Wanaochelewa kurudi nyumbani sio wajinga

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,526
3,801
Mwanaume hakikisha unafika nyumbani kwako angalau kuanzia saa moja na nusu kwenda juu lakini usichelewe sana. Kimsingi mwanaume aliyeoa anatakiwa kuwa nyumbani kati ya saa moja na nusu na saa tatu japo wengine mpaka saa tano au saa sita. Hiyo sio nzuri

Ila ni kosa namba moja kwa mwanaume kurudi nyumbani saa kumi sijui saa kumi na moja, ukiwahi kurudi nyumbani na umekaa tu mke wako ataanza kukupa kazi zake umfanyie. Wewe kama mwanaume utaona anazingua, usipofanya ataona humpendi na ukizifanya atazifanya kuwa majukumu yako na inaweza kufika hatua atataka mpangiane mpaka zamu ya kudeki nyumba.

HASARA ZA MWANAUME KUWAHI KURUDI NYUMBANI NI PAMOJA NA....
1. " Sijisikii vizuri, nisaidie kuosha nyombo...."
2. " Sisi tunapika, we kanunue chumvi na nyanya..."
3. "Unapoangalia TV hapo nikuletee mchele uuchambue...."
4. " Kumbe ulifika mapema, mbona hujapika sasa...."
5.
6.
7.
8. Malizieni nyingine......

Hawa ndugu zetu ukiwafulia nguo leo basi atataka kila siku ufue, ukiosha vyombo leo atataka kila siku uoshe. Sasa wewe endelea kujifanya unawahi kurudi nyumbani mapema ukaona kwamba ni baba bora kumbe unabomoa nyumba yako, "UKIONA WANAUME WANACHELEWA KURUDI NYUMBANI UJUE SIO WAJINGA"
 
Kuna jirani yangu ni fundi seremala ofisi yake haipo mbali na kwake. Siku moja kaamua kujiongeza na kubandika maharage mkewe alikua katoka, mkewe karudi akafurahi kweli. Siku nyingine mwamba kaendelea na shughuli zake mkewe alikua katoka bahati mbaya this time hakubandika maharage. Mkewe karudi kaanza kummind kwa nini hakufanya kama mwanzo na kuanza kuropoka kwa sauti. Bibi alitembezewa makonzi hayo Uchebe akasome.
 
Dah! Yaani niwahi kurudi halafu anitume kazi za kupika!!!??
Mm hawezi hata kuthubutu kutamka hayo.

Lakn pia kuwahi nyumbani ndio mambo ya kuanza kuchunguzana mpaka kwenye simu. Muda sahihi Wa mwanaume kurudi ni saa mbili mpaka saa NNE.
 
Kuna jirani yangu ni fundi seremala ofisi yake haipo mbali na kwake. Siku moja kaamua kujiongeza na kubandika maharage mkewe alikua katoka, mkewe karudi akafurahi kweli. Siku nyingine mwamba kaendelea na shughuli zake mkewe alikua katoka bahati mbaya this time hakubandika maharage. Mkewe karudi kaanza kummind kwa nini hakufanya kama mwanzo na kuanza kuropoka kwa sauti. Bibi alitembezewa makonzi hayo Uchebe akasome.
 
Kuna jirani yangu ni fundi seremala ofisi yake haipo mbali na kwake. Siku moja kaamua kujiongeza na kubandika maharage mkewe alikua katoka, mkewe karudi akafurahi kweli. Siku nyingine mwamba kaendelea na shughuli zake mkewe alikua katoka bahati mbaya this time hakubandika maharage. Mkewe karudi kaanza kummind kwa nini hakufanya kama mwanzo na kuanza kuropoka kwa sauti. Bibi alitembezewa makonzi hayo Uchebe akasome.
Wanawake sio wa kuwaendekezaa mkuu..!!
 
Mhhh inategemea na jinsi mnavyoishi na mke uliyenae. Mume wangu anarudig saa moja na nusu mpaka saa mbili na akikuta kuna baadhi ya vitu havijakaa sawa huwa anasaidia hasa upande wa mtoto kama kumlisha na kucheza nae ili mimi mke nifanye shughuli nyengine za upishi ukizingatia cna msichana wa kazi. So kusaidia mambo ya nyumbani ni hulka tu ya mtu sio wote wanaopenda kuishi kiboss kisa tu wameoa basi ndo kamaliza kila kitu mke afanye hapo ukute na mke nae anamajukumu ya kikazi au biashara.
 
Siku asipokusaidia unajisikiaje?
 
Nadhani hapa inategemeana na wana ndoa nyie mna tabia gani' mimi nyumbani kwetu Baba alikua anarudi saa9 toka kazini na alikua afisa wa serikali anabadili na kutoka tena ni mnywaji saa11 yuko home anakula na kutulia tu akifanya vitu vyake toka nnasoma primary mpaka namaliza High School na sikuwahi kuona Mama anampa kazi zake za nyumbani Mzee hata kwenda dukan kununua chumvi au soda sikuwahi kuona.

Hapa inategemea na kuzoeshana kwenu na pia kila mtu afahamu majukumu yake ndani ya ndoa yaan hata kama mwanamke ni mfanyakazi lazima pia atambue majukumu yake kama mwanamke ndani ya nyumba na pia mwanaume lazima afahamu majukumu yake ndani ya nyumba' angalizo kusaidiana ndani ya nyumba ni muhimu kwani pia upendo huongezeka baina ya wanandoa na pia ni namna ya kupeana unafuu na mapumziko baina yenu.
 
Back
Top Bottom