Wanaochelewa kurudi nyumbani sio wajinga

Wanaochelewa kurudi nyumbani sio wajinga

familia zipo tofauti, wanafanya hivo wenye wake wasiojielewa, wengine hurudi mapema ajili yakukaa na watoto nakuwafunza.
Yeye hawezi kuwafunza watoto? Kwanzaa hiyo ni kazi ya mwalimu shuleni. Nyumbani mke kazi yake ni kukumbusha watoto kumalizia homework
 
Siku asipokusaidia unajisikiaje?
Kawaida tu kwasababu natambua hilo ni jukumu langu kama mama na mke yeye anafanya msaada wa hiyari tu kama baba ili aweke mchango wake kwa malezi ya mtoto. Asipofanya haimaanishi kwamba hajali hapana atafanya mengine ya muhimu pia hata kama yasipohusika na majukumu ya nyumbani. Ni swala la kujitambua tu nafasi yako kama mke na mama na kama baba na mume. Mfano kama kuna tatizo linaitaji ela mama anazo ina maana hawezi kutoa mpaka baba aje kisa nijukumu lake kuhudumia familia ? Ni kusaidiana katika kila jambo na kila mtu atambue mipaka yake pia tusivuke mipaka.
 
Kuna jirani yangu ni fundi seremala ofisi yake haipo mbali na kwake. Siku moja kaamua kujiongeza na kubandika maharage mkewe alikua katoka, mkewe karudi akafurahi kweli. Siku nyingine mwamba kaendelea na shughuli zake mkewe alikua katoka bahati mbaya this time hakubandika maharage. Mkewe karudi kaanza kummind kwa nini hakufanya kama mwanzo na kuanza kuropoka kwa sauti. Bibi alitembezewa makonzi hayo Uchebe akasome.
Uchebe akasome [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kawaida tu kwasababu natambua hilo ni jukumu langu kama mama na mke yeye anafanya msaada wa hiyari tu kama baba ili aweke mchango wake kwa malezi ya mtoto. Asipofanya haimaanishi kwamba hajali hapana atafanya mengine ya muhimu pia hata kama yasipohusika na majukumu ya nyumbani. Ni swala la kujitambua tu nafasi yako kama mke na mama na kama baba na mume. Mfano kama kuna tatizo linaitaji ela mama anazo ina maana hawezi kutoa mpaka baba aje kisa nijukumu lake kuhudumia familia ? Ni kusaidiana katika kila jambo na kila mtu atambue mipaka yake pia tusivuke mipaka.
Wanawake wenzio walioko humu humu tu hawawezi kununua hata luku incase imeisha kabla baba hajarudi. Unakutana na giza kama vile mama hawezi nunua umeme na sio kwamba hela hana ni ubinafsi tu.

Hongera sana kama ni kweli unayaishi uliyoongea. Hakika wewe ni mwanamke wa mfano wa kuigwa kabisa.

Mwingine akisaidiwa jukumu anataka kuligeuza liwe lako na usipofanya anazira kabisa. Hii ndio sababu ya kuwakwepa tu na kurudi mida mibovu. Pia drama za kijinga haziepukiki ukikaa na mwanamke mda mrefu.
 
Ishu sio kuwahi kurudi nyumbani. Ishu ni umekosea kuoa mzeee. Umeshindwa kusimamisha utawala kama baba uonekane wew baba muda wote,na nafasi yako ya kiutawala ionekane.

Hata ukichelewa kurudi nyumbani, ukishindwa kusimamisha utawala wa baba, utakuja na hoja zingine, USIRUHUSU MKEO AFANYE KAZI, MKE AKIZINGUA MPIGE MAKOFI.

Story nyingi za kichief utaona tu, chief yupo mitaa ya utawala wake nyumbani, vipi na yeye alikuwa anapangiwa kazi,mzee. Chief mbali babu zetu, walikuwa akitoka mishe zake, kulima,kuwinda, hushinda nyumbani na kutoka jioni kwenda kupasha akili, vipi nao walikuwa wanapangiwa kazi.

Tengeneza mazingira uongozi wa baba uonekane, kumbuka mke ni rafiki yako, pia. Kuna matendo ya kuongeza au ku show love, ajue unafanya hayo kwa ajili hiyo. Kama anapika una msaidia hili au lile,ni way tu kukuza chemistry yenu.

UNAKIMBIA KUTULIA KWAKO KISA UNAOGOPA MKEO ATAKUTUMA, NANI MTAWALA SASA HAPO. KUWA HOME, TUMIA AKILI KUMTALA.
 
Sijaolewa bado. Siwezi kumtuma kaka yangu au mdogo wangu wa kiume achambue mchele au kukata kitunguu wakati napika. Sembuse mume 🍆

Daah natamani uwe ubavu kwangu....

