Wanafunzi Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) wamegoma

Wanafunzi Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) wamegoma

Vyuo vya dini mf.SAUT ukiandamana umetimuliwa wao wanasema mkataba wako na loan board hauwahusu utapiga shule kama kawaida ata usipopewa mwaka mzima, yan kwao n kama vle mzazi kakunyima hela hom af unaandamana chuoni


Kwa zama hizi lazima kila mtu asimame imara kupigania haki yake. Taratibu za kudai haki zinaeleweka! Haiwezekani watu mna shida pesa hakuna then mnaogopa kudai ati chuo hakiitambui bodi ya mikopo! Haiitambui vipi wakati ada wanapokea kutoka hiyo bodi? Nadhani enzi za kutemea chuo flan kigome na wengine wakomae madarasani and still wafurahie matunda ya mikopo zimekwisha. Kama kuna shida za msingi simameni pamoja na muwe na kauli na msimamo mmoja.Nakumbuka sana ule wimbo wa " Solidarity forever" enzi za akina Mtatiro.
 
Habari wanaJF,

Sote tunaumbuka namna mheshimiwa raisi alivyokataa mikopo kucheleweshwa sasa tataizo limejitokeza tena na wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu.

Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizo kuwa zikitolewa na bodi juu ya lini fedha hizo zitatolewa.

Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki mbili pasipo kupatikana.

Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.
 
Mnamgomea nani hapo maana UDSM (kama chuo) hausiki na kutoingizwa kwa hizo pesa. Fuateni HESLB, Prof. Mukandala fukuza hao wote.
 
Mnagomea nani hapo maana UDSM (kama chuo) hausiki na kuingizwa kwa hizo pesa. Prof. Mukandala fukuza hao wote.
Wanagomea kama wanaudsm na chuo kina mamlaka ya kuwasaidia na ndo maana tangazo la jumatatu linaonesha utawala na serikali walithibitisha
 
Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu.

Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizo kuwa zikitolewa na bodi juu ya lini fedha hizo zitatolewa.

Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki mbili pasipo kupatikana.

Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.

Chanzo:Mwananchi online
 
Kunji mnalipigia wapi rev square au utawala nije kuwapa kampan.poleni Sana
 
generation ya hovyo hovyo. siku hizi vyuo migomo yenu ni kutetea matumbo yenu tu. mambo muhimu ya kitaifa hata kauli tu hamatoi.
Wacha ujinga, hiyo ni haki yao, bila chakula wataishi vipi
 
Ahadi ya Magufuli kwa wanachuo!
''Nitahakikisha fedha mnapata kwa wakati,sio mnacheleweshewa fedha ambazo ni haki yenu''!
Leo hii yuko busy na vipele amesahau ahadi zake!
 
Magufuli nchi imemshinda mapema sana tatizo kubwa likiwa ni kukurupuka na kudharau wengine wakati akiwa anagombea alisema wanafunzi watapewa mikopo yao kwa wakati sasa hivi imekuwa tofauti ama kweli siasa unafiki.
 
Solution simple tuu akija kesho kutwa hakuna mwanachuo kwenda kweny uzinduz wake wanazingua wiki ya 10 hakuna pesa
 
Back
Top Bottom