Wanadiplomasia Wabobezi wameanza kupotea na ni adimu sana Tanzania miaka hii ya karibuni

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,328
24,211
1696338652732.png

John Malecela

1696338479178.png

Salim Ahmed Salim
1696338767262.png

Mrisho Kikwete
1696338544812.png

Balozi Mahiga
1696338909118.png

Liberata Mulamula

images.jpeg-4.jpg

Balozi Asha Rose Migiro( kunradhi balozi)

edmainphoto-1.jpg

Prof Anna Tibaijuka( kunradhi Prof)

Kuna wakati Tanzania tulikuwa na hazina kubwa ya wanadiplomasia waliokubuhu kutetea maslahi ya nchi na Afrika kwa ujumla.

Kizazi hicho sasa kimeanza kutoweka kwa kasi.

Wana Diplomasia wanaoteuliwa sasa kuwa Mabalozi ni wale waliostaafu kazini na kiukweli hawana nguzu za kuendesha diplomasia kikamilifu.

Tulikuwa na Career Diplomats, Diplomats waliokulia, kufundishwa na kutekeleza kazi za kidiplomasia kwa weledi mkubwa.

Walikuwa wana uwezo wa kudiffuse diplomatic tiffs ktiya nchi na nchi, na kati ya nchi yetu na nchi nyingine duniani.

Hili limenijia kichwani baada ya sherehe ya juzi kumuenzi Dr Salim Ahmed Salim , mwana Diplomasia aliyebobea na kujulikana duniani pote.

Je leo tunaweza kupata mwana diplomasia mwenye CV utendaji na kuthubutu kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UN auo Umoja wa Afrika?

Serikali ingefaa kuliona hili kwa uzito wake.

UPDATE

20231013_153431.jpg

Asante sana mama Samia, kwa tamko lako la kuirudishia Tanzania umaarufu uliokuwa nao kidiplomasia.
Nakushukuru Mama Samia kwa kuwa msikivu, kwa michango chanya kwa Taifa.
 
Nhar sheftek 9dami, banli zhri ana

Ntaya mktabi, w nta 3ini ana

Kat7ama9ni kat7ama9ni, wmajayb khbar

Loukan bidiya, ana 9lbi nsh3l fih nar
 
Kuna wakati Tanzania tulikuwa na hazina kubwa ya wanadiplomasia waliokubuhu kutetea maslahi ya nchi na Afrika kwa ujumla.

Kizazi hicho sasa kimeanza kutoweka kwa kasi.
Mkuu Jidu, Jidu La Mabambasi , naunga mkono hoja, Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa
Wana Diplomasia wanaoteuliwa sasa kuwa Mabalozi ni wale waliostaafu kazini na kiukweli hawana nguvu za kuendesha diplomasia kikamilifu.
Ni kweli, naunga mkono hoja, wengine wanateuliwa ubalozi na kupostiwa nje ili tuu kupunguza kelele!, wengine wanapostiwa nje kuondoa kiwingu, wale ma DGIS!.
Tulikuwa na Career Diplomats, Diplomats waliokulia, kufundishwa na kutekeleza kazi za kidiplomasia kwa weledi mkubwa.

Walikuwa wana uwezo wa kudiffuse diplomatic tiffs ktiya nchi na nchi, na kati ya nchi yetu na nchi nyingine duniani.
Hili nimelizungumza hapa Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?
Hili limenijia kichwani baada ya sherehe ya juzi kumuenzi Dr Salim Ahmed Salim , mwana Diplomasia aliyebobea na kujulikana duniani pote.

Je leo tunaweza kupata mwana diplomasia mwenye CV utendaji na kuthubutu kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UN au Umoja wa Afrika?
Hatuna!. Labda yule dogo kule Asia
Serikali ingefaa kuliona hili kwa uzito wake.
The good one aliyepo ni Balozi Mulamula, ndio hivyo tena, alipoondolewa hatukuelezwa sababu, as if uteuzi wa a carrier diplomats ni hisani ya rais aliyepo madarakani!. It's not!. Mabalozi wa kuteuliwa kwa hisani ya rais, yes waendelee kuteuliwa lakini mabalozi wa carrier diplomats waendelee kupikwa, huwezi kuwatetegea mabalozi hisani tuu na kuwaondoa carrier diplomats kwa majungu majungu!. Nimeuliza hapa Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
P
 
Pamoja na yote zama nazo zimebadilika.....

Mathalani komredi El Commandante Salim A.Salim ni kizazi cha wapigania UHURU wa Zanzibar/Tanganyika.....

Kilikuwa ni kipindi cha mapambano ya kusimama kama TAIFA.....akakutana na siasa za KIJAMAA zenye upande mkubwa tu duniani.....

Akajitupa "miguuni" mwa siasa hizo.......

Upande wa pili ,China ikataka kuondolewa UANACHAMA wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.....El Commandante Salim A.Salim akapambana kuhakikisha kiti cha CHINA hakipokwi hiyo nafasi.....

Leo hii ni yeye pekee aliye mshindi wa tuzo ya HESHIMA YA MARAFIKI WA CHINA BARANI AFRIKA....

Hakuna mwafrika mwingine aliyetunukiwa hivyo

#Siempre Mwanadiplomasia El Commandante Salim Ahmed Salim

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom