Wanajeshi Arusha wafanya ukatili wa kutisha

Wanajeshi Arusha wafanya ukatili wa kutisha

Baadhi ya wanajeshi kutoka kikosi cha TMA Monduli wanaolinda chanzo cha maji katika kijiji cha Olgilai Arumeru wamemtesa kwa kipigo msichana Neema Alfred baada ya kuwakatalia tendo la ndoa walilohitaji baada ya msichana hiyo kupita eneo hilo wakati akitoka kuokota kuni.

View attachment 444616
Mod: naomba upost huu uzi fb tuchangie kwa wingi huyo binti apate haki
 
Unajua Bongo haya matukio ya sex abuse na rape yanatokea sana lakini watu wanashindwa kufikisha mashitaka katika vyombo vya dola kwa sababu hayapewi kipaumbale na uzito wowote kwenye jamii. Hilo unakubaliana na mimi au hapana??

Jambo la pili unaona vyombo vyetu vya dola vinatii sheria au la??

Jambo la tatu, huyo dada Neema adanganye kufanyiwa hivyo kwa malipo gani anayotarajia kulipwa kwa uongo huo au kwa madhumuni gani?? Kabla hujasema muongo lazima utazame motive ya uongo wake. Kama huoni motive basi hakuna cha uongo. Hayo mambo kina dada zetu wanafanyiwa kila leo.

Sijapinga hoja zako mkuu
 
Bakiza akiba ya maneno hii habari haijajitosheleza
Inatia shaka askari wampige mdada? Ngumu
Kama kweli walimpiga anza kuwaza yafuatayo
1. Alijibu nyodo baada ya kupita njia au sehemu asiyoruhusiwa kupita kwa wakati huo
2. Yaweza kua alipita na mtu wake na wakajibu nyodo kwa askari ndo wakapewa adabu kidogo.
3. Kadundwa na mtu wake ambae ni askari

Kwa kawaida askari akiwa zaidi ya mmoja ni ngumu kumshambulia raia hasa mwanamke bora angekua mwanaume, sheria za kijeshi ziko complicated sana askari hawezi kumshambulia raia bila sababu maana kufanya hivyo ni kujitia risk kwenye kazi yake
Kudos
 
Hana uwezo wa kuzuia asibakwe na wanajeshi halafu wanaheshi wa bongo hawana mambo hayo
 
wanajeshi wangapi? waliwezaje kumpiga wakashindwaje kumbaka? aache uongo aseme tu kapewa kipigo
Unaonyesha usivyo jali. Aliwakatalia ndipo wakampiga. Kumbaka walijua wataangukia kwenye miaka 30 jela. Kumpiga wataweka maelezo kuwa alikatisha eneo nyeti.

Wapigania haki msaidieni ikiwa ni suala la kweli
 
Hao siku zote niwakorofi hata mtu akipita maeneo karibu walipo wao wanakupiga wanakutesa kama wanataka ngumi watafute mechi hata na hedhiopia au wanatuonea sisitu
 
Kwa watu tuliowahi kuishi karibu na kambi za jeshi, hayo mambo yanatokea mara nyingi sana. Kuna mzee mmoja alishawahi kupigwa na wanajeshi mpaka akavunjwa mbavu kisa ng'ombe wake walikatiza eneo la jeshi. Kambi siitaji.
Huwezi kuwaachia ngombe apite kwenye maghala ya silaha jeshini sio Wizara ya kilimo
 
Tatizo michango mingi humu JF imekaa kimaslahi ya vyama,. Ndio maana mambo yasiyo na udhibitisho ni rahisi kupata michango kutosha.

Hiyo hiyo habari ingehusisha Bavicha ungeshangaa michango inavyobadilika toka kwa walewale wanaojifanya kulaani hili tukio hili la bila ushahidi wa kutosha.
 
Mtu ana D mbili form four unadhani weledi wakutumikia jeshi upon kweli? Wengine La saba! Kupata jeshi ni zari kwake na wala hakutegemea sasa kwanini asifanye kazi bila weledi, ifike mahali tuweke qualifications za juu kujiunga jeshi Mana mambo ya manguvu sasa yanaondoka ni Intelligence na Technology ndio Ina take over katika military, Hawa kina mula & Ngosha tuwaache waendelee Kula Dona huko makwao mana akili ya kupambanua mambo hawana kabisa
 
Aende mahakamani tutamchangia pesa akawashitaki jeshi sio la baba zao
 
Back
Top Bottom