Wana UKAWA tunamhitaji Prof. Lipumba lasivyo patachimbika

Wana UKAWA tunamhitaji Prof. Lipumba lasivyo patachimbika

Ww mweu kweli kawe mtiifu ccm.mpuuzi ww uwezi tupangia mbona kabla awajaungana ukusema lipumba amie cdm.taira ww
 
Wana Jf wasalaam!
Likiwa joto la uchaguzi limeanza kupanda lakini kwa upande wa UKAWA bado wana mtihani mkubwa sana kumchagua atakaye wawakilisha kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Wana UKAWA wengi wamekuwa wakipendelea Mh prof .Lipumba apeperushe bendera ya UKAWA kwani kwa sasa ana mvuto ndani na nje ya UKAWA kuliko Dr Slaa ambaye anaonekana kulazimisha lazima agombee!

Wana Jf mwezi December nilipata nafasi ya kukaa na vijana kama kumi pale Tengeru na tulibadilishana mawazo kuhusu siasa za Tanzania na wengi walijikita kujadili nani anafaa kugombea Urais kati ya Lipumba na Slaa hapa ndio ubishi ulipo anza na wengi walitaka Slaa apumzike wakisema Lipumba ndio anaye faa kipindi hiki kama wanataka kuchukua nchi na atawasaidia kufuta zile propaganda za udini.

Lakini wengine walishikilia msimamo kuwa hata kielimu Lipumba anamzidi Slaa kwani Slaa hana Elimu yeyote zaidi ya kusomea dini na Ikulu hatupeleki kiongozi wa dini kwakweli kwenye hili walibishana sana wengi wakisema Elimu ya Slaa haitambuliki kimataifa na si mtaalam wa jambo lolote.
Kuna mwingine aliendelea kusema kuwa Slaa hafai kugombea Urais maana amekuwa akichochea migogoro ndani ya chama chake na kuwagawa wanachama kwenye makundi!

Wengi walikuwa wana sisitiza kuwa patachimbika kama Lipumba hatopitishwa na hakutakuwa na maelewano kwenye hilo na wakasema Lipumba asipopitishwa kura zao watampa mgombea wa CCM kama walivyo fanya 2010!

Wana Jf joto la uchaguzi liliendelea nilipo pata safari ya kwenda Tanga nilipita mtaa fulani pale Tanga mjini na hapo nilikuta wakijadili siasa kwa upana na wengi walionekana kuunga mkono UKAWA na walikuwa wanasema wana furahishwa na mwenendo wa UKAWA lakini wana kerwa nakampeni za chinichini zinazo fanywa ili kumpitisha Slaa kugombea Urais.. na wengi walikuwa wakiongea kwa jaziba huku wakisisitiza kuwa mipango ya kumpitisha Slaa kugombea Urais hazito kubalika na patachimbika kabisa siku hiyo na hawatoburuzwa na mtu...
Kuna kijana mmoja alisema kuwa wao kama UKAWA wana mhitaji Lipumba lasivyo patachimbika ..maana wanaona dalili za mizengwe! Pia alisema ana kerwa na baadhi ya viongozi wao kuwatuma vijana wao kwenye mitandao ili wawapambe na kuwapigia campaign wakati muda bado....na aliendelea kusisitiza kuwa "kama chadema wanataka kuwajua CUF ngangari kwa vitendo wajaribu mizengwe".

Kwakweli wana Tanga walionekana wenye imani kubwa na Lipumba na walisisitiza kuwa ni wakati sasa Mchumi huyo kuiongoza nchi hii!

Karibuni wana jamvi!

Wewe Punguani isiyejielewa lini ukawa msemaji wa UKAWA.
 
Ww umekuwa msemaji wa ukawa tangu lini?????
Hayo ni maoni ya lumumba siyo ya ukawa.
Hakuna ukawa mropokaji kama ulivyobwatuka.
 
We tezi dume kweli kwani 2010 Lipumba hakupitishwa? Dr Slaa ndiye aliyesababisha tezi dume akaanguka kifaa pale jangwani halafu leo unakuja na ngonjera zako za kitezi dume hapa. Lipumba kaanza kugombea muda toka enzi za Mkapa,yeye ndiyo atakuwa analazimisha lakini sio Slaa. CCM ndiyo inakazi:- 1. kati ya kambi ya wapinga ufisadi na kambi ya mafisadi. 2. Kati ya Mkristo na Muislamu 3. Mtanganyika au Mzanzibar. Hapo lazima CCM iangukie pua tu.
Teh Teh kwa hiyo ninyi hamtaki Lipumba wala kumsikia mnamtaka Slaa ...
 
