Hali ya vyoo kwenye shule anayosoma mtoto wako ikoje?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu kwema?

Katika mambo ambayo wazazi huzingatia kuuliza yakoje shuleni, vyoo huwa havimo na kama kuna wazazi wanauliza basi ni 1%.

Katika sehemu zinazoongoza kwa uchafu katika mazingira ya shuleni vyoo ni namba moja ikifuatiwa na canteen. Jamani kuna baadhiya shule vyoo ni vichafu na vinatia kinyaa, na kukiwa na uhaba wa maji nhali ndio mbaya zaidi.

Na hapa hapa si kwa shule binafsi wala serilikali wote ni wale wale tu, labda zile private wanazolipa pesa ndefu tunaweza kuwatoa kwenye orodha hii, ila hizi binafsi za kawaida nao vyoo huwa hovyo tu, japokuwa kwa serikali hali ni mbaya zaidi.

Hii inaweka mazingira magumu kwa wanafunzi kushiriki kakikamilifu shuleni, na mazingira yanakuwa magumu zaidi hasa kwa wanafunzi wa kike ambao wameanza kuingia kwenye siku zao, kuwa katika hali ile bila maji ni mateso.

Nikikumbuka choo cha shule ya msingi (ya serikali) niliyosoma hali ilikuwa mbaya, maji kutoka ni siku moja moja, muda mwingi mikojo na vinyesi vimetapakaa ovyo.

Sekondari ilikuwa binafsi lakini nako hali ilikuwa mbaya vile vile, kulikuwa na vyoo vya kukaa na vya shimo, vya kukaa vilikuwa vya kutumia kukiwa na maji na vya shimo wakati maji yanasumbua, muda mwingi ilikuwa vinatumika vyoo vya shimo maana maji ilikuwa changamoto (miaka mingi imepita shida ya maji bado iko pale pale😂🤣🤣). Na vikitumika vya shimo sio kwamba kuna maji, hakuna, mwendo wa kutoka kizungu na tishu, na hapo sasa mpaka hizo tishu ziwepo!

Unakuta mtoto ana U.T.I sugu na hujui imetoka wapi, chances are ameipata shuleni sababu mazingira ya vyoo kwa shule nyingi siyo ya kuridhisha.

Ni sehemu ambayo haitiliwi sana mkazo lakini inaweza kusababisha magonjwa mengi kwa mtoto wako, U.T.I ni mfano mmoja tu.

Ukweli ni kwamba, vyoo vingi shuleni, hasa vya serikali vina hali kama ya kwenye huo uzi nimeambatanisha hapo chini.

Unajua choo cha mtoto wako kinafanaje shuleni? Au ni jambo dogo halina haja kufatilia? Tuona na mazingira yalivyo kwa picha itakuwa vizuri.

Pia soma:

Songea: Shule ya Msingi Mshangano ina vyoo vichafu sana
 
Kazi ya mzazi wa kibongo ni kulipa ada, kulalamikia walimu wakiomba michango, kuwaponda hawafundishi mtoto akifeli la saba na form 4( maana hapo katikati hata hafatilii matokeo wala maendeleo yake).

Choo ni mbali mnoo wakati hata uniform tu ni muhula hadi muhula.
 
Kazi ya mzazi wa kibongo ni kulipa ada, kulalamikia walimu wakiomba michango, kuwaponda hawafundishi mtoto akifeli la saba na form 4( maana hapo katikati hata hafatilii matokeo wala maendeleo yake).

Choo ni mbali mnoo wakati hata uniform tu ni muhula hadi muhula.
Umesema kweli Mkuu, ni wazazi wachache pia wanaofatilia hata maendeleo ya masomo ya watoto wao. Ni changamoto
 
Nakumbuka miaka Ile secondary ukienda Chooni lazima uvue shati Kwanza
 
Back
Top Bottom