Rais wa Guinea Bissau avunja Bunge bila kutangaza tarehe ya kufanyika Uchaguzi mpya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Rais wa Guinea-Bissau siku ya Jumatatu alivunja bunge kabla ya uchaguzi mpya kufanyika akisema "jaribio la mapinduzi" limelingiza taifa hilo la Afrika Magharibi katika mgogoro mpya.

Rais Umaro Sissoco Embalo, alitoa amri ya kulivunja bunge lenye idadi kubwa ya wapinzani na kutangaza kuwa tarehe ya uchaguzi wa wabunge "itawekwa kwa wakati muafaka, kulingana na katiba".

Ghasia zilizuka kati ya walinzi wa taifa na kikosi maalum cha walinzi wa rais usiku wa Alhamisi katika mji mkuu Bissau, na kusababisha vifo vya watu wawili.

Rais Embalo, ambaye alikuwa Dubai akihudhuria mkutano wa hali ya hewa wa COP28, alirejea Bissau siku ya Jumamosi na kutangaza kuwa "jaribio la mapinduzi" lilikuwa limemzuia kurejea mapema.

Siku ya Jumatatu, alisema kumekuwa na "hujuma" kati ya walinzi wa taifa na "baadhi ya wanasiasa waliomo ndani ya vyombo vya Serikali".

Akimaanisha "utendaji wa kawaida wa taasisi za serikali umekuwa mgumu".

"Ukweli huu unathibitisha uwepo wa mgogoro mkubwa wa kisiasa," aliongeza.

Walinzi wa taifa walikivamia kituo cha polisi siku ya Alhamisi jioni na kumchukua Waziri wa Fedha Souleiman Seidi na Katibu wa Hazina Antonio Monteiro, ambao walikuwa wakishikiliwa kwa mahojiano, kulingana na maafisa wa jeshi na wa kijasusi.


DW Swahili
 
Katika safisha safisha inayoendelea Rais wa Guinea Bissau amevunja Bunge na kutangaza Hali ya hatari Ili kukabiliana na jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa wiki Iliyopita wakati Rais huyo akiwa Dubai kwenye Mkutano wa COP 28.

View: https://twitter.com/BBCAfrica/status/1731720846484422799?t=i8S-Vr4O3yoZA9T2pwmmZw&s=19

My Take
West Afrika Bado hakujatulia ikisingatiwa kwamba Sierra Leone nako mapigano yalizuka ambayo yalitokana na jaribio la kuoindua Serikali.
 
Duuuh! yawezekana pande za huko,wanajeshi wanasahaulika na wanasiasa,hivyo kufanya mipango kila mara ya kuzipindua tawala zilizopo.
 
Back
Top Bottom