Picha Adimu ya Julius Nyerere, Salim Ahmed Salim na Ali Hassan Mwinyi 1980s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
Picha hiyo hapo chini kaniletea ndugu yangu na kaniandikia maneno haya:

"Picha adimu hiyo nimekutunuku, iandikie habari."

Kulia ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dr. Salim Ahmed Salim na Rais Ali Hassan Mwinyi.

Nyuma ya Dr. Salim Ahmed Salim ni Dr. Salmin "Komando" Amour.

Kwa kuwa nimeombwa niandike nitajaribu.

Nitawaangalia watu hawa kwenye picha na nitaeleza mimi nawakumbukaje.

Komando Dr. Salmin Amour hii "Doctorate" yake ilizua mjadala mkali sana magazetini katika miaka ya 1990.

Baadhi ya watu wakihoji ithibati yake.

Nakumbuka Ali Nabwa alitoa majibu ya utetezi lakini alipata shida sana.

Nakumbuka msomaji mmoja akasema hakuna haja ya watu kubishana kwa jambo ambalo ni rahisi sana kuthibitishwa.

Akasema itakuwa vyema ijulikane chuo alichosoma, utafiti wake wa huo uzamivu unahusu nini na nani alimsimamia, yaani nani "supervisor" wake na mwisho iwekwe "dissertation" yake isomwe.

Sikumbuki baada ya hapo nini kilitokea.

Naweza pia nikaeleza mkasa wa Dr. Salmin Amour kuiingiza Tanzania katika OIC mwaka wa 1993 vipi jambo hilo lilivyomkera Mwalimu Nyerere na kumpa shida kubwa sana Rais Ali Hassan Mwinyi.

Mkasa huu ulianza mwaka wa 1989 wakati Zanzibar ilipoiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitaka Zanzibar ipate "Obsever Status" katika OIC.

Waziri Mkuu Joseph Warioba alilipeleka ombi lile kwa Salim Ahmed Salim aliyekuwa Makamu Waziri Mkuu.

Salim Ahmed Salim alizuia ombi lile.

Sasa Dr. Salmin Amour alipokuja kuitumbukiza Zanzibar katika OIC Bunge likawaka moto.

Likaundwa kundi la wabunge 55 waliodai kuwepo serikali ya Tanganyika.

Rais Ali Hassan Mwinyi akapata shida kubwa sana hali kadhalika Waziri wa Nchi za Nje Ahmed Diria.

Sukwa Said Sukwa akasema Bungeni kuwa anaeweza kuweka mambo sawa ni Mwalimu Nyerere.

Nyerere akasema Zanzibar ijitoe kwanza OIC ndipo yeye ataingia kuuzima moto uliokuwa unawaka nchi nzima.

1696331780497.png

1696331813972.png

Hivyo ndivyo ilivyokuwa."
 
Mzee salaam, uliyoyaandika ni mazuri lakini hayaunganishi taswira ya kwenye picha.
Nadhani ungeanzia kuteuliwa kwa Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar kisha Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Kukataliwa kwa Salim Ingawa alikuwa most qualified nyakati zote anagombea..
Kisha kuinuka na kuanguka kwa Komando Salmin
Shukran
 
Truth,
Ningeweza lakini nilipenda kuandika hayo.
 
Mzee salaam, uliyoyaandika ni mazuri lakini hayaunganishi taswira ya kwenye picha.
Nadhani ungeanzia kuteuliwa kwa Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar kisha Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Kukataliwa kwa Salim Ingawa alikuwa most qualified nyakati zote anagombea..
Kisha kuinuka na kuanguka kwa Komando Salmin
Shukran
Hayo andika wewe, maana unayajua, mtoa hoja kaandika anayoyajua
 
Safi. Nimejifunza jambo kwenye historia ya Tanganyika na Zanzibar. Naomba kudokezwa watu wangapi wameshashikilia hiki cheo cha naibu waziri mkuu. Na kilikuwa na tija gani?
 
Safi. Nimejifunza jambo kwenye historia ya Tanganyika na Zanzibar. Naomba kudokezwa watu wangapi wameshashikilia hiki cheo cha naibu waziri mkuu. Na kilikuwa na tija gani?
Nawajua Salim Ahmed Salim,Augustino Mrema na huyu wa sasa Dotto Biteko halafu wote wameteuliwa na Marais kutoka Zanzibar(sijui kwa nini!)
 
Isingekuwa figisu za wana mtandao huyu Mzee alitakiwa afuate baada ya Mwinyi
 
Komando Dr. Salmin Amour hii "Doctorate" yake ilizua mjadala mkali sana magazetini katika miaka ya 1990.

Baadhi ya watu wakihoji ithibati yake.
Nakumbuka sekeseke la kununua Benz ya wizi kama sijakosea iliibiwa South Africa ikauzwa kwa SMZ
 
Nyerere akasema Zanzibar ijitoe kwanza OIC ndipo yeye ataingia kuuzima moto uliokuwa unawaka nchi nzima.
Zanzibar haijujitoa OIC, ilitolewa kwa kulazimishwa kwa ahadi Tanzania ndio itajiunga.
Azimio la kuunda serikali ya Tanganyika lilipitishwa, ndipo Mwalimu akawa mbogo na kulihutubia Bunge lilipokaa kama kamati ya chama, ndipo Azimio hilo likafutwa!.

Sasa kitu cha ajabu sana kuhusu Azimio lile, lilikuwa ni Azimio halali kabisa na lilipitia hatua zote!, lakini hivi karibuni Bunge letu limewahi kupitisha Azimio batili, Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG?

Nilipowatonya wabunge wetu hoja hii Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba ndipo waheshimiwa wabunge wetu, wakalisunda uvunguni kimya kimya Azimio lile batili, na kuipokea Ripoti ya CAG, ila Azimio hilo batili, japo halikutekelezwa lakini bado lipo!.

Ni ajabu sana Azimio halali la Bunge linafutwa, halafu Azimio batili lipo!
P
 
Inasemekana Salim alikuwa mtiifu sana kwa Mwalimu Hata ukiisoma hiyo Picha utapata jibu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom