Wanafunzi na walimu ni kama maadui

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,703
36,143
Mwanangu alirudi nyumbani siku moja huku akiongea kusema "Ile shule siitaki , usiponihamisha siendi tena"
Imagine mtoto wa darasa la kwanza Mwalimu anamwadhibu kwa kumpigisha ukutani.

Hilo nikamtuma wife akaongee na mwalimu aliyefanya huo ujinga likaisha. That was January.

Maisha ya shule huyu mwanangu yanaendelea vizuri.

Majuzi kachapwa kwa kutokufanya zoezi na utoro huku mwanangu hana trend ya utoro. Ilikuwa mistake tu ya utoto aliandika zoezi karatasi ya nyuma badala ya mbele. Akiona uwazi kwenye daftari kwa nyuma huwa anatumia huo uwazi. Sasa mwalimu hakuona zoezi la jana na kuhesabu tu kuwa mtoto hajafanya kazi ya Jana.

Nimeongea na mwanangu kuwa asiandike nyuma sasa hata kama ameacha karatasi isiyo na maandishi.
Sasa hata ingekuwa ni kweli mtoto hajafika shule au alifika lakini hajaandika ni sahihi umchape?

Enzi hizi bado walimu wanaendelea kuchapa watoto?

Walimu mpaka kesho hawajui kuwa mabosi zao sio maafisa elimu, madiwani na ma DED bali wanafunzi.

Je, kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kumchapa boss wake?

Kama watoto ni wasumbufu hiyo haiwapi uhalali wa kuwachapa watoto ni aina ya maboss waliowachagua , wawahudumie vivyo hivyo.

Shule za serikali zinaongoza kwa kuzalisha watoto vilaza kwakuwa walimu hawajagundua kuwa wanafunzi ndio maboss wao.

Wanafunzi na walimu ni kama maadui.
 
Hata biblia imetuasa mara moja Moja kiboko ni lazima, mtoto anasoma saikolojia haraka sana tena vya sa ivi ni vijanja kweli akishabaini kua hawezi kuchapawa pindi akifanya makosa ataanza Tabia nyingi za ajabu

Mtoto anachoogopa ni fimbo, japo siungi mkono uchapaji usiozingatia sheria, umri na Hali za watoto, ila mara moja Moja sio mbaya

Enzi zetu aisee bakora zilikua zinatembea sio poa
 
Hata biblia imetuasa mara moja Moja kiboko ni lazima, mtoto anasoma saikolojia haraka sana tena vya sa ivi ni vijanja kweli akishabaini kua hawezi kuchapawa pindi akifanya makosa ataanza Tabia nyingi za ajabu

Mtoto anachoogopa ni fimbo, japo siungi mkono uchapaji usiozingatia sheria, umri na Hali za watoto, ila mara moja Moja sio mbaya

Enzi zetu aisee bakora zilikua zinatembea sio poa
Mathematics O level nimefundishwa na Mzungu, ni mmarekani. Anasema kule darasa zima wanapata One na ikitokea mtoto ka loose basi ana two.

Adhabu ya viboko waliiondoa kwakuwa ni utumwa.

Je, kati ya nchi hii ya mafimbo na US ni nchi ipi ina wasomi bora?

Hizi shule za kata ambazo walimu wanashindana kupiga fimbo ukitazama matokeo ya form four ni uchafu mtupu
 
Acha tu! Alinificha hadi ngozi nyeupe ikatoka
Kisa nimekosea kuhesabu vijiti😔
Pole sana Mkuu

Najua alifanya hivyo Kwa lengo la kukusaidia ufanye vizuri Masomo yako

Ndiyo maana leo hii Wazee tunajivunia kukupata wewe kama Daktari Bingwa wa magonjwa ya watoto 😜🤗
 
Kuna mwalimu shule ya msingi yombo pale kiwalani alinipiga kwenzi aisee na mie nikarudisha usiwe mnyonge aisee walimu ni miyeyusho sana
 
Pole sana Mkuu

Najua alifanya hivyo Kwa lengo la kukusaidia ufanye vizuri Masomo yako

Ndiyo maana leo hii Wazee tunajivunia kukupata wewe kama Daktari Bingwa wa magonjwa ya watoto 😜🤗
Dahhh! Mkuu usinikumbushe machungu mambo ya kua daktari nilitamani lakini kichwa cha science nilikua sina😂
 
Sidhani kama ni sahihi kutumia Lugha hiyo mbaya Kwa Walimu wetu.

Ungeweza kutumia Lugha ya kawaida kuelezea hayo uliyotaka kuyaeleza na ujumbe ungefika tu...

Tufahamu kwamba Kuna wakati watoto wetu huwa wanakuwa watundu sana na wanaudhi hivyo kustahili Viboko japo kidogo kuwarekebisha.

Tuliosoma zamani, Viboko ilikuwa ni kawaida kuchapwa ili kutukumbusha kusoma Kwa bidii pamoja na kufanya mazoezi ya nyumbani (homework).

Bahati mbaya nilisoma Shule yenye Walimu Wanajeshi.

Wao walikuwa wanachapa na kutoa adhabu za kijeshi kama ile kuita mvua, Push ups na hata kuegemea ukuta kichwa Chini miguu juu n.k

Tuache kuwalea watoto kimayai mayai na tukumbuke maandiko yanasema "usimnyime Mwanao Viboko"

Mtoto akikosea lazima aadhibiwe ili kumnyoosha.
 
Back
Top Bottom