Wanaodai rais kuongezewa muda sio wachochezi?

Wanaodai rais kuongezewa muda sio wachochezi?

Uchochezi kama huu ulitokea wakati awamu ya pili ikikaribia kuisha ambapo baadhi ya watu akiwemo marehemu Horace Kolimba (katibu Mkuu wa CCM enzi hizo) walijenga hoja kuwa Mzee Ruksa aongezewe muda wa urais. Aliyemaliza huo ulevi wa madaraka enzi hizo alikuwa ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alieleza kuwa wale waliopendekeza muda uongozwe walifanya hivyo kwa manufaa yao binafsi na siyo manufaa ya nchi wala raisi aliyekuwa madarakani Enzi hizo yaani Mzee ruksa. Na lisisitiza kuwa hata yeye kuna watu walimshauri kuwa asing'atuke kwa sababu nchi ilikuwa bado changa kwa yeye kung'atuka. Baadaye aligundua kuwa nchi walizokuwa wakiongelea hao wapambe zilikuwa ni familia zao na siyo Tanzania.
 
Kazi ya DCI kwa sasa ni kuchunguza kauli ya uchochezi ya mamvi, Haya ya kwenye thread yako yasubiri kwanza. Ova
 
acha aongezewe tu kwni inakuuma nn?!!maana anafanya vizuri


Kwani akili zako zina ukubwa gani kaka yangu? unashindwa kuchangia mada unaropoka tu. kwani walioweka katiba walikuwa wanaumwa nini kuamua iwe kipindi cha miaka mitano mitano?
 
Mnafikiri magufuli akibadili katiba,jumuiya za kimataifa zitamuacha salama?mtawekewa vikwazo zaidi ya zimbabwe.njaa kali,pesa hamna,uchumi umekufa,hela haina thamani.
UNAFIKIRI KUNA MTU ATAINGIA BARABARANI TENA KUMSAPOTI MAGUFULI?
MTAJUTA.
 
Mnafikiri magufuli akibadili katiba,jumuiya za kimataifa zitamuacha salama?mtawekewa vikwazo zaidi ya zimbabwe.njaa kali,pesa hamna,uchumi umekufa,hela haina thamani.
UNAFIKIRI KUNA MTU ATAINGIA BARABARANI TENA KUMSAPOTI MAGUFULI?
MTAJUTA.


Tanzania ikiwekewa vikwazo watakao umia ni wapinzani maana ccm wanaishi kwenye miji tofauti na wapinzani.
 
Kama mnajua hajamaliza miaka mitano nini kinawasukuma kudai aongezewe muda? hivi mna kiwewe cha nini?
Na angetokea wa kutaka apunguziwe muda hata mwezi mmoja kwenye hiyo miaka mitano,angekuwa amesha kamatwa,kwa uchochezi!
 
Wakoromije nawaona wengi wengi hapa, sijui kiswahili kigumu, hawajui kusoma, au tatizo liko wapi? Maana maada inasema hivi mtu anajibu vile, duh!!
 
Inanikumbusha kipindi kile 2014/2015 makundi mbalimbali kuandamana kumuomba Lowassa achukue form kupitia CCM,naona team JPM wanaorganise the same move.
 
Tanzania ikiwekewa vikwazo watakao umia ni wapinzani maana ccm wanaishi kwenye miji tofauti na wapinzani.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] waache tu wajiroge.magufuli kaingia kwa katiba.SIO MAPINDUZI.sasa mdanganyeni.mje muone cha moto.na vile hsmjawahi kuwekeweka vikwazo.mtamchukia mapema.
 
Mara ya mwisho kusikia hilo neno la kuongezewa muda, nakumbuka nilizima Tv na sikutana tena kufuatilia jambo hilo,,,,nilikereka sana nakumbuka
 
Hivi mtu anaeshawishi katiba ivunjwe anaitwaje vile?

Je wakijitokeza wengine wakitaka kuandamana kwamba muda wa Raisi upunguzwe watabaki salama?

Viongozi tumieni mizania zenye uzito sawa pande zote
 
Back
Top Bottom