wanaJF niliokutana nao.....wamenisababishia balaa

wanaJF niliokutana nao.....wamenisababishia balaa

Poa Cheusi,

Bibi ni nusu ya babu na ndyo maana tunashikiriana kuwalea wajukuu vizuri!!

Mambo yenu ya kufichana fichana ndiyo yatawafanya msababishe wenzenu wakimbizwe ICU au waende jumla!!

Kwani unadhani akija akasoma ukumbini kwako atakuta nini??

Babu DC!!

kwa kweli babu labda hivyo vituko vyangu unavyovisema maana huko pm sina la ajabu nifanyalo hata pm mara nyingi kama siielewi elewi wala sijibu,
halafu mwambie bib nina mazungumzo naye karibia nitahitaji mazungumzo kati ya bibi na mjukuu,kuna mafunzo fulan nahitaji toka kwa bibi
 
Kwani nimeshindwa nini kusema toka mwanzo??

Au unataka niseme kile unachotaka wewe??

Anyway.....Cheusi anamjua aliyezimia zaidi ya mtu yeyote!.... Ila naamini siyo wewe!!

Anyway! Hata mimi naamini pia wewe hujui nilichotaka kukisema (kama kipo). Ila nimekubali yaishe. Kwangu mimi sikuwa na shida na ngumi au mateke maana vyote hivyo sivihimili ati!
 
Hongera sana Cheusi,

Mwombe tu Mungu yasikukute...Ila yakikukuta hata kama ni PM ya kulazimishwa lazima neema ikushukie hata kama itatoka kwa shetani ili ukikwepe kitanzi!!

Best wishes,

Babu DC

thanx.ila babu siwezi kuachika kwa ajili ya pm,maana nikiachika kwa pm nitkua mwanamke mjinga kuliko wote.Haiwezekani.
 
Anyway! Hata mimi naamini pia wewe hujui nilichotaka kukisema (kama kipo). Ila nimekubali yaishe. Kwangu mimi sikuwa na shida na ngumi au mateke maana vyote hivyo sivihimili ati!

Powa kaka,

Sasa wewe ulitaka kusemaje??

Babu DC!!
 
Hivi CheusiMangala ~ Mtambuzi?
Mim na shemeji yeni tulienda mahala kupata dinner,wkt tunasubiri tuletewe chakula tukiwa tumekaa kwenye viti shemeji yenu akaniaga kuwa anakwenda kujisaidia,alipoondoka nikatoa laptop yangu nikaanza kusurf JF nikiwa nimesign in.

Meza yetu ilikua karibu na mlango wa kuingilia ktk hotel hiyo na mim nilikua nimeupa mgongo mlango huo,kwa maana hiyo mtu anayeingia aliweza kuona kilichopo ktk screen ya laptop yangu.Mwanzon nilikua naficha screen ili mtu sione ninachofanya ila baada ya kuingia JF na kuanza kusoma moja ya thread nilijisahau kabisa kuficha screen.

Haukupita muda nikashangaa wakaka watatu nisiowafahamu wakija mbele yangu wakiwa na mshawasha wa ajabu.Nikiwa bado najiuliza hawa ni wa kina nani mbona kama wananifahamu mmoja wao akasema"Cheusimangala habari yako mkuu".Nikatamani kubisha kuwa mm sio Cheusimangala maana huwa sipendi kabisa urain wajue kuwa Cheusimangala wa JF ndio mim kwani huko uraian wana image tofauti kabisa na hii ya cheusimangala.Nikiwa sijui niwajibu nin mwingine akasema"Yaani cheusie daah kweli hizi avatar zinatudanganya sana maana nilikua na picha nyingine kabisa juu yako tofauti na unavyoonekana."

Nikiwa bado nafikiria jinsi ya kukana kuwa mim sio cheusimangala mara nikamuona shemeji yenu anarudi kutoka maliwatoni alipokua huku akiwatizama vijana wale watatu kwa sura yenye kujiuliza ni wa kina nani.Alipofika karibu ikabidi niwaambie vijana wale" huyu ndiye shemeji yenu" nikitumai kwamba wataondoka na kuniachia nafasi ya kujua nitamweleza nini juu ya watu wale ambao hajawahi kuwaona.

