Wanandoa na extended family


Umenena vyema.Point ya msingi ukiishi na ndugu yeyote ukaona habebeki mrudishe kwao.Tafuta ambae kweli anaonesha anajua anachoitaji.
 
Heri yangu mie nilepiga marufuku ndugu zangu kukaa kwa wanandoa. Tena hili ndio lilikuwa la kwanza kusisitiza kati ya yote. Ndugu asaidiwe huko aliko.
 

Unafikiri walosema adui yako muombee njaa walikosea.
 

unapotoa msaada usiufanye deni wala usingoje shukrani!

Naomba mnisaidie kitu ndugu zangu,

Haya mnayoyasema ni kutokana na uzoefu au wishful thinkng plus sweet delirium?
 
Wanawake wamejaa na roho mbaya sana, mbona ndugu zao wakijazana kwa mume hawanung'uniki?...binafsi sioni tatizo kuishi na ndugu wa mke/mume as long as wanajibehave katika maadili yaliyo mema.
 

hahahaa, unikwaze nini ndugu yangu wewe una familia yako na misingi yako na mini nina familia yangu na misingi yangu, nilitakak uelewa tu kama unamaanisha kufuga kwa maana ya mtu anakaa tu hana aa wala bee au na mtoto wa dada yako unayemsomesha naye unamfuga? Tunatofautiana makuzi mkuu, wengine tumetoka familia duni sasa tukiwa wabinafsi tutakuwa hatutendi haki. Kama mtu hana kazi na amekuja kwangu obviously anataka nimtafutie kazi, nitamtafutia, kama hana vigezo mashamba yapo atakwenda kusaidia kazi huko na kuwa usefull!
 
Wanawake wamejaa na roho mbaya sana, mbona ndugu zao wakijazana kwa mume hawanung'uniki?...binafsi sioni tatizo kuishi na ndugu wa mke/mume as long as wanajibehave katika maadili yaliyo mema.

Picture this wewe ndio mama mwenye nyumba anakuja binamu yako kakorofishana na mume wake kwa sababu alisahau birthday yake. anakuja kukuomba wewe dada yake akae kwako, mimi ninakutimua saa hiyo hiyo hata kabla haujaketi. Ndugu wa aina hii awe wa mume au wa mke natimua tu. kuzoeana kunapunguza heshima.
 
Naomba mnisaidie kitu ndugu zangu,

Haya mnayoyasema ni kutokana na uzoefu au wishful thinkng plus sweet delirium?

kaka tunatofautiana makuzi, marehemu babu yangu mimi alikuwa mfugaji mkubwa sana, watoto wake wote hakukaa nao ni shuleni kutoka shule wakaajiriwa wakawa wa mjini, "wafugwa" na watu baki, wengine raiya wa kigeni ndiyo waliomsaidia kazi za shamba, shuguli za nyumbani, alipofariki mifugo na mashamba iligawanywa mpaka kwa hao "wafugwa" wakaanzisha maisha yao! usiwachukulie ndugu wenye shida kama wafugwa, binafsi nawachukulia kama watu wanaohitaji msaada tu na najitahidi kuwasaidia kwa faida yangu na yao pia!! again, tunatofautiana makuzi, aliyekulia familia bora ni ngumu kuelewa!
 
Na sijui kwanini wanawake tumejijengea picha ya kwamba ndugu wa mume wote ni mizigo. Kuna ambao hawana shida jamni ukiishi nao.Binafsi siwezi shindwa kuishi na ndugu yeyote.Labda yeye ashindwe kuishi na mimi au tushindwane tabia.

Mtu ambae nkiishi nae itabidi Mungu anioongezee hekima ya mara mbili nlonayo labda mama mkwe.
 

Naomba tuelewane walau kwenye hili dogo. Sina maana kwamba sina ndugu wenye shida na wala siwasaidii. Ni kikupa undani wa jinsi ninavyowasaidia utashangaa. Hata hivyo msimamo wangu ni kwamba ndugu hatakaa kwangu. Period!

Nina sababu nyingi na InshaAllah, nitaeleza baadaye!
 

