barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
*MHESHIMIWA RAIS UGOMVI WAKO NA SERIKALI ZA MITAA HAUJAISHA?*
Yamkini wengi hawafahamu historia hii ya mapambano kati ya Mheshimiwa JOHN POMBE MAGUFULI na SERIKALI ZA MITAA TANZANIA (HALMASHAURI) leo nitapata kuwajuza japo kidogo na nyinyi mfahamu sababu nyingi za leo Serikali za Mitaa kuumia na Maamuzi ya Serikali.
Yapata Miaka Takribani mitano iliyopita palikuwa na pata shika nguo kuchanika kati ya Waziri Wa ujenzi na miundombinu Mh.John pombe Magufuli na Serikali za mitaa.
Ilikuwa tarehe 21 ya mwezi Februari 2011 ambapo akiwa kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es salaam, mbele ya mwenye kiti wa kamati ya bunge ya miundombinu wakati huo Mh.Peter Serukamba, Mheshimiwa Rais alitoa taarifa ya kuondoa mabango ya Matangazo, mali za Serikali za mitaa nchi nzima, eti kwa kuwa halmashauri zilikuwa zinakusanya kodi kwenye maeneo yasiyo yake bali yalikuwa maeneo ya Tanroads ambayo Mheshimiwa Rais alikuwa akiya simamia.
Kama kawaida yake alipokuwa waziri mara nyingi alipokuwa akiongea hoja za namna hiyo alikuwa akitaja na sheria inayompa jeuri ya maamuzi yake, wakati huo akitaja sheria namba 3 ya mwaka 2007.
Basi kesho yake tarehe 22 february Mheshimiwa Waziri John Pombe Magufuli akaagiza Mameneja wote wa Tanroads mkoa, waanze mara moja operesheni ya kuondoa mabango nchi nzima yaliyo barabarani,
Huku kwa agizo hilo Halmashauri za Dar es salaam pekeyake zilikuwa zinaenda kupoteza kiasi cha shillingi billioni 5, hivyo kwa mikoa yote nchi nzima halmashauri zingepoteza kiasi Tsh Billioni 45.
Hapo ndipo Tulipoamua na sisi kama serikali za mitaa kuacha unyonge baada tu ya Mameneja wa Tanroads kuanza kuweka alama za "x" kwenye mabango tulipaza sauti zetu kuamshana madiwani wote nchi nzima na kuanza kufikisha kilio chetu kwa njia za vyombo vya habari, mpaka tulipo sikika kwamba ulikuwa ni uamuzi wa ovyo na mbaya kupoteza mapato halali ya halmashauri kwa ugomvi usio na tija.
MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:: Magufuli apigilia msumali mabango barabarani
Namkumbuka marehemu Didas Masaburi kwa Dar es salaam ndiye aliyeitisha kikao cha Madiwani na Mameya mpaka kwemda kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na baadae Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kutuambia *"hilo limekwisha nimewaelewa nendeni, mabango hayato ondolewa tena"*, kwa wakati ule tulimshinda Rais John Pombe Magufuli Ila sasa ni nini kinaendelea baada ya yeye kuwa Rais wa Jmuhuri wa Muungano wa Tanzania? Ugomvi umekwisha? kwa maana yeye sasa ni Rais wa nchi au Ndiyo ameamua Kulipiza visasi kwetu serikali za mitaa?
*Ona sasa haya yafuaatayo;*
1. Alipochaguliwa akaamua yeye mwenyewe kuwa ndiye waziri wa TAMISEMI yaani serikali za mitaa ziwe chini yake, je aliamua kwa moyo mkunjufu kuwa mlezi wetu? URAFIKI WA MASHAKA.
2. Alipokuwa tu Waziri wa TAMISEMI kwa maana Tamisemi kuwa chini ya OFISI YA RAIS akabadilisha Wakurugenzi wote wale waliokuwa wanajulikana kwa kuchapa kazi akateua makada wa chama chake ili KUJIPANGA KISAWASAWA
3. Haikupita muda wakapitisha uamuzi wakiondoa kodi za majengo "property tax" zilizokuwa zinakusanywa na serikali za mitaa miaka yote na angalau kusaidia halmashauri nyingi kujiendesha zenyewe wakazirudisha TRA huku wakijua hawana timu ya watu wa ukusanyaji kufikia kila mtaa na kila nyumba kama serikali za mitaa.
