishatoa maelekezo hayo kuwa ifikapo September mwka huu mabasi yote yawe na vizibiti mwendo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jamanne Sagini ambaye Pia ni Mwenyekiti wa Balaza la Taifa la Usalama barabarani amesema baraza la Taifa la Usalama barabarani kwa kushirikiana na baraza la kazi litaendelea kutoa mafunzo ya Usalama barabarani kwa viongozi wa umma wakiwemo makatibu wakuu na wabunge ili kuwajengea uwezo wa kukemea matukio amabayo yanapelekea ajali kutokea.
Nae Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Atupele Mwakibete ambaye ni kaimu Mwenyekiti wa baraza hilo, amemshukuru Waziri Masauni kwa kumteua kuwa katika baraza hilo ambapo ameahidi kwakushirikiana na baraza na wadau wa Usalama barabarani na kutatua changamoto zilizopo
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Wilbroad Mutafugwa amesema kuwa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani toka limeanzishwa kusimamia kamati za Mikoa na Wilaya umesaidia ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya fedha zilizotokana na ada za ukaguzi wa magari mbalimbali.
MICHUZI BLOG