Wanamibia wang'aka baada ya watoto wanne wa Rais kujumuishwa kwenye ujumbe wa Serikali kwenye mkutano wa hali ya hewa COP28

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Baadhi ya WaNamibia wamekasirishwa baada ya kujua kwamba watoto wanne wa Rais Hage Geingob walijiunga na ujumbe wa serikali kwenye mkutano wa hali ya hewa wa COP28.

Walikuwa miongoni mwa watu sita kutoka familia ya rais iliyoorodheshwa kama sehemu ya ujumbe wa Namibia huko Dubai.

Ofisi ya Rais Geingob ilithibitisha siku ya Jumatatu kwamba watoto wake walifika katika jiji hilo, lakini ilikana madai ya kwamba safari yao ilifadhiliwa na serikali, pia ofisi hiyo haikusema wanafamilia wengine gharama zao zililipwa na nani.

"Rais Geingob na Bibi Geingos(Mkewe) walilipia ndege na gharama za malazi za watoto wao," Rais wa Namibia alipost X siku ya Jumatatu.

"Wanamibia na vyombo vya habari vinapaswa kuondoa mashaka kwamba hakuna hata senti moja ya fedha za umma zimetumika kwa watoto wa Rais."

Rais aliongeza kwamba madai hayo yalikuwa "yenye na yamechochewa kisiasa" na yanalenga kuvuruga "kazi nzuri" ya Rais Geingob na ujumbe wa Namibia huko COP28.

Lakini baadhi ya WaNamibia wamepuuzia mbali jibu la rais kama lisilotosheleza, wakisema haliwezi kuthibitisha kwamba safari ya watoto wa Rais Geingob na wanafamilia wake ilifadhiliwa kwa kibinafsi.

Baadhi ya wakosoaji pia wameitaka ofisi ya rais kueleza jukumu la wanafamilia wake kwenye Mkutano wa COP28 na kwa nini waliorodheshwa kwenye ujumbe wa serikali ikiwa safari yao ililipwa kibinafsi.

"Mnaamini sisi ni wapumbavu? Kwanini wangeweza kuorodheshwa kwenye orodha ya wajumbe kama hawako sehemu yake? Kuna umuhimu gani wa kuwepo kwao Dubai pamoja na wajumbe wa serikali?" mmoja wa WaNamibia alijibu X.

"Tunatarajia ripoti kamili itakayowasilishwa [bungeni]," alisema Mbunge wa Namibia Inna Hengari.

Awali, alikuwa ameikosoa serikali kwa kuripotiwa kufadhili safari ya familia ya rais, huku wakidai hawana fedha za kufanikisha safari ya mbunge na afisa wa bunge kwenda COP28.

Ghadhabu hiyo inaonyesha upinzani mkubwa dhidi ya serikali za Kiafrika kwa kutuma ujumbe mkubwa kwenye COP28, ambao baadhi ya wananchi wanasema unadhihirisha ubadhirifu wa fedha.

Baadhi ya serikali, ikiwemo Nigeria, Tanzania, na Kenya, zimejitetea kwa kusema kuwa wajumbe wengi hawalipwi na serikali kwa kuwa wanawakilisha vyombo vya habari, asasi za kiraia, na taasisi binafsi.

Chanzo: Anger in Namibia over Dubai COP28 trip by president's children
 
ngozi nyeusi tunamatatizo kweli !!!maana huku Tanzania Samia amekwenda na umoja wa wanawake wa ccm
 
Wakati Marais wengine wa Afrika wakishutukiwa Kwa kwenda na lundo la wajumbe huko Dubai kwenye Mkutano wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa COP 28,huko Namibia Rais Hage Geingbob ameshutumiwa Kwa kubeba Watoto wake kuwa sehemu ya ujumbe wa Serikali.

Wananchi wamekasirika wakitaka maelezo inakuaje Watoto wa Rais waambatane kwenye ujumbe wa Nchi huku Serikali ikisema wanafamilia hao wa Rais walijigharamia wenyewe.

View: https://twitter.com/BBCAfrica/status/1731980788197925092?t=UU-3fbe9FWe-W4NAAIzgFQ&s=19

My Take
Ogooa sana Nguvu ya Mwanamke,hapa lazima first lady alilazimisha mambo kama huko Nchi jirani First lady anavyompelekesha yule Rais Nabii. 🤣🤣🤣🤣
 
This is Africa!
 
Rais Nabii kaoa Uchaggani? 😀😀
 
Mikutano hii ni balaa, nimegogle sehemu nikaona pesa ya kigeni iliyotumika na president Mwinyi na ujumbe wake kwenye mkutano kama huu pale Brazil 🇧🇷, Ile pesa kwa wakati ule ungejenga lines nne za barabara ya lami,kutoka chalinze hadi Dar, kwa thamani ya wakati ule, wapi gazeti na waandishi wa gazeti la motomoto wangethibitisha hili
 
Back
Top Bottom