4. Ulikuwa uamuzi wa Halmashauri zote kuungana kuagizwa kuondoa posho za madiwani huku serikali ikijua fika Madiwani hawalipwi mshahara na hawana tena fedha za kuendeshea shughuli zao za kazi, HOJA YA KUWASHIKISHA ADABU MADIWANI
5. Ukiondoa ubaguzi wa halmashauri zinazo ongozwa na wapinzani na wale wa chama chake, miradi yote ya wapinzani iliyohitaji "RUHUSA" Kutoka seriklali kuu chini ya wizara yake ya TAMISEMI hakuna halmashauri ya upinzani iliyopata ruhusa kuleta mradi mkubwa wa maendeleo kwa kisingizio tutapewa sifa
mfano....
a) Stendi ya mabasi Moshi (CHADEMA)
mpaka leo danadana huku ya Msavu Morogoro ilipewa kibali haraka.
b) Dampo la takataka Kinondoni Chinibya (CHADEMA) Nasikia leo ya kuwa Meya wa kichina (CCM) Wanataka kumsaidia ruhusa ipatikane.
6. NI HILI LA KUPOKONYA MIHURI YA WENYEVITI SERIKALI ZA MITAA. Mimi sijawahi kuona Duniani mtu anapewa ofisi anatakiwa kusaini fomu, muhuri wake anashikiwa na mtu mwingine kazi yake iwe kuweka saini tu juu ya eneo analohitajika kufanya hivyo.
Katibu Mkuu TAMISEMI ameshashusha maagizo ya kupokonya mihuri wenyeviti serikali za mitaa; Je ni muendelezo wa kuziuwa serikali za mitaa?
Wenyeviti wa serikali za mitaa wapo kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 145 lna 146 zote zinataja uwepo wa serikali za mitaa na wajibu wake
pamoja sheria zilizotungwa kama ufafanuzi wa jumla katika sheria za serikali za mitaa sura 287 na ya 288 toleo la 2002 awali sheria za serikali za mitaa namba 7 na 8 za mwaka 1982
katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza kuwa serikaki za mitaa zitakuwa na majukumu yafuatayo;
(a) Kutekeleza majukumu ya serikali za mitaa katika maeneo yao.
(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na usalama wa wananchi katika maneo yao.
(c) Kuimarisha Demokrasia katika maeneo yao na kuhakikisha wanaitumia kuleta maendeleo ya watu wao.
Je kuingilia na kuvuruga serikali za mitaa kunakofanywa na awamu ya tano siyo kuisigina katiba?
SHERIA ZIMEWEKA WAZI MAJUKUMU YA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA
(a) Kuwa mwenyekiti wa mikutano ya kamati za mtaa na mikutano ya mtaa.
(b) Kusuluhisha migogoro midogomidogo ambayo haistahili kuitwa kwenye kamati ya mtaa, au kupelekwa kwenye baraza la usuluhishi la kata au mahakama.
(c) Kuwa msemaji wa mtaa.
(d) Kuongoza na kuwahamasisha wananchi wake washiriki katika shughuli za maendeleo, sherehe za kitaifa, mikutano ya hadhara itakayoitishwa na mtaa, halmashauri au jiji na serikali.
(e) Kuwakilisha mtaa kwenye kamati ya maendeleo ya kata.
(f) Kutekeleza kazi atakayopewa na kamati ya maendeleo ya kata.
(g) Kutekeleza kazi atakazopewa na kamati za mtaa au mkutano mkuu wa mtaa.
(g) Kusimamia kazi zote za kamati za mtaa.
(f) Kutunza rejista za wakazi wa mtaa wake.
Swali; Je Wenyeviti wa Serikali za Mitaa watafanyeje Majukumu yote haya bila mihuri, hiyo mikutano na vikao ni nani atasaini mihutsari yao? je aliye agiza wapokonywe mihuri ameliona hili?
Je wenyeviti hawa si ndiyo mnaowatumia wakati wa uchaguzi watangaze zoezi la kujiandikisha ?
Je wenyeviti hawa si ndiyo mnao watumia Kuitisha wananchi kama viongozi wa serikali wanakuja maeneo yao?
Je wenyeviti hawa wa serikali za mitaa si ndiyo mnao walipa malipo "kiduchu ya posho zao" shillingi 50,000 elfu kwa mwezi?