Kweli kabisa ukimtanguliza Mungu hakuna jambo gumu,mimi kuna wakati nilikuwa naumia kwanini kila ninapowatendea hawa ndugu mema ndivyo ambavyo inakuwa shida,nikamwomba Mungu anipe njia ya kutatua hilo,nikaona njia ya kwanza ni kuacha mashindano,pili ni kutoa zaidi ya mwanzo,ikawa ndugu akija kwangu akiomba mkate mmoja mimi ntatoa miwili hata mitatu. Akija kwangu akakuta sijui nina mapazia gani mazuri akiomba namtolea na mengine,kataka sijui kitenge changu nitaenda kununua na vingine viwili nimpe. Na hii imesaidia sana kuondoa kelele za kuvutana vitu vidogovidogo visivyo na maana. Na hata wenyewe wamefika mahali wameshindwa wanaona labda mtu anichokoze kwenye hili ananikuta mie peace tu.
 
Hongera, you real deserve it ... mimi pia nimeoa, I thought bado nikukaribishe kupambanisha chemistry na bro wangu!Anyway, kila la kheri na maisha mema ...

Asante sana nawe pia uwe na maisha mema.
 

Pole sana ndugu yangu. Naamini hutoi na kujiumiza mwenyewe.

Kwa upande wangu, siwezi kumlaumu mke wangu kwa jinsi yoyote atakavyowatendea ndugu. Hata mimi nilikuwa na mawazo kama wanaume wengine kwamba labda hawapendi ndugu zangu. Ila uzoefu umenifunza kwamba ndugu hawabebeki, hawashibi, hawatosheki.....Kadri unavyojitesa ndivyo wanavyodai zaidi.

Dawa ni kutoa pale unapoweza na kuwahudumia wakiwa kwao!
 
Hakuna sababu ya ndugu kutoka kijijini kuhamia kwako, watu lazima wakubali maisha ni magumu kila sehemu mjini na vijijini na inatubidi kufanya kazi kwa bidii. Afadhali ukae na ndugu unamsomesha, sasa mtu mzima asie na aaa wala bee kazi kubadili station za TV hata mimi tutakosana. Kafanye kaziiii full stop
 
Nadhani hii husababishwa na kati ya moja ya au kwa pamoja sababu tatu kuu. 1)Malezi 2) maisha duni/changamoto za maisha 2)Tabia mbaya binafsi.

1)Malezi;
Msingi wa malezi yenye tabia mbaya ndiyo chanzo.Wapo waliolelewa kibinafsi ambao hujijali wao na ndugu zao tu kwamba wanastahili zaidi.Hawa huziendeleza tabia hizo za wivu, umbea, vijimaneno,kunung'unikia mambo madogo n.k hata pale achukuliwapo na familia ya ndugu yake huyo kwajili ya msaada tu.

2)Maisha duni/changamoto za maisha;
Hii hutokea pale familia iliyojikokota kwa shida kutoka kimaisha(kupeleka watoto shule n.k) na hatimaye mmoja wa wanafamilia akapata nafasi nzuri/akaweza kujimudu vizuri tu bila shida...basi wanafamilia/ukoo huwa na hisia kuwa chochote akipatacho ndugu yao huyo ni sharti kiwafae wana familia/ukoo kwanza kabla ya mke/au mume aliyeolewa wakati wa maisha yakiwa vizuri.Hapo vitimbi huanza.

3)Tabia mbaya binafsi.
Ukiachilia sababu mbili ziizotangulia,baadhi yetu tumeumbwa,au tumeendekeza kwa kujizoesha tabia za ubabe,ubwana au ubibi...hii ni kwa wanandoa binafsi ambayo pia hupandikiza kwa ndugu zake au hulka tu na mwelekeo wa jumuiya na marafiki.

Kukabiliana ni vyema familia ikaishi yenyewe na kutoa msaada kwa mbali tu...binadamu tuna mapungufu, heri mapungufu na kukosoana wakosoane wanandoa wenyewe.
 

Umenena vyema asante kwa mchango wako...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…