Pole sana ndugu yangu. Naamini hutoi na kujiumiza mwenyewe.
Kwa upande wangu, siwezi kumlaumu mke wangu kwa jinsi yoyote atakavyowatendea ndugu. Hata mimi nilikuwa na mawazo kama wanaume wengine kwamba labda hawapendi ndugu zangu. Ila uzoefu umenifunza kwamba ndugu hawabebeki, hawashibi, hawatosheki.....Kadri unavyojitesa ndivyo wanavyodai zaidi.
Dawa ni kutoa pale unapoweza na kuwahudumia wakiwa kwao!
kwani ni ndugu wote wanaohitaji msaada?? wangine yaweza kuwa ni matembezi tu! lkn km ni msaada bhac asaidiwe hukohuko aliko!! pia jambo hili mm nilihusisha na kipato kidogo, maana mtu anapoingiwa na roho ya uchoyo ndo bifu linapoanza!!Heri yangu mie nilepiga marufuku ndugu zangu kukaa kwa wanandoa. Tena hili ndio lilikuwa la kwanza kusisitiza kati ya yote. Ndugu asaidiwe huko aliko.
Asante sana,wewe sasa ni baba kamili,ukikuta mwanaume kaongea haya ujue amekomaa haswaa,nikupongeze kwa hilo.
Haswaa ni kutoa kadri unavyoweza,uchoyo wa nini?kikiwepo ni kutoa tu,kisipokuwepo ndugu aelewe tu hilo halipo na haliwezekaniki.
Kuishi na ndugu inahitaji moyo hua wanataka anachokufanyia mume nae awafanyie hivyo hivyo
Habari za jioni mabibi na mabwana katika jukwaa hili?
Naomba tujadili changamoto zitokanazo na kuishi na ndugu wa mume/mke, watoto wa kambo katika familia.
Hii imekuwa changamoto hasa kwa wanawake tushindwa kuishi na ndugu ama watoto wa mwanaume.
Kuna msemo huu "Ndugu hawana jema, hata uwabebe mgongoni" je msemo huu una ukweli?
Je tatizo ni nini?
Ni jinsi gani ya kukabiliana na changamoto hizo??
Nina mifano hai miwili ambayo wadada wameshindwa kuvumilia kuishi na ndugu. Wanalalamika ndugu wa mume wana masimango, hawaridhiki na chochote wanachofanyiwa...
Karibu kwa mjadala
Kuishi na ndugu ni ujima.
Naelewa kutembeleana kwa muda, lakini kuishi na ndugu dunia ya leo kunaongeza msuguano.
Mh, Mie mwenyewe nilikulia kwa kaka yangu na kusomeshwa na kaka yangu...
Kwa kweli nakosa hata la kusema maana shemeji yangu yaani mke wa kaka yangu yeye nadhani yuko kwenye nafasi nzuri kueleza kuhusu jambo hilo.
Lakini labda niseme tu kwamba kwa mila za Kiafrika kuishi na ndugu haikwepeki, hata kama umezaliwa peke yako.
Naamini wale wadau wa Leo Tupo Hapa Pub wanamjua MJEDA
CC: charminglady, Paloma, watu8, Asprin, Kaizer, Ruttashobolwa, Mentor, Madame B KakaKiiza, LiverpoolFC, Erickb52, Filipo, Jiwe Linaloishi, Kipaji Halisi
Mentor, iwapo MJEDA angesema atusaidie huko tulipo, labda hata hapa JF msingenijua.....Ukiweza..wasaidie huko walipo!
Kuna ndugu wanakera balaa.
Anakula vitu ovyo kwenye friji, viguu anaweka juu ya sofa, haflash choo wala nini.
Mh, Mie mwenyewe nilikulia kwa kaka yangu na kusomeshwa na kaka yangu...
Kwa kweli nakosa hata la kusema maana shemeji yangu yaani mke wa kaka yangu yeye nadhani yuko kwenye nafasi nzuri kueleza kuhusu jambo hilo.
Lakini labda niseme tu kwamba kwa mila za Kiafrika kuishi na ndugu haikwepeki, hata kama umezaliwa peke yako.
Naamini wale wadau wa Leo Tupo Hapa Pub wanamjua MJEDA
CC: charminglady, Paloma, watu8, Asprin, Kaizer, Ruttashobolwa, Mentor, Madame B KakaKiiza, LiverpoolFC, Erickb52, Filipo, Jiwe Linaloishi, Kipaji Halisi
Hiyo ni tabia mbaya inabidi ikemewe kwa nguvu zote.................
Mentor, iwapo MJEDA angesema atusaidie huko tulipo, labda hata hapa JF msingenijua.....
Kuna mambo mengine kuyajadili kijumla jumla hatuwezi kupata muafaka, mimi labda tu niseme kwamba sishabikii kuishi na ndugu hasa kwa mazingira ya sasa, lakini wengi wetu hapa tumelelewa na ndugu na kusomeshwa na ndugu, kwa hiyo wakati tunapinga hapa, lazima tukumbuke tulipotoka........
Mzee Mtambuzi pale ambapo utaanza kumkemea ndipo atakapoanza kusema ubaya wa mke.
Kuna wanaoenda mbali na kusema maneno ya uongo na uchonganishi.
Wanataka kila wafanyalo hata liwe baya lisikemewe.
Kuna ndugu wanakera balaa.
Anakula vitu ovyo kwenye friji, viguu anaweka juu ya sofa, haflash choo wala nini.