Baada ya utambulisho ule mmoja akasema "ooh bwana shemeji nice to meet you" kisha akaendelea" yaani jamii forums ni pana sana unaweza kukutana na members wenzio katika mazingira usiyotegemea kabisa"
Kisha shemeji yenu kwa mshangao akaniuliza"ina maana mpenzi unaifahamu jamii forums?kabla sijamjibu akauliza swali jengine"wewe ni member au unapita kusoma soma tu kwa nje?Nikiwa na mim nashangaa kuwa kumbe na yeye anaijua jamii forums akaniuliza swali jengine"unatumia username gani huko jamii forums"swali hilo lilinizidishia hofu kwani katika vitu nilivyokua sitaki ajue ni kuwa mim ni cheusimangala wa jamii forums lakini nikiwa bado nafikiria haraka haraka nini cha kumdanganya nikasikia mmoja wa wakaka wale akikohoa kidogo huku wote watatu wakionekana kujisikia vibaya kutokana na shemeji yenu kuonekana kupaniki kwa kugundua kuwa naijua jamii forums akasema" cheusie acha sisi tukuage bana nice to see you".Roho yangu ilidunda sana baada ya yule kaka kuniita kwa jina la cheusimangala.

"Ina maana mpenzi wewe ndiye cheusie!...cheusimangala...!this can not be true!no no no"This is a night mmmm...."shemeji yenu hakumaliza alichotaka kusema kwani alidondoka chini na kupoteza fahamu huku michuzi iliyomwagika kutoka mikononi mwa muhudumu aliyekua karibu yake tayari kwa kutuwekea chakula mezani ikiwa imechafua shati lake zuri la blue alipendalo kuliko yote na bila kuchelewa niliwaona wale vijana watatu wakitoka mbio bila hata kutoa msaada kwa mwenzao Huku nikiwasikia wakiambiana"hii tukairushe wapi wakuu habari mchanganyiko au chit chat?"Nikiwa najiandaa kupiga yowe la kuomba msaada alarm yangu ikanishitua kutoka usingizini.

Unafikiri ni kwa nini ktk ile ndoto shemeji yenu alizimia baada ya kugundua kuwa mim mpenzi wake ndiye cheusimangala?Je mim ni mcharuko sana, hapa jf LOL ,au kwa vile ilionesha kuwa na yeye ni member mwenzetu je labda aliwahi kunitongoza pm nikamkubali kirahisi?
 
Kama roho yako imedunda kwa hili na mie mumeo roho yangu ifanyeje? Mh! Naanza kukufuatilia kwa karibu maana naanza kuamini wewe ni yule tunaefahamiana kiaina! Wajumbe wengine JF hamjaona post hii tafadhali!

Orait, noted😛oa
 
Cheusi asante dear kwa hadithi nzuri.....unaonaje ukiandika mkitabu kabisa hata cha page 80 tu? Naamini kitapendeza na kuwa kizuri. Una kipaji hicho

Hapa nimeona sana hili neno PM linatajwa....kuna nini huko PM?
 
Cheusi asante dear kwa hadithi nzuri.....unaonaje ukiandika mkitabu kabisa hata cha page 80 tu? Naamini kitapendeza na kuwa kizuri. Una kipaji hicho

Hapa nimeona sana hili neno PM linatajwa....kuna nini huko PM?

asante kwa kushukuru,kuna kuna hadithi ya page nyingi tu nimeiandika ila sijui taratibu za uchapishaji,na pia sbb ya ubize natafuta muda wa kufuatilia nijue taratibu lkn ipo siku nitakitoa tu na ww lazima nikupatie copy yako.
Kuhusu pm nadhan kwa sbb nimetaja pm kwenye hii story ndo maana.
 
Back
Top Bottom