Wanaharakati: Ziachieni simu za VodaCom!




Recta!

Wacha ngonjera!!

Huo wimbo wa ajira na kodi hautaingia akilini bila ya kutoa takwimu! Come straight lay out the CIP of Vodacom utueleze wliwekeza shilingi ngapi? How much kodi wamelipa in the name of VAT kwa miaka yao and the rest and how much wamegawana na mafisadi wa CCM! Na ngapi zimekwenda kwa bibi!!
The peanut donations ni danganya toto its only the cost of sms for a few days ila kwa sababu wewe hujui unaona kivuno!!

Kama ita click in my head I go with you bus otherwise mimi sipandi basi la wajinga recta!!! Hata kama umetumwa na ccm kuwatetea lakini Voda ni ufisadi per se come sun come rain ila wewe kula hiyo pombe chafu ya msimbazi humpati mtu makini !!but as usual 90% ya waTZ kondoo wako behind you mpaka utumbukie!!
 

Mkuu,

Ni wazo zuri. Ila naona hasara zake zitakua kubwa kuliko faida.

Binafsi sidhani kama hii mbinu hapa ndo mahali pake. Nijuavyo, hii mbinu ya kususia bidhaa/huduma za kampuni inatumika pale inapokuwa imethibitishwa kwamba shuguli za kampuni husika zinaathiri kwa kiasi kikubwa jamii flani au mazingira. Kwa mfano kampuni ya DeBeers inaponunua almasi kutoka kwa waasi/nchi zisizo na usalama (conflict zones) inakua inafadhili moja kwa moja mauaji na uhalifu mwingine wa kivita huko Sierra Leone na nchi zingine za Africa. Wanaharakati na wanamazingira walipoona haya walihamasisha wanunuzi wa almasi wasinunue bidhaa za DeBeers mpaka watakapojiridhisha kwamba hizo bidhaa/almasi hazijatoka kwenye maeneo yenye migogoro ya kisiasa/conflict zones. Hakika hii kampeni imefanikiwa.

Tukirejea nyumbani, sidhani kama ni muafaka kufananisha Vodacom na DeBeers. Wananchi wanaonufaika kwa huduma na ajira za Vodacom ni wengi. Isitoshe watuhumiwa wa ufisadi wanaomiliki hisa Vodacom ni "minority interest", japo mtaji wao si haba. Hivyo basi, mimi naona hoja ya kususia bidhaa za Vodacom kwavile baadhi ya wanahisa wanatuhumiwa kwa ufisadi ni hoja dhaifu.

Tuendelee kupambana na ufisadi kwa njia za kisheria na kisiasa. Tukipiga vita watuhumiwa binafsi, wataanguka lakini nafasi zao zitachukuliwa na wengine. Tukiupiga vita mfumo wa kifisadi na tukaushinda, basi hata watu binafsi wanaonufaika na mfumo wataangamia na kuisha.
 
Any developments here with this very useful thread. Au tunasubiri bado masaa 24 yaliyobaki? Sijui au pengine yameisha.
 

Inasemekana kuwa hawa hawajalipa kwa kipindi kirefu kodi ya makampuni na hata kulikuwa na utata kuhusu ulipaji wao wa VAT.
Je unaweza kutuwekea data hapa kwa miaka mitano ya nyuma kwa mafanikio haya unayonadi hapa, wamelipa PAYE kiasi gani, Corporation tax kiasi gani, VAT kiasi gani, tax zitokanazo na importation yao ya vitu mbalimbali walilipa kiasi gani? Vinginevyo ni porojo zile zile tunazoletewa na kuzisikia toka kwa promoters wa mafisadi huku zikiwa hazina chembe za ukweli ili kututamanisha ushirika na wezi wakubwa hawa.
 
Kwani issue hapa ni kususia huduma za voda au ni suala kujihami na la kiusalama zaidi kwa wale wanaharakati hususan wanaotumia mtandao wa vodacom...?

