Wanaodai rais kuongezewa muda sio wachochezi?

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,131
2,000
Watanzania wenzangu tusicheze na mambo yanayoonekana kama mzaha, kumbe ndani yake kuna maafa.

Zaburi 1:1 heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki, wala hakusimama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

Swala hili la Rais kuongezewa muda limeanza kushika kasi kiasi kwamba tumelichukulia kama utani tu na mzaha, ila ukweli ni huu matamshi yote yanayotamkwa ya kumuongezea Rais muda ni uchochezi maana yanaenda kinyume na katiba. Je kama watu wangejitokeza na kusema Rais apunguziwe muda, vyombo vya dola vingechukulia kuwa ni mzaha na utani au mtu huyo angechukuliwa hatua za kisheria?

Je kama wangejitokeza watu wakabeba mabango yaliyoandikwa tunaomba bunge libadilishe vifungu vya katiba Rais apunguziwe muda wa kutawala iwe miaka mitatu tu, vyombo vya dola vingewavumilia?

Kumbukeni wakina Mgabe, Kagame na Museven walipata watu wachache walioanza kuchochea hivyo kuwa waendelee kuongoza na matokeo yake wamefanya hivyo.

Hatujaona Rais akikemea watu hao wanaotoa matamko ya kuvunja katiba na kuchochea fikra za watanzania, maana imani huja kwa kusikia.

Wanaosema Rais aongezewe muda sio wachochezi?
 

sir longo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
1,072
2,000
acha woga ww, hata miaka mitano hajamaliza mmeanza kuweweseka. tulieni raisi afanye kazi.
 

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
5,477
2,000
acha aongezewe tu kwni inakuuma nn?!!maana anafanya vizuri
 

HesabuKali

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
2,169
2,000
Kama limesemwa na CCM ni halali kabisa, hebu jaribu kuota tu kama Rasi hatagombea tena 2025 ukapajue central japokuwa kikatiba 2025 hawezi kugombea ila utaitwa mchochezi na unahatarisha amani kwani huko Namtumbo Songea, kanda ya ziwa na Mzee Mwinyi wameomba aongezewe muda, sasa kwanini wewe hujasubiri maamuzi ndio uote?
 

Alfan issa

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,163
2,000
Aongezewe tu ili mzidi kunyooka maana hamna namna, kama ameweza kuweka ndan mafisadi nguli we unafikir mchezo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom