Wananchi kutokuelewa mambo kwa haraka kunachelesha maendeleo Afrika

Noti bandia

JF-Expert Member
May 3, 2020
2,145
3,358
Naweza kusema licha ya changamoto nyingi za kiuongozi zilizopo nchi zetu za kiafrika lakini pia wananchi kutokuelewa mambo Kwa uharaka na kutekeleza kunafanya nchi zetu kuchelewa kupiga hatua za kimaendeleo. Nitatoa mifano kadhaa.

1. ujenzi wa vyoo Bora, hapa ni matrilioni ya pesa yametumika kumuelimisha wananchi umuhimu wa kuwa na vyoo Bora lakini mpaka Leo miaka zaidi ya 60 ya uhuru bado kaya zinakosa vyoo au kuwa na vyoo vya asili. Hasara yake ni kwamba wachache wameneemeka na project za kuelimisha na kufaidi maposho Kila mwaka. Hizi pesa zingeenda hata kwenye miundombinu tungepiga hatua.

2. Kulima kilimo Cha kufuata kanuni za kilimo. Hv inakuwaje mtu anashindwa hata kumuomba jirani yake imekuwaje yeye kavuna gunia ishirini za mahindi kwenye ekari moja na yeye kavuna gunia Tano kwenye ekari moja wakati wapo kwenye eneo linalofanana. Aisee nguvu wananchi wanazotumia Kulima na wanachovuna ni vitu viwili tofauti kabisa. Kama ni ishu ya mbolea za dukani ni gharama inamaana hata mbolea za wanyama nazo ni gharama.

Unajua watanzania tunavichwa vigumu Sana🤣🤣🤣 yaani ninayo majirani zangu nawaambia kabisa njooni mchukue mbolea ya wanyama for free mkapandie mazao coz kwangu ni nyingi , majibu nayopewa unaweza kuzimia. Ooh aridhi yetu inambolea ya kutosha ukiweka mbolea za wanyama inaaribu ardhi, sasa angalia mazao yanayoota unaweza kulia.

3. Kunawa mikono baada ya kutoka choo au kabla ya kula. Hv kweli Kwa miaka hii ni ya kufundishana umuhimu wa kunawa mikono baada ya kutoka choo au kabla ya kula? Unaweza kuhisi masiara lakini haya mambo yapo
Niseme tu kama basi hiki kizazi kimeshindikana Serikali iwekeze kwenye hiki kipya angalao lamda miaka ishirini ijayo tunaweza kuwa na watu waelewa angalao wanajua hata umuhimu wa choo
 
Back
Top Bottom