Mkuu Vivanet, kweli kwa Kiswahili Mayalla ni njaa ila sio ile njaa ya kuhitaji shibe au mlo no njaa ya baa la njaa, famine, linalotokana ukame, draughts katakana na mabadiliko ya tabianchi.
Baada ya kuiona kasi yake aliyoanza nayo, hatuna haja ya kusubiri, miaka kumi ni michache haitoshi kunyoosha vizuri nchi ikanyooka.
Maadam wanaotaka aongezewe muda sio yeye bali ni watu, na katiba ni ya watu, na walioweka ukomo kwenye katiba ni watu, hivyo watu wakiamua kuuondoa ukomo, watauondoa tuu, kwa sababu katiba sio msahafu kusema haibadilishwi.
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia yenye katiba ya watu iliyotengenezwa kidemokrasia na kuongozwa na watu, hivyo tuna serikali nzuri ya watu, inayoongozwa na watu, kwa manufaa ya watu, "of the people, by the people and for the people", we the people, tukiamua Magufuli aongezewe muda, ataongezewa muda!.
Nia tunayo, uwezo tunao na sababu tunazo. Nimezieleza humu
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Na 2025 akiamua mwenyewe kupumzika, tuneshauri Makonda aandaliwe kumpokea
.
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze....
Paskali