Hilo jambo linawezekana kabisa. Either Wamembaka baada ya Kumpiga au Walimpiga baada ya kukataliwa kupewa vitu hayo yote ni makosa makubwa kabisa ambayo hayatakiwi kufumbiwa macho na lazima wachukuliwe hatua za kisheria.
Jeshi letu la Tanzania haliko friendly to Citizens. Mindset zao ni mbovu kabisa na wanajiweka kuwa wako above the law. Mwanajeshi ukimbishia hata kama ni haki yako basi watakuchangia kukupiga hadharani. Haya mambo tunaona kila mara. Utakuta gari za jesho au Polisi ndio zakwanza kuvunja sheria barabarani pasipo kuwa na emergency yoyote. So are they above the law?? Na utaona hakuna mtu anayezungumza, si vyombo vya habari wala Social media hazi condemn upuuzi huu. Tuko very quite ni kama tumeridhika. Huu ni ujinga wetu watanzania. Media zetu kazi kuandika umbeya tu na kubobea kwenye siasa. Hazina mchango wowote katika kuleta mwamko na mwelekeo wa sheria nchini.
Ukiharibikiwa na gari yako barabarani mbele ya kambi ya Jeshi basi watakuja kukutisha na kukudhalilisha hata kama uko na familia yako. Badala ya wao kukupa msaada au kukusogeza sehemu ambayo utapata msaada. Jeshi kazi yake kulinda na kuhudumia Raia wakati wa matatizo, maafa na kulinda usalama. Wananchi hawapaswi kuogopa Jeshi. Mungu aepushe mbali nchi yetu ikitokea mapinduzi ya Serikali Jeshi ndio litakuwa la kwanza kuhujumu watu na kubaka watoto wakike na kuvunja nyumba za watu.
Jeshi latakiwa kuwa wapole kwa Raia. Na endapo watafanya kitu tofauti na maadili ya Jeshi hatua zichukuliwe papo hapo. Lazima tu adopt utilization of law like developed countries. There is no one ABOVE the law. Time imefika kwa Watanzania kujua haki zetu.
Msichana Neema ni Shujaa na amedhulumiwa haki zake za msingi nchini mwake. Lazima apewe support na hili jambo lifikishwe kileleni mwa sheria.