Wanafunzi kushambulia kwa mawe Ofisi za Mtaaluma Shule ya Sekondari Nyiendo wilayani Bunda kunatoa taswira gani kwa walimu na wanafunzi shuleni hapo?

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
201
440
šŸ„²
 
Attachments

  • FB_IMG_1698672998698.jpg
    FB_IMG_1698672998698.jpg
    58.1 KB · Views: 10
Red card zihusike, hapo wakilea upuuzi watavuna wendawazimu.

Fukuza wote waliohusika na ujinga huo bila huruma wala busara au hekima warudi kwao wakawarushie wazazi wao hayo mawe.
Red card na wamebakiza wiki Moja tu wafanye mtihani wao wa kuhitimu

Hapo kama kuna hasara wamesababisha adhabu mbadala labda ni kuzuia leaving, results slip na vyeti Kwa wanafunzi wote wa kidato cha nne mpaka pale watakapolipa fidia ya uharibifu
 
Hata wangekuwa wamebakiza mtihani mmoja wakifanya ujinga kama huo ni kufukuza tu.

Dawa ya moto ni moto.
 
Wasalaam wanajamvi,Kuna jambo limetokea kwenye shule ya Nyiendo Sekondari jumatano iliyopita majira ya saa 12:00 jioni.Utaratibu wa shule ni watoto kutoka saa 11:00jioni.Utaratibu huu ni mzuri sana maana unampa wasaa mzuri mwanafunzi kuweza kujisomea katika muda wa ziada.
Awali utaratibu huu ulikubalika ufanyike wakati huo watoto wakiendelea kupata chakula shuleni wakati wa jioni.Zoezi lilianza na kuendelea vizuri mpaka pale mahusiano ya walimu na wazazi yalipoingia dosari hali iliyopelekea wazazi kususia mchango wa chakula shuleni.
Pamoja na wazazi kugomea utoaji wa chakula,mkuu wa shule na walimu wake waliweka nta masikioni na kuamuru mwanafunzi awe amekula au ana njaa atakaa shule mpaka hiyo jioni.Sasa hapo ndipo likaanzia tatizo.
Mwalimu aliyekuwa zamu ajulikanae kwa jina la Monica Deogratias aliamuru kengele kugongwa ili wanafunzi watawanyike.Wanafunzi walipofika parade wakaanza kupaza sauti "tuna njaa tuhurumieni....!" Walimu nyie mna mishahara mmekunywa chai tuhurumieni......"Wakaendelea ."...Tutawanyisheni bwana tumechoka wengine tuna dozi nyumbani...."Naye akawajibu mnajifanya mnajua sana eti sasa subirieni.Akawatelekeza parade na kuingia ofisini.Kelele zikazidi sasa hadi ikawa kero juu ya kero....
Hali hiyo ikapelekea Makamu Mkuu wa shule ambaye inajulikana WAZI ni smart sana kichwani Masue Tarsila kumfuata mwalimu wa zamu na kumuuliza vipi T.O.D(Teacher on Duty)hawa wanafunzi bado una kazi nao?Akajibiwa kijeuri "madamu waache nipo nao.....!"
Ghafla wanafunzi wa kidato cha nne waliokuwa mistari ya nyuma wakaanza kurusha mawe kuelekea ofisi ya mtaaluma.Kinachoshangaza wengi iweje wanafunzi wale washindwe kurusha mawe ofisi ya walimu, ofisi ya mkuu wa shule ama ofisi ya malezi ambazo zipo karibu yao wakaamua kurusha mawe ofisi ya mtaaluma?Maswali ni mengi kuliko majibu.....Mimi na wewe hatuijui labda tumpelekee mganga kuku na udi atueleze!

Kikubwa walimu tambueni hii generation ina demands zake nyie mliohitimu kidato cha nne miaka 10 iliyopita na kuendelea tambueni nyakati zimebadilika.Busara,umoja kati yenu utaleta tija!

Picha chini wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyiendo katika Moja ya mahafali yao ya miaka ya hivi karibuni.

Nawasilisha mimi mjukuu wa kigogo!
Si kweli wanafunzi walikuwa na njaa kama wanavyodai, huu ni mpango uliopangwa na wazazi pamoja na wanafunzi wenyewe wawe wanatoka mapema ili waweze kurudi nyumbani kusaidia wazazi wao kulima na kuvuna bangi na mihadarati mingine.
 
