Wanachama wa CCM maji yamewafika shingoni

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,160
Katika historia ya nchi hii, hakijawahi tokea kipindi cha majaribu ya aina hii, ambayo wanaccm wanapitia hivi sasa

Huu uchaguzi wa serikali za mitaa, umewavua nguo na hivi sasa mpo uchi wa mnyama

Kitendo cha hao wasimamizi wa uchaguzi, ambao ni makada wa CCM kukata majina ya wagombea wa upinzani kwa sababu za kipuuzi kabisa, ambazo hata mtoto mdogo hawezi kuthubutu kuzifanya

Tumeshuhudia hao wasimamizi wa uchaguzi wakikata majina ya wagombea wa upinzani kuwa eti hawajui kusoma na kuandika, ambapo wengine ni diploma holders!

Tumeshuhudia pia wakidai kuwa baadhi ya wagombea wa upinzani wakiwa disqualified kwa madai kuwa hawana shughuli maalum za kujipatia kipato, wakati wanajuliksna na wakazi hizo sehemu wanazoishi kuwa wana shughuli maalum za kuwaingizia kipato.

Lakini hao wasimamizi wa uchaguzi wamelazimika kuyatenda hayo ikiwa ni "maagizzo" maalum baada ya kikao chao walichofanya pale Magogoni!

Tumeshuhudia pia wasimamizi wa uchaguzi wakiwaengua zaidi ya asilimia 90 ya wagombea wa vyama vya upinzani kuwa hawana sifa za kushiriki katika uchaguzi huo wakati wenzao wagombea wa CCM wakipitishwa kwa asilimia 100!

Baada ya vyama makini vya upinzani kutangaza kujitoa, tunamwona Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo, akitangaza kuyarejesha majina yote ya wagombea wa vyama vya upinzani yaliyokuwa yamekatwa awali!

Hivi katika mazingira ya aina hiyo bado tu nyinyi maccm mnaendelea tu kung'ang'ania tu ni lazima uchaguzi huo uenddlee kufanyika tarehe 24 mwezi huu?

Ni kwanini basi hamuwi waungwana wa kukiti kuwa ni nyinyi ndipo mliouvuruga uchaguzi huu, kwa hivyo muwaombe samahani wananchi wa nchi hii, kwa kadhia kubwa mliyoisababishia nchi hii na hivyo muahirishe uchaguzi huu hadi tarehe nyingine, ili uandaliwe upya chini ya Tume mpya ya uchaguzi itakayoridhiea na vyama vyote vya siasa.

Kwa kuendelea kuonyesha ubabe na ulevi wa madaraka na kuendelea na UCHAFUZI huu bila kuuahirisha, hakika nyinyi wanaccm mnalipeleka shimoni Taifa letu.
 
Achana na mambo ambayo hayaondoi njaa yako wala kukupa shibe. You can’t change the world
 
Kinana alikuwa mwanamkakati mzuri wa kisiasa, ambaye nyakati za uchaguzi aliivusha CCM ktk changamoto nyingi. Lkn waraka wake na mzee mwenzake wakambeza, haya sasa tunashudia vitimbwi vya kisiasa kupitia hawa makada "naive" sampuii ya akina Jafo wakicheza bahati na sibu ndani ya ulingo mpana wa kisiasa bila kujali madhara.
 
Jidanganye......Anawamudu wote hao. Kote huko kaweka watu ambao hawakutegema kukwaa vyeo hivyo
Hata Mugabe enzi zake alijidanganya hivyo hivyo kuwa amewaweka watu wake kwenye hayo majeshi, lakini ikafika wakati wakamgeuka na kumwambia Mzee tuondokee na tuachie Ikulu yetu na Mzee Mugabe akatii!
 
CCM wanapaswa kujua ili wawepo madarakani sio lazima kuua upinzani..

Ni ngumu Sana kulazimisha raia waipende ccm huku Uhuru wa kutoa maoni haupo, demokrasia haipo, wapinzani kuzuiwa haki zao..
 
.
IMG_20191107_154617.jpeg
IMG_20191107_154613.jpeg
 
jamaaa anaweza kuwaangushia jumba bovu kina January, Kinana, etc kuwa ndiyo wanaomhujumu ili aonekane mbaya.

tusubiri... maana CCM kwa spinning ndiyo wenyewe!
 
Back
Top Bottom