wanaJF niliokutana nao.....wamenisababishia balaa

Mim na shemeji yeni tulienda mahala kupata dinner,wkt tunasubiri tuletewe chakula tukiwa tumekaa kwenye viti shemeji yenu akaniaga kuwa anakwenda kujisaidia,alipoondoka nikatoa laptop yangu nikaanza kusurf JF nikiwa nimesign in.

Meza yetu ilikua karibu na mlango wa kuingilia ktk hotel hiyo na mim nilikua nimeupa mgongo mlango huo,kwa maana hiyo mtu anayeingia aliweza kuona kilichopo ktk screen ya laptop yangu.Mwanzon nilikua naficha screen ili mtu sione ninachofanya ila baada ya kuingia JF na kuanza kusoma moja ya thread nilijisahau kabisa kuficha screen.

Haukupita muda nikashangaa wakaka watatu nisiowafahamu wakija mbele yangu wakiwa na mshawasha wa ajabu.Nikiwa bado najiuliza hawa ni wa kina nani mbona kama wananifahamu mmoja wao akasema"Cheusimangala habari yako mkuu".Nikatamani kubisha kuwa mm sio Cheusimangala maana huwa sipendi kabisa urain wajue kuwa Cheusimangala wa JF ndio mim kwani huko uraian wana image tofauti kabisa na hii ya cheusimangala.Nikiwa sijui niwajibu nin mwingine akasema"Yaani cheusie daah kweli hizi avatar zinatudanganya sana maana nilikua na picha nyingine kabisa juu yako tofauti na unavyoonekana."

Nikiwa bado nafikiria jinsi ya kukana kuwa mim sio cheusimangala mara nikamuona shemeji yenu anarudi kutoka maliwatoni alipokua huku akiwatizama vijana wale watatu kwa sura yenye kujiuliza ni wa kina nani.Alipofika karibu ikabidi niwaambie vijana wale" huyu ndiye shemeji yenu" nikitumai kwamba wataondoka na kuniachia nafasi ya kujua nitamweleza nini juu ya watu wale ambao hajawahi kuwaona.

Baada ya utambulisho ule mmoja akasema "ooh bwana shemeji nice to meet you" kisha akaendelea" yaani jamii forums ni pana sana unaweza kukutana na members wenzio katika mazingira usiyotegemea kabisa"
Kisha shemeji yenu kwa mshangao akaniuliza"ina maana mpenzi unaifahamu jamii forums?kabla sijamjibu akauliza swali jengine"wewe ni member au unapita kusoma soma tu kwa nje?Nikiwa na mim nashangaa kuwa kumbe na yeye anaijua jamii forums akaniuliza swali jengine"unatumia username gani huko jamii forums"swali hilo lilinizidishia hofu kwani katika vitu nilivyokua sitaki ajue ni kuwa mim ni cheusimangala wa jamii forums lakini nikiwa bado nafikiria haraka haraka nini cha kumdanganya nikasikia mmoja wa wakaka wale akikohoa kidogo huku wote watatu wakionekana kujisikia vibaya kutokana na shemeji yenu kuonekana kupaniki kwa kugundua kuwa naijua jamii forums akasema" cheusie acha sisi tukuage bana nice to see you".Roho yangu ilidunda sana baada ya yule kaka kuniita kwa jina la cheusimangala.

"Ina maana mpenzi wewe ndiye cheusie!...cheusimangala...!this can not be true!no no no"This is a night mmmm...."shemeji yenu hakumaliza alichotaka kusema kwani alidondoka chini na kupoteza fahamu huku michuzi iliyomwagika kutoka mikononi mwa muhudumu aliyekua karibu yake tayari kwa kutuwekea chakula mezani ikiwa imechafua shati lake zuri la blue alipendalo kuliko yote na bila kuchelewa niliwaona wale vijana watatu wakitoka mbio bila hata kutoa msaada kwa mwenzao Huku nikiwasikia wakiambiana"hii tukairushe wapi wakuu habari mchanganyiko au chit chat?"Nikiwa najiandaa kupiga yowe la kuomba msaada alarm yangu ikanishitua kutoka usingizini.