Ni vigumu kumuelewa Mwanakijiji kwa kua hajaweka complete information ni kama kitendawili na watu wanajaribu kutegua which kwa maoni yangu in the forum like this angetakiwa awe muwazi zaidi toka mwanzo ili watu waweze kuchambua hoja yake vizuri... but kuna mwanachama mmoja ametoa ushauri kwa mamlaka husika ziangalie suala la privacy kwenye mambo ya simu hasa za mkononi kwamba kwa sasa office ya IGP, DCI, TISS wana uwezo wa kusikiliza chochote kinachoongelewa na watu wanaotumia mtandao wa Vodacom, so kwa kuangalia hilo labda Mwanakijiji anajaribu kutuambia/kuwaambia wanaharakati wa ufisadi kua wawe makini na hasahasa waachane na hizo line sababu zinaweza zikawapa hawa watu sehemu nzuri ya kuanzia katika mapambano yao na watu wanaopambana na ufisadi....( may be hivyo vyombo hapo juu navyo ni vibaraka wa ufisadi)

.... but hayo ni mawazo yangu tu na najaribu kuuweka huu mjadala kwenye upande huo zaidi.... lakini mtenguaji wa kitendawili hiki ni Mwanakijiji na nadhani sasa ameshapata miji mingi na niwakati wake sasa wakukitegua na kueleza alikua na maana gani kuanzisha hii thread.. (may be siko mbali na ukweli)
 
We ndugu uko nchi gani? Tunaomba usituletee udini hapa. Tanzania si taifa la kiislamu kususia bidhaa za Israel. Be carefull usituletee laana katika taifa letu.
Taratibu, taratibu, usilete jazba. Tunazungumza kiungwana humu ndani. Kwa taarifa yako mimi sio Muislam, ni Mkristo aliyezaliwa na kulelewa katika familia ya Kikristo, na nitakuwa Mkristo daima. Naona suala la Israel linawachanganya wengi. Israel ya Biblia na serikali ya Israel ya Netanyahu ni vitu viwili tofauti. Sina haja ya kutoa somo hapa zaidi, lakini kwa kifupi uelewe hivyo. Wapingao sera za serikali ya Israel sio Waislamu tu, bali binadamu wote popote pale walipo wapendao usawa na ubinadamu. Kutetea sera za serikali ya Israel za ukoloni, unyanyasaji na ubaguaji haukufanyi wewe uwe Mkristo bora.

Kwa taarifa yako, kama ulikuwa huna habari, sio wote ambao tupo JF tunaishi Tanzania. Tumesambaa ulimwenguni mwote...lakini bado tu Watanzania. Kwa hiyo, wakati wowote utakapotokea ufisadi wa aina yoyote tutapiga kelele, maana huko Tanzania bado wapo ndugu zetu, mama, baba mjomba, shangazi etc. ambao maisha yao yanazidi kuwa duni kutokana na ufisadi mkubwa ambao unaendela kushamiri.

Utaipata laana kama utalala usingizi mzito wakati binadamu wenzako wanateseka. Kama unafanya hivyo, ndugu yangu, laana ulishaipata zamani.
 


Mkuu Mkereme, naheshimu mawazo yako.

Hizo takwimu nadhani unaweza kuzitafuta mwenyewe.

Haikuwa nia yangu na wala sio lengo la post yangu kuanika takwimu za uchangiaji wa Vodacom katika pato la Taifa kwa namna yoyote. Mkuu, sikuwa na haja ya kufanya hivyo kwani sio jukumu langu na pia ni dhahiri hata takwimu halisi zikitolewa zinaweza kuonyesha uchangiaji mkubwa zaidi ya ninavyoweza kuupata. Ni kazi ya mamlaka husika kufuatilia kama zinaona zinakosa mapato yoyote yanayotegemewa. Vile vile zinaweza kuanika ukwepaji wowote wa kodi wanaoweza kuubaini.