Nyumba ni tanuri la Moto kwa wanaume waliokosea kuoa (unaoa mwanamke shepu kichwani hajitambui hana haibu wala huruma)....Ila mwanamke anaejitambua atahakikisha hambughudhi mume wake na atafanya nyumba ndo bustani ya mumewe...yaani ata Kama kachoka mumewe usiku akihtaji mechi atampatia bila kinyongo wala maneno.
 
Yeye hawezi kuwafunza watoto? Kwanzaa hiyo ni kazi ya mwalimu shuleni. Nyumbani mke kazi yake ni kukumbusha watoto kumalizia homework
baba wenye mawazo yako mara nyingi matoto yao hua tegemezi hadi uzeeni na mara nyingi hutamani ufe ili yajimilikishe mali zako, be care with ur family ucreat misingi bora itakayowawezesha kujitegemea mapema after school.
 
Mwanaume hakikisha unafika nyumbani kwako angalau kuanzia saa moja na nusu kwenda juu lakini usichelewe sana. Kimsingi mwanaume aliyeoa anatakiwa kuwa nyumbani kati ya saa moja na nusu na saa tatu japo wengine mpaka saa tano au saa sita. Hiyo sio nzuri

Ila ni kosa namba moja kwa mwanaume kurudi nyumbani saa kumi sijui saa kumi na moja, ukiwahi kurudi nyumbani na umekaa tu mke wako ataanza kukupa kazi zake umfanyie. Wewe kama mwanaume utaona anazingua, usipofanya ataona humpendi na ukizifanya atazifanya kuwa majukumu yako na inaweza kufika hatua atataka mpangiane mpaka zamu ya kudeki nyumba.

HASARA ZA MWANAUME KUWAHI KURUDI NYUMBANI NI PAMOJA NA....
1. " Sijisikii vizuri, nisaidie kuosha nyombo...."
2. " Sisi tunapika, we kanunue chumvi na nyanya..."
3. "Unapoangalia TV hapo nikuletee mchele uuchambue...."
4. " Kumbe ulifika mapema, mbona hujapika sasa...."
5.
6.
7.
8. Malizieni nyingine......

Hawa ndugu zetu ukiwafulia nguo leo basi atataka kila siku ufue, ukiosha vyombo leo atataka kila siku uoshe. Sasa wewe endelea kujifanya unawahi kurudi nyumbani mapema ukaona kwamba ni baba bora kumbe unabomoa nyumba yako, "UKIONA WANAUME WANACHELEWA KURUDI NYUMBANI UJUE SIO WAJINGA"
Hapo unakuwa umeoa au mmeoana!? Mnawatoaga wapi wa hivyo!?
 
naunga mkono hoja.

kuna watu wanabisha hapa, ila ukweli damu nzito kuliko maji, kitendo cha kurudi mapema mke akaaanza kulalamika amechoka kwa pilika za mchana, watoto(hasa kama wadogo bado),usafi wa nyumba nk. akikuomba msaada hata wa kusugua fridge chafu huweze kataa.

so ili kuzuia hilo, pata dharula ya kiwahi kurudi kila siku, ikiwezekana boss awe na kikao kila baada ya muda wa kutoka,ila epuka sana kurudi na harufu ya pombe.
 
baba wenye mawazo yako mara nyingi matoto yao hua tegemezi hadi uzeeni na mara nyingi hutamani ufe ili yajimilikishe mali zako, be care with ur family ucreat misingi bora itakayowawezesha kujitegemea mapema after school.
Baba kuwapetiti watoto kuanzia jioni baada ya kutoka kazini haisaidii kuwaandaa wajitegemee baadaye. Watch out! Kwanza ndo mwanzo wa kuwadekeza.
 
yani nimesoma comments za humu nimebaki hoi, hv kufanya majukumu ndani ya nyumba yenu ni kumsaidia mwanamke? unanisaidiaje kwa mfano wakati hicho chakula tunakula wote? hivyo vyombo hata wewe unatumia? usafi wa nyumba hata wewe unakuhusu mana ndimo unapoishi, sasa iweje mwanaume useme eti kufanya hayo ni kusaidia? kwani mnaoa ili mpate wafanyakazi wa ndani au partner wa maisha? yani wote tunatoka asubuhi kwenda kutafuta maisha, tunarud nyumbani jioni wote tumechoka, badala ya kusema niwahi tukasaidiane na mwenzangu eti unachelewa kisa utatumwa kazi, sasa ulitakaje? kwani punda wako huyo? Aisee nashukuru kwa mume niliyenae nyumbani anawahi kurudi vzr sana na kama kuna cha kufanya atafanya tu, sijawahi kumsikia anaongea utaopolo eti ananisaidia.

Isitoshe, mimi kwetu tumezaliwa wa4 wakike wawili na wakiume wawili, wazazi wetu walitulea kwa USAWA wote tulikuwa tunazamu za kazi za ndani kuanzia usafi hadi kupika, hakukuwa na kazi eti hii ya mwanamke hii ya mwanaume
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom