Ugonjwa wa Kipindupindu, Wananchi tusiilaumu Serikali

ngara23

JF-Expert Member
Aug 31, 2019
2,393
5,243
Ugonjwa wa kipindu pindu unazidi kuuwa watu wengi huku kanda ya ziwa

Ni aibu kwa zama hizi jamii kukumbwa na ugonjwa wa uchafu kama kipindupindu.

Watu wanashindwa kuzingatia usafi wa mikono na chakula

Ukifika mikoa kama Mwanza na Dar es Salaam utashangaa uuzaji wa ovyo ovyo wa vyakula, mama mantilie hawaoshi vyombo kwa usahihi na kwa maji moto, kuna inzi kila sehemu

Watu wanakula mandazi na vitumbua vilivyomwagwa ovyo na nzi wameyazingira sokoni

Hali ya vyoo na maji ya kunywa ni mbaya.

Wananchi wameamua uchafu kuwa sehemu yao

Serikali ikiwafukuza mama ntilie wasiozingatia afya za wateja, watu wataanza kulalama

Hivi serikali ije ikukumbushe kunawa mikono, kutawaza, kula chakula kisafi kweli

Hii jamii inayoteswa na Kipindupindu itaweza kweli kuwaza mambo ya viwanda, biashara, technology

Serikali inatoa elimu bure watu wanasoma bado jamii inakumbwa na Kipindupindu

Tichukue hatua sote, tudhibiti hili gonjwa la ovyo na la aibu kwa zama hizi la Kipindupindu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dodoma ni HQ ya nzi duniani I suspect! Kuna haja ya kubadili Katiba ili kuweka vifungu mahususi vya kupambana na hawa wadudu wachafu! Nzi wa Dodoma sio poa maeneo ya vyakula uswahilini.
 
Ugonjwa wa kipindu pindu unazidi kuuwa watu wengi huku kanda ya ziwa

Ni aibu kwa zama hizi jamii kukumbwa na ugonjwa wa uchafu kama kipindupindu.

Watu wanashindwa kuzingatia usafi wa mikono na chakula

Ukifika mikoa kama Mwanza na Dar es Salaam utashangaa uuzaji wa ovyo ovyo wa vyakula, mama mantilie hawaoshi vyombo kwa usahihi na kwa maji moto, kuna inzi kila sehemu

Watu wanakula mandazi na vitumbua vilivyomwagwa ovyo na nzi wameyazingira sokoni

Hali ya vyoo na maji ya kunywa ni mbaya.

Wananchi wameamua uchafu kuwa sehemu yao

Serikali ikiwafukuza mama ntilie wasiozingatia afya za wateja, watu wataanza kulalama

Hivi serikali ije ikukumbushe kunawa mikono, kutawaza, kula chakula kisafi kweli

Hii jamii inayoteswa na Kipindupindu itaweza kweli kuwaza mambo ya viwanda, biashara, technology

Serikali inatoa elimu bure watu wanasoma bado jamii inakumbwa na Kipindupindu

Tichukue hatua sote, tudhibiti hili gonjwa la ovyo na la aibu kwa zama hizi la Kipindupindu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kinyesi kinacho--bubujika Kariakoo na Posta Dar es salaam ni wanyonge ndio wanapaswa wazibue mifereji?
Nyumba ambazo hazina vyoo watu wanakunya kwenye mifuko na kutupa majalalani ni nani anapaswa kuwafungia? Mbona maandmano ya katiba serikali inakuja juu na ina bajeti ya kuzuia demokrasia?
Mama lishe wanao uza chakula posta na kariakoo vichochoroni sehemu zisizo rasmi na hakuna hata kunawa mikono, wauza karanga wanapoenda chooni wana acha wapi makapu yao?
Wauza karanga wanatawaza na maji au tissue na je wanapopima mnajua mikono yao? sisi tuwakimbize hao wauzaji ama serikali ndio itoe miongozo na wananchi waache kula kula ovyo kama mbuzi?
 
Sujawahi ona baa hapa Dar wameeeka mabomba ya maji watu wanawe zaidi ya vindoo.Inaonyeshs ma bwana afya hawanaufahamu kudu kunawa kabla ya Kila. Kila bar iwekwe mabomba.
 
Niko mwanza takribani ni mwezi Sasa lakini hapa nilipo maeneo ya nyegezi maji ni shida sana yanatoka bombani kwa mgao inalazimika wakati mwingine ununue yanayotembezwa, huo usafi bila maji utaufanya vipi kwa usanifu, bado eti tusilaum
 
Back
Top Bottom