Wananchi na wasafiri wa Mbeya na ushabiki wa mwendokasi wa mabasi ya abiria

HARRISON ONE

Member
Jan 8, 2014
42
30
Kuna tabia ya ushabiki wa mwendokasi wa mabasi hasa yaendayo Mbeya ambayo naona siku hadi siku inazidi kukua. Sasa sijui ni ushamba au nini.

Kufukuzana huko mtakuja kufa kwa kwa ujinga. Mikoa mingi sasa ina kampuni kubwa za mabasi ya abiria lakini hawana ujinga huo kama wanaofanya mabasi ya Mbeya -Dar.
 
WaTz tumejaza pumba kichwani, siku ya siku hatutaki bendera ipepee nusu mlingoti kwa jambo la kipuuzi
 
Uzoefu wangu Mbeya.

Ni mabingwa wa kuchambua na kutabiri hatma ya watu.

Siku moja nimepanda ki-Coster toka Tukuyu mpaka Mbeya. Dereva na jamaa mmoja alikaa kushoto kwake. Walimchambua mtu na maisha yake toka tunaondoka Tukuyu mpaka tunafika Mbeya. Nilishangaa sana!
 
Mwendokasi ni biashara ya Mabus hata abiria wenyewe kama bus halikimbii Kwa Kasi hawapandi tena.

Abiria ndiyo chanzo cha mwendokasi Kwa barabara zote nchini
 
Ligi ya hayo mabasi haikuanza leo au jana! Ilishakuwepo tangu enzi hizo za akina Kiswele/mwanahapa, Comfort, Lupelo, Scandinavia, Lang'ata, nk. Tena gari zilikuwa zinatembea usiku kwa usiku! Yaani asubuhi hiyo barabara Dar Mbeya, unakutana na masemi trailler pekee! Tena yale ya pulling!

Hivyo kwa sasa ni muendelezo tu! Na hasa ukichukulia hiyo route ina wafanyabiashara wengi, ambao kimsingi kwao muda ni mali. Anyway, sishabikii mwendokasi! Ila pia si muumini wa kuona gari linapoteza muda mwingi barabara kwa sababu nyepesi nyepesi. Kufa kupo tu.
 
zui wa 3 huu sasa unamhusu sauli na new force (hasa sauli) japo mtoa mada hajasema openly. Srikali italaumiwa isipochukua hatua.
 
Ligi ya hayo mabasi haikuanza leo au jana! Ilishakuwepo tangu enzi hizo za akina Kiswele/mwanahapa, Comfort, Lupelo, Scandinavia, Lang'ata, nk. Tena gari zilikuwa zinatembea usiku kwa usiku! Yaani asubuhi hiyo barabara Dar Mbeya, unakutana na masemi trailler pekee! Tena yale ya pulling!..
uko sahihi Mbeya ligi ya mabasi ni long time enzi za kina matema beach safina luck star hekima ...
 
Kuna tabia ya ushabiki wa mwendokasi wa mabasi hasa yaendayo Mbeya ambayo naona siku hadi siku inazidi kukua. Sasa sijui ni ushamba au nini.

Kufukuzana huko mtakuja kufa kwa kwa ujinga. Mikoa mingi sasa ina kampuni kubwa za mabasi ya abiria lakini hawana ujinga huo kama wanaofanya mabasi ya Mbeya -Dar.
Sasa kama Kuna mikoa inapeleka gari chache DSM unazan ushindani wa gari unakuja wap af ajari ipo tu at gari ikitembea taratibu na Kama we ni muoga upandage gari Moshi
 
Ligi ya hayo mabasi haikuanza leo au jana! Ilishakuwepo tangu enzi hizo za akina Kiswele/mwanahapa, Comfort, Lupelo, Scandinavia, Lang'ata, nk. Tena gari zilikuwa zinatembea usiku kwa usiku! Yaani asubuhi hiyo barabara Dar Mbeya, unakutana na masemi trailler pekee! Tena yale ya pulling!

Hivyo kwa sasa ni muendelezo tu! Na hasa ukichukulia hiyo route ina wafanyabiashara wengi, ambao kimsingi kwao muda ni mali. Anyway, sishabikii mwendokasi! Ila pia si muumini wa kuona gari linapoteza muda mwingi barabara kwa sababu nyepesi nyepesi. Kufa kupo tu.
Kwa taarifa yako asilimia 80 ya madereva wa magari makubwa tukianzia mabasi mpaka maroli wanatea mikoa ya Mbeya songwe na Iringa na ndio vidume njia zote mpaka huko kwako na wao sera ni moja chapailale
 
Kuna tabia ya ushabiki wa mwendokasi wa mabasi hasa yaendayo Mbeya ambayo naona siku hadi siku inazidi kukua. Sasa sijui ni ushamba au nini.

Kufukuzana huko mtakuja kufa kwa kwa ujinga. Mikoa mingi sasa ina kampuni kubwa za mabasi ya abiria lakini hawana ujinga huo kama wanaofanya mabasi ya Mbeya -Dar.
Baada ya mabasi ya Moshi kupata ajari na kuua Kibaha na kuacha mtindo huo Mbeya wakashika mkwanja wa spidi, na wakati huo walikuwa na mabasi mazuri na barabara nzuri kuliko zote. Ukitoka Dar saa 12 asubuhi saa 9 mchana uko Kyela, shabash! Chombo hakifunguliwi madirisha mpaka kinafika, ukifungua dirisha mizigo ya ndani inaanguka.
 
Niliwahi kutoka njombe saa 06:00 nikafika dar saa 15 kasoro. BUDGET hiyo.
siku hiyi unafika saa 18 kwa muda huo wa kutoka.
 
Back
Top Bottom