Wanafunzi wa Kidato cha sita Shule ya Sekondari Chamwino wamempa FURAHA YA KUSHTUKIZA mwalimu wao wa HESABU/ADVANCED MATHEMATICS, MR. EMANUEL GEORGE KIPAHO kwa kumnunulia usafiri wa Baiskeli kwa kutambua mchango wake na juhudi zake anazozitoa kufundisha darasani na muda wake wa Ziada.
Shule hii ina michepuo miwili ya EGM NA CBG mwalimu huyu amekuwa mhimili sana kwa wanafunzi hawa.
Matokeo ya kidato cha sita kwa shule hii yamekuwa yakiongozwa na mchepuo wa EGM.
Nafikiri CHAMA CHA WALIMU pamoja na Serikali tuendelee kutoa motisha na Hamasa kwa walimu kama hawa kwani licha ya kutimiza majukumu yao lakini wanatumia muda wao wa ziada kuhakikisha wanapata kizazi Bora.
Leo hawa wanafunzi wametoa Baiskeli kulingana na uwezo wao kuna siku watatoa zawadi ya gari.
Chama kinaweza kuwatambua hata kwa kuwapa vyeti vya uwajibikaji Bora hii itapelekea Walimu kujituma zaidi.
Mwalimu Kipaho pia ni Mwalimu wa Nnidhamu. Mungu amjalie afya pamoja na Walimu wote wanaotumia muda wao wa ziada kuhakikisha Wanafunzi wanafanya vizuri.💪