Je wenyeviti wa serikali za mitaa si ndiyo wanaotegemewa kuhimiza wananchi walipe kodi na ushuru wa halmashauri mbona mnawachokoza bila sababu?
je wenyeviti hawa si ndiyo wanao tia mihuri yao kwenye fomu za utambulisho kwenda benki, taasisi za serikali na hata kwenye barua za dhamana polisi? nani atasaini kwa niaba yao?
Je watendaji wa mitaa "mamluki" kwakuwa karibu wote sio wakazi wa mitaa wanayofanyia kazi, kama watendaji watawatambuaje watu wa mtaa, kwenye dhamana?
Je wenyeviti wa serikali za mitaa si ndiyo mnawaita walinzi wa amani kwenye mitaa,huku mnachukua mamlaka zao?
Je awamu ya tano ya serikali hii haiwaitaji wenye viti wa mitaa katika shughuli zao za kuleta maendeleo?
Je hakuma njia nyingine ya kutatua tatizo kama lipo au changa motto mpaka serikali ifikie hatua ya kuwapokonya mihuri yao?
WENYEVITI SEEIKALI ZA MITAA WAKIMBILIE WAPI NA RAIS NDIYE WAZIRI NA MKUU WA TAMISEMI?
JE MSHEMIWA RAIS UGOMVI WAKO NA SERIKALI ZA MITAA BADO UNAENDLEA?
Imetolewa na
Senior Councillor ubungo
Mstahiki Meya
Manispaa ya Ubungo
Boniface Jacob.
Katibu Mkuu Tamisemi ametoa maagizo kwa Makatibu Tawala Mikoa Tanzania Bara kuwanyang'anya mihuri wenyeviti wote wa mitaa na kuwapoka madaraka yao kupitia waraka wenye kumbukumbu CCB.126/215/01 wa tarehe 30/11/2016 (Utawekwa jamvini)
Pamoja na sababu nyingi alizotoa kupitia waraka huo amesema kuwa nanukuu ........kwa mantiki hiyo Wenyeviti kuendelea kuwa na mihuri bila ya kuwa na MAMLAKA ni ukiukwaji wa Sheria. Kazi ya Mwenyekiti ni kuongoza vikao vya maamuzi.....
Katika barua hiyo Katibu Mkuu amewatuhumu kuwa ....Imebainika kuwa baadhi ya Wenyeviti wamekuwa wakitumia mihuri hiyo kama chanzo chao binafsi cha mapato kwa kudai malipo kwa maelezo kwamba wao hawapati posho. Hoja hii haiwezi kuhalalisha wao kuwa na mihuri......
Katibu Mkuu ametoa maelekezo kuwa kazi zote zilizokuwa zinafanywa na Wenyeviti zifanywe na Maafisa Watendaji wa Mitaa/ Vijiji/ Vitongoji...
Kwa hatua hiyo ya TAMISEMI imepelekea kuondoa kwa Wenyeviti
Wenyeviti kupitia Viongozi wao wamepanga kutoa msimamo wao kuhusiana na jambo hili ambapo wengi wanasema kuwa wananchi ndiyo watakaopata shida kubwa kutokana na kukosekana huduma stahiki ya ofisi za mitaa nyingi kukosa watendaji na kutohudumiwa baada ya saa tisa alasiri...
- Mamlaka ya kuwatambua wakazi wa mtaa ambao wanahitaji kuthibitishwa na mamlaka mbalimbali kama ni wakazi halali. hii ni kwa sababu hakuna mtendaji wa Mtaa ambaye ni 'native' wa eneo husika kwani watendaji wengi huishi mbali na ofisi zao
- majukumu ya kuwa mkuu wa ulinzi na uslama wa mtaa
- kuthibitisha mihtasari ya vikao mbalimbali vya mtaa hivyo kupelekea uwezekano wa watendaji kupika mihtasari hasa inayotoa ripoti ya miradi ya maendeleo
- kutatua migogoro midogo kama inavyoainishwa kwenye Sheria kwani maamuzi yote hayatakuwa na uthibitisho wa mhuri...
NB:
Jana tarehe 09/01/2017 nimekuwa mhanga wa kwanza mtaani kukosa huduma ya mwenyekiti kutokana na kwamba ofisi haina mtendaji na anayekaimu yupo likizo, kutoka ofisi ya mtaa hadi ofisi ya Kata ni kilometa 11....
Urasimu unabisha hodi Tanzania