Habarini wanajamvi!
Nimekuwa nikifuatilia mikutano ya Magufuli, kuna kitu kimoja kiko dhahiri. Wanao mshangilia kuna wakati wanaonesha mashaka nadhani wanapo kumbuka ugumu Wa maisha mtaani. Washangiliji Wa kweli Ni rahisi kuwatambua! Hawa Wa Magufuli wanafanana sana na walio kuwa wanamshangilia IDD Amini.unafiki mtupu.Wanachama na viongozi ndani ya chama chao hawana amani ya moyo! Ku a kitu wanatafakari.
It is very true.
Unapokuwa na Mkuu wa nchi wa aina ya JPM, hakuna mtu ambaye ndani ya moyo wake anaweza kuwa na amani kwa asilimia 100.
Kwa kuwa Mkuu ameamua kuiendesha hii nchi kwa staili ya ONE MAN SHOW, na bila kuzingatia Katiba ya nchi inamuelekeza vipi na kwa staili ya kutoa matamko ya majukwaani........
Kwa hiyo hakuna anayeweza kutabiri kuwa kesho Mheshimiwa ataibuka na tamko gani......
Tumeshuhudia matamko mengi sana yenye utata mkubwa.
Nitatoa mfano wa matamko hayo yenye ukakasi mkubwa.
1. Ni mimi pekee ambaye ninapaswa kuzunguka nchi nzima na kuwaeleza watanzania ambacho Serikali yangu inachotegemea kuwafanyia watanzania, wanasiasa wengine wa vyama vya upinzani nawapa likizo hadi mwaka 2020.......
2. Nasikia kuna watu wanasema bandari yetu ya Dar haina tena meli zinazoleta mizigo TZ, niwaambie waTz kuwa tunataka meli zinazolipa kodi, hao waliokimbiza meli zao ni wale waliokuwa hawalipi kodi, waache waende kwenye hizo bandari za nchi nyingine wanakoruhusu ukwepaji kodi.......
3. Nasikia watalii wanatishia kutokuja nchini kutokana na Serikali yangu kuintroduce VAT kwa watalii, nami nasema hao watalii na waende zao, mimi nataka watalii wenye pesa zao wenye uwezo wa kulipa kodi........
4. Watumishi wote wa Umma wahamie Dodoma haraka iwezekanavyo, wakiendelea kubaki Dar wajue kuwa nyumba zote za serikali zilizoko Dar nitaziuza na zigeuzwe kuwa Hoteli, kwa hiyo hao watumishi watakaobaki Dar watakuwa wamejifukuzisha kazi na itabidi watafute nyumba zao za kuishi......
5. Nitawashusha wale waliokuwa wanaishi kama Malaika na hivi sasa waishi kama mashetani.......
Hakika TZ hivi sasa tunapita katika kipindi kigumu sana ambacho huwezi kutabiri Mkuu wa nchi ataibuka na tamko gani kesho..........
Hivi sasa nakumbuka maneno ya busara aliyowahi kutamka baba wa Taifa katika moja ya hotuba zake miaka ile ya 90 kuwa watanzania ni lazima tuchague Rais ambaye ataiheshimu na kuitii Katiba ya nchi yetu, kama tutapata Rais ambaye hatataka kuitii na kuiheshimu Katiba yetu ya nchi, Mwalimu aliongea kwa msisitizo mkubwa kuwa Rais wa aina hiyo HATUFAI.............