Wanaodai rais kuongezewa muda sio wachochezi?

Watanzania wenzangu tusicheze na mambo yanayoonekana kama mzaha, kumbe ndani yake kuna maafa.

Zaburi 1:1 heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki, wala hakusimama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

Swala hili la Rais kuongezewa muda limeanza kushika kasi kiasi kwamba tumelichukulia kama utani tu na mzaha, ila ukweli ni huu matamshi yote yanayotamkwa ya kumuongezea Rais muda ni uchochezi maana yanaenda kinyume na katiba. Je kama watu wangejitokeza na kusema Rais apunguziwe muda, vyombo vya dola vingechukulia kuwa ni mzaha na utani au mtu huyo angechukuliwa hatua za kisheria?

Je kama wangejitokeza watu wakabeba mabango yaliyoandikwa tunaomba bunge libadilishe vifungu vya katiba Rais apunguziwe muda wa kutawala iwe miaka mitatu tu, vyombo vya dola vingewavumilia?

Kumbukeni wakina Mgabe, Kagame na Museven walipata watu wachache walioanza kuchochea hivyo kuwa waendelee kuongoza na matokeo yake wamefanya hivyo.

Hatujaona Rais akikemea watu hao wanaotoa matamko ya kuvunja katiba na kuchochea fikra za watanzania, maana imani huja kwa kusikia.

Wanaosema Rais aongezewe muda sio wachochezi?
Tena washtakiwe kwa kuvunja KATIBA ya JMT
 
Waende wakamuulize graduate wa arts ambae wazaz wake wote wamekumbwa na ishu ya vyet feki kama anakubaliana na rais kuongezewa mda wa utawala
 
NGOJA AMALIZE MIAKA KUMI, NDIPO TUTAAMUA KUMPA MIAKA MINGINE KUMI, KILA JAMBO HUJA KWA WAKATI WAKE. ENYI UKAWA MSIWEWESEKE. TUTAKAPOAMUA TUMEAMUA HAKUNA WA KUTUZUIA.
Watanzania wenzangu tusicheze na mambo yanayoonekana kama mzaha, kumbe ndani yake kuna maafa.

Zaburi 1:1 heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki, wala hakusimama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

Swala hili la Rais kuongezewa muda limeanza kushika kasi kiasi kwamba tumelichukulia kama utani tu na mzaha, ila ukweli ni huu matamshi yote yanayotamkwa ya kumuongezea Rais muda ni uchochezi maana yanaenda kinyume na katiba. Je kama watu wangejitokeza na kusema Rais apunguziwe muda, vyombo vya dola vingechukulia kuwa ni mzaha na utani au mtu huyo angechukuliwa hatua za kisheria?

Je kama wangejitokeza watu wakabeba mabango yaliyoandikwa tunaomba bunge libadilishe vifungu vya katiba Rais apunguziwe muda wa kutawala iwe miaka mitatu tu, vyombo vya dola vingewavumilia?

Kumbukeni wakina Mgabe, Kagame na Museven walipata watu wachache walioanza kuchochea hivyo kuwa waendelee kuongoza na matokeo yake wamefanya hivyo.

Hatujaona Rais akikemea watu hao wanaotoa matamko ya kuvunja katiba na kuchochea fikra za watanzania, maana imani huja kwa kusikia.

Wanaosema Rais aongezewe muda sio wachochezi?
 
Vivianet, sometimes you have to swallow the bitter with sweet, ili ukombozi wa kweli upatikane sometimes lazima watu wale mijeledi, wateswe na kuteseka, na ni kwa kupigwa kwao sisi tunaponywa. Ili kupata dhahabu safi, lazima kwanza ipitie kwenye tanuru la moto. Magufuli anaipitisha nchi kwenye tanuru la moto kuisafisha dhahabu yake, ikitoka itakuwa ni dhahabu safi, tatizo rundo la dhahabu chafu ni kubwa sana kwa muda uliopo kuisafisha, hivyo tunampigia chapuo akae as long as it takes kusafika, kama atahitaji muda kama Kagame, Museveni au Mugabe, let it be!.

P.
si lazima kila kitu afanye yeye atuachie mifumo ya kuendeleza alichokianzisha muda wake ukiisha.
uongozi ni mbio za vijiti na utamaduni huu tunao tayari itatumika nguvu sana kuukiuka utaratibu huu.
 
NGOJA AMALIZE MIAKA KUMI, NDIPO TUTAAMUA KUMPA MIAKA MINGINE KUMI, KILA JAMBO HUJA KWA WAKATI WAKE. ENYI UKAWA MSIWEWESEKE. TUTAKAPOAMUA TUMEAMUA HAKUNA WA KUTUZUIA.

Sasa kama mnajua hivyo kwa nini mmeanza kuchochea mnahitaji kuchukuliwa hatua za kisheria
 
Back
Top Bottom