Unafikiri ni kwa nini ktk ile ndoto shemeji yenu alizimia baada ya kugundua kuwa mim mpenzi wake ndiye cheusimangala?Je mim ni mcharuko sana, hapa jf LOL ,au kwa vile ilionesha kuwa na yeye ni member mwenzetu je labda aliwahi kunitongoza pm nikamkubali kirahisi?
Ndoto yako basi Cheusimangala ikahamia Kwangu, wacha nikumalizie iliishaje najua unahamu ya kujua kilichoendelea, basi Wale vijana watatu walipotoka Mbio njiani si wakadakwa na Polisi wakidhaniwa ni wezi wakapigwa Tanganyika Jeki hadi kituoni kujieleza.

Ndipo walipohadithia hiyo Story yote Mkuu wa Kituo kumbe nae ni Member humu jf akashikwa na Mshawasha aje amuone huyo ''Cheusimangala'' Ndipo alipowauliza hao Vijana watatu wanatumia user Gani ndani ya jf Wa kwanza akasema yeye ni Rejao Mkuu wa Kituo Alistuka Akaguna Mh! wa Pili ni Mwita25 na wa Tatu alikuwa ni Washawasha

Mkuu wa Kituo akaanza na Wa Kwanza Akamuambia wewe Rejao nenda nimekuachia huru (huyu alijua ni Msukule wa Nape asije akamletea matatizo..(Ni ndoto tu usi mind)

Wa Pili wewe Mwita25 utalala humu ndani sababu umekula pesa za chama then umekisariti una kesi zako hapa Nyingi zimewasilishwa na ff na ritz...

Wa tatu ni Washawasha wewe mkuu huwa unapenda kulog off sasa nakupa kazi moja ukanioneshe huyo Cheusi mangala nina hasira nae sana kwani alisema angenialika kwenye sherehe yake ya kuvikwa pete na siku zikapita hajanialika leo lazima alale lock up ukishanionesha nitakuruhusu ulog off...

Kule hubby wa Cheusi mangala alipoanza kuonesha dalili za kuzinduka, Cheusimangala akijawa na hofu akidhania mumewe ndio kesha log off! hafla Mkuu wa kituo akaingia pale mahala huku jicho la mahaba likimmulika ''cheusimangala'' alipogundua kumbe ni kipenzi chake cha primary school kipenzi kilichomfundisha mahaba na ucharuko.

Mkuu wa kituo alistuka kwani alikuwa anatumia nick ya ritz alipokuwa school hapo hapo Cheusimangala alijistukia akitamka kwa nguvu hey ritz jamani ni za siku nyingi my dear? hatujaonana miaka mingi ulikuwa wapi siku zote! mumewe akazinguka hafla kusikia hilo jina akakosa amani kabisa... na mie hapo hapo alarm yangu ikanistua nikaamka niwahi Kwa job...
 
hahahaa safi sana mkuu,
kumbe hawakufanikiwa kwenda kuirusha hewan wakaishia lupango.
leo nitaota tena.
 
pheeeeeew! wish ingekuwa kweli ,mmmmmmh! mara unagundua mwenzi wako ni Rejao au FF hlf huwa mnakutana mara kwa mara jukwaa la siasa ....ila mwenzi wangu anafahamu yangu z it mbaya ,anyway huyu ni mimi huko huko mtaani......kuna watu nahamu ya kuwafahamu hapa jf......
 
Shosty una mtiriko mzuri sana..yani mpaka nimefika uliposema ndoto ndiyo nikajua uliota..Nilidhani ni for real!..

Bora ibakie kuwa ndoto..
 
pheeeeeew! wish ingekuwa kweli ,mmmmmmh! mara unagundua mwenzi wako ni Rejao au FF hlf huwa mnakutana mara kwa mara jukwaa la siasa ....ila mwenzi wangu anafahamu yangu z it mbaya ,anyway huyu ni mimi huko huko mtaani......kuna watu nahamu ya kuwafahamu hapa jf......
Kama kina nani hao unaopenda kuwafahamu ndani ya jf?
 
mimi kiukweli natamani sana kumfahamu mzee mwanakijiji, pakajimmy, faizafoxy, ashadii na firstlady
 
pole kwa kufeel cheated,ila inaonekana hunipendi ndo mana umeudhika kuwa sio ndoto.
Hapana, you got it twisted mami, that isnt the case at all, and definetly not what i meant.

Nimeudhika kwasabu the story is too nice to be fictious.lol

So sikutegemea kuwa itakuwa fiction, thats how nice and exciting it was lol!, unaweza kuwa mtunzi mzuri tu, so take it as a credit bibiye and not hate...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom