2025DG
JF-Expert Member
- Jan 30, 2023
- 508
- 1,426
Ni hisia za furaha zilizopitiliza hadi kuleta machozi katika mashavu ya Emmanuel Kipaho ambaye ni mwalimu katika Shule ya Sekondari Chamwino mkoani Dodoma baada ya kupewa zawadi ya baiskeli na wanafunzi wake.
Tukio hili linarandana na msemo unaosema ‘chanda chema huvikwa pete’, naam!
Hivi ndivyo unavyoweza kusema kwa jabali hili la somo la Hisabati ambalo hutembea takriban kilomita nane kila siku kuwahi kutimiza ndoto za watoto wa Kitanzania katika shule hiyo.
Kutokana na kujitoa kwa mwalimu huyo, wanafunzi wanaosoma kidato cha sita katika shule hiyo waliamua kumshtukiza kwa kumzawadia baiskeli.
“Kwangu ilikuwa ni surprise (kushtukiza) nilipigiwa simu na mwalimu mkuu msaidizi akinieleza kuwa wanafunzi wananihitaji shuleni Jumamosi (Julai 29, mwaka huu).
Nikamuuliza kuna nini, hakunijibu badala yake akaniambia hafahamu,”amesema Kipaho.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita, William Zawadi amesema wazo la kumpatia zawadi mwanafunzi huyo lilikuja baada ya kutambua kuwa wanafunzi wa shule nyingine hawakuwa wamefika mbali kama wao walipofika.
Amesema mara baada ya kumaliza likizo, walijadiliana na kuona kuwa wamnunulie baiskeli atakayoitumia kama usafiri kwenda na kurudi shuleni kwa sababu wanafunzi hao hawakuwa na uwezo wa kumnunulia gari.
Amesema katika fedha zao za matumizi kila mwanafunzi alijitolea Sh5, 000 na kufanya jumla ya Sh190, 000 wakaenda kumnunulia baiskeli.