Ninachotaka kusema ni ukweli kuwa UFISADI hauwezi kuondolewa kwa kuua uwekezaji (wa ndani na/au wa nje). Sioni sababu wala faida zitazopatikana kama tamaa yetu itabaki kuwa Vodacom ife. Ususiaji wa namna hiyo ni UFISADI mkubwa zaidi ya ule tunaojaribu kupambana nao. Maana UFISADI huo unaua nguvu yoyote ambayo Taifa linaweza kuwa nayo.

Mkereme, Mimi si mfanyakazi, mwekezaji wala mtu yeyote mwenye interest ndani ya Vodacom. Vile vile, mimi siwezi kutumwa na chama cha siasa kutetea niliyoandika hapo juu. Niliyoyaandika ni imani yangu (si ya kisiasa) kuhusu uwekezaji wa Vodacom nchini na umuhimu wa ustawi wa kampuni kama hizo.

Ukweli ni kwamba, kukimbilia umasikini haiwezi kuwa dawa/silaha ya kupambana na ufisadi wala suluhu ya matatizo yoyote tuliyonayo. Haihitaji jitihada sana kujua hilo.
 
Kama ndo hivyo basi angewapelekea hao wanaharakati kwenye private mail zao.

Nnavyofahamu ukishabandika thread basi unaalika wanajamii wote waijadili.

Yes, lakini haina maana kwamba we kila unalolisoma hapa basi unalichukulia kama amri kumi za Mungu, chuja tafakari ondoka na yanayo faa, ndiyo maana hiki ni kisima cha great thinker, just think about it and adjudicate, afterall the decision is yours!

But as for me.. I say No to 'VODAMAFISDI COM'
 
Voda doesnt need u.. thats the thing... And u cannot harm it in that fashion. Nikama panzi kusimama mbele ya tembo nakusema "hupiti hapa leo" its just STUPID!
 
Hivi ile ultimatum ya 72hrs bado haijapita? Mwanakijiji tunasubiri kufafanuliwa what will happen kabla hatujatupa line zetu za Vodacom.
 
mwanakijiji njoo uwaambie wanaharakati ambao hawakupata ujumbe wako wa kutupa line za voda nini kimewatokea baada ya yale masaa 72 kupita
 
Nadhani hayo masaa 72 yana karibia kuisha. Ngoja tuone kita kacho tokea.
 
usingoje sana ndugu yangu; yawezekana "usione" chochote kwani si vyote vinaonekana.
Asante MMKJJ, kama sio vya kuonekana, maana wengine wetu ambao sio wanaharakati, hukututendea haki kutoonya, vitisho na altimatum ya kuihama voda bila kutoa sababu za msingi, we were a bit disturbed na katuacha na maswali bila majibu kuhusu nia yako halisi.
Hata hivyo asante kwa angalizo, tunajiendelezea zetu na voda yetu, huku tukikamuliwa na kufa kizungu na tai shingoni.
 

ndugu yangu nimesema "yawezekana".. sijui what will happen or how.. ninachojua ni kuwa something will happen. Nimeangalia sana watu wanachosema na kujaribu kuhisi kwanini nimesema nilichosema. Well.. I wish I could give more info but Ican't isipokuwa aliyepewa ujumbe kaupata.
 
Gharama za huduma za voda ndicho kilio cha watu wengi, anayeshauri kuachana na vidacom nia yake ni nzuri. Hiki kilio kitawafikia vodacom na kuwafanya watakakari upya. Huwezi ukauumiza umma kwa bei mbaya za huduma kisha unyamaziwe kwa sababu umeajili watanzania. HAPANA
 
Mkuu Mkjj naomba ufafanuzi ni wanaharakati gani unaozungumzia? Wanaharakati is a broad term. Mimi ambao ni mwanaharakati wa mazingira kwanini nitupe line? Na wale ambao ni wanaharakati wa haki za binadamu je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…