Wasalaam wanajamvi,Kuna jambo limetokea kwenye shule ya Nyiendo Sekondari jumatano iliyopita majira ya saa 12:00 jioni.Utaratibu wa shule ni watoto kutoka saa 11:00jioni.Utaratibu huu ni mzuri sana maana unampa wasaa mzuri mwanafunzi kuweza kujisomea katika muda wa ziada.
Awali utaratibu huu ulikubalika ufanyike wakati huo watoto wakiendelea kupata chakula shuleni wakati wa jioni.Zoezi lilianza na kuendelea vizuri mpaka pale mahusiano ya walimu na wazazi yalipoingia dosari hali iliyopelekea wazazi kususia mchango wa chakula shuleni.
Pamoja na wazazi kugomea utoaji wa chakula,mkuu wa shule na walimu wake waliweka nta masikioni na kuamuru mwanafunzi awe amekula au ana njaa atakaa shule mpaka hiyo jioni.Sasa hapo ndipo likaanzia tatizo.
Mwalimu aliyekuwa zamu ajulikanae kwa jina la Monica Deogratias aliamuru kengele kugongwa ili wanafunzi watawanyike.Wanafunzi walipofika parade wakaanza kupaza sauti "tuna njaa tuhurumieni....!" Walimu nyie mna mishahara mmekunywa chai tuhurumieni......"Wakaendelea ."...Tutawanyisheni bwana tumechoka wengine tuna dozi nyumbani...."Naye akawajibu mnajifanya mnajua sana eti sasa subirieni.Akawatelekeza parade na kuingia ofisini.Kelele zikazidi sasa hadi ikawa kero juu ya kero....
Hali hiyo ikapelekea Makamu Mkuu wa shule ambaye inajulikana WAZI ni smart sana kichwani Masue Tarsila kumfuata mwalimu wa zamu na kumuuliza vipi T.O.D(Teacher on Duty)hawa wanafunzi bado una kazi nao?Akajibiwa kijeuri "madamu waache nipo nao.....!"
Ghafla wanafunzi wa kidato cha nne waliokuwa mistari ya nyuma wakaanza kurusha mawe kuelekea ofisi ya mtaaluma.Kinachoshangaza wengi iweje wanafunzi wale washindwe kurusha mawe ofisi ya walimu, ofisi ya mkuu wa shule ama ofisi ya malezi ambazo zipo karibu yao wakaamua kurusha mawe ofisi ya mtaaluma?Maswali ni mengi kuliko majibu.....Mimi na wewe hatuijui labda tumpelekee mganga kuku na udi atueleze!

Kikubwa walimu tambueni hii generation ina demands zake nyie mliohitimu kidato cha nne miaka 10 iliyopita na kuendelea tambueni nyakati zimebadilika.Busara,umoja kati yenu utaleta tija!

Picha chini wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyiendo katika Moja ya mahafali yao ya miaka ya hivi karibuni.

Nawasilisha mimi mjukuu wa kigogo!
Mwalim tumeona ujumbe wako. Simmering haki
 
Red card na wamebakiza wiki Moja tu wafanye mtihani wao wa kuhitimu

Hapo kama kuna hasara wamesababisha adhabu mbadala labda ni kuzuia leaving, results slip na vyeti Kwa wanafunzi wote wa kidato cha nne mpaka pale watakapolipa fidia ya uharibifu
Siyo lazima wafanye wakiwa shuleni, km wametenda jinai wakihurumiwa saaaaana watafanyia gerezani. Vitoto vya sku hizi ni vitovu vya nidhamu sn hata kwa wazazi wao. Kichwani penyewe peupe wanafauli kimtindo tu ingekuwa kipindi chetu Pepa tulizokuwa tunafanya Tena ktk nyakat ngumu, no tuition, no enough books, pamphlet lenyewe kulipata ilikuwa mbinde, shule zilikuwa umbali mrefu sn zaidi ya 10-30 na tulitembea kwa mguu au baiskeli lakini tulipasua Pepa kwa viwango vya kimataifa. Hawa wa sasa wanajua ngono tu na kuvaa milegezo but most of them are empty.
 
Walimu wa kizazi hiki sijui Mana matatizo gani, mmeacha kufundisha watoto wetu mmegeukia uripota na ushabiki maandazi
 
Wangeweza kuondoka pasi na kurusha mawe kwenye ofisi(kuharibu Mali za shule )
Hapo kama Kuna kilichoharibika ni wajiandae na malipo
Afrika kila kitu ni ukatili. Ndiyo maana tunakuja kuwa na viaongozi wasio na empathy. Hao walimu wana ubongo wa nguruwe?
 
Back
Top Bottom