Sipingani na elimu ya Prof. Lipumba kwa maswala ya uchumi. Ila nisingempendekeza awe mgombea wa urais, kwani kwa miaka karibu 20 amegombea kwa CUF na hajaambulia kitu. Ukawa haiwezi kumbeba.

Lakini pia sijahau bado ule mkanda uleletwa hapa akitubia katika msikiti mojawapo. Hotuba iliyoonesha mwelekeo wa udini asilimia 100. Hilo ni hatari kwa usalama wa nchi na amani yake.

Hatutaki raisi ambaye atakuja kuhalalisha tukachomewa makanisa yetu kama wafanyavyo huko kwa wenzetu. Makanisa tumeyajenga kwa jasho la senti ya maskini. Mtuache tuabudu kwa amani.

Mgombea urais anayesema 'sasa ni zamu yetu', au 'sisi (waislamu) tumeonewa', hatufai.

Kwangu mimi haijalishi mgombea wa dini gani, ila asitangulize udini. Tunamtaka mgombea mcha Mungu. Haijalishi anaabudia wapi. Ila awe mcha Mungu. Tunamtaka mgombea anayeheshimu dini za wenzake, iwe ni ya kuabudu chini ya milima, mito, au miti mikubwa. Ila asiwe waabudu mashetani, maana hao hata katika tamaduni zetu hawapo. Wanaingia kwa sababu tu ya biashara, kupata hela ya haraka. Sijui wanapataga?

Kuhusu hotuba hiyo aliyotoa Prof. Lipumba, msiniulize, mkitaka waombeni MODs watuwekee tena hapa. Maana ilikuwa Jukwaa la siasa mwaka jana au juzi.

Kwa sababu hiyo tu nasema kuwa rais hafai, labda waziri wa fedha kwa taaluma yake.

Teh Teh kwa hiyo wewe ukiwa mwana UKAWA unamuita Lipumba mdini? Mbona Slaa ni Padri kwani ikulu imegeuka nyumba ya ibada? uoni ni hatari kupeleka padri ikulu
 
Wana Jf wasalaam!
Likiwa joto la uchaguzi limeanza kupanda lakini kwa upande wa UKAWA bado wana mtihani mkubwa sana kumchagua atakaye wawakilisha kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Wana UKAWA wengi wamekuwa wakipendelea Mh prof .Lipumba apeperushe bendera ya UKAWA kwani kwa sasa ana mvuto ndani na nje ya UKAWA kuliko Dr Slaa ambaye anaonekana kulazimisha lazima agombee!

Wana Jf mwezi December nilipata nafasi ya kukaa na vijana kama kumi pale Tengeru na tulibadilishana mawazo kuhusu siasa za Tanzania na wengi walijikita kujadili nani anafaa kugombea Urais kati ya Lipumba na Slaa hapa ndio ubishi ulipo anza na wengi walitaka Slaa apumzike wakisema Lipumba ndio anaye faa kipindi hiki kama wanataka kuchukua nchi na atawasaidia kufuta zile propaganda za udini.

Lakini wengine walishikilia msimamo kuwa hata kielimu Lipumba anamzidi Slaa kwani Slaa hana Elimu yeyote zaidi ya kusomea dini na Ikulu hatupeleki kiongozi wa dini kwakweli kwenye hili walibishana sana wengi wakisema Elimu ya Slaa haitambuliki kimataifa na si mtaalam wa jambo lolote.
Kuna mwingine aliendelea kusema kuwa Slaa hafai kugombea Urais maana amekuwa akichochea migogoro ndani ya chama chake na kuwagawa wanachama kwenye makundi!

Wengi walikuwa wana sisitiza kuwa patachimbika kama Lipumba hatopitishwa na hakutakuwa na maelewano kwenye hilo na wakasema Lipumba asipopitishwa kura zao watampa mgombea wa CCM kama walivyo fanya 2010!

Wana Jf joto la uchaguzi liliendelea nilipo pata safari ya kwenda Tanga nilipita mtaa fulani pale Tanga mjini na hapo nilikuta wakijadili siasa kwa upana na wengi walionekana kuunga mkono UKAWA na walikuwa wanasema wana furahishwa na mwenendo wa UKAWA lakini wana kerwa nakampeni za chinichini zinazo fanywa ili kumpitisha Slaa kugombea Urais.. na wengi walikuwa wakiongea kwa jaziba huku wakisisitiza kuwa mipango ya kumpitisha Slaa kugombea Urais hazito kubalika na patachimbika kabisa siku hiyo na hawatoburuzwa na mtu...
Kuna kijana mmoja alisema kuwa wao kama UKAWA wana mhitaji Lipumba lasivyo patachimbika ..maana wanaona dalili za mizengwe! Pia alisema ana kerwa na baadhi ya viongozi wao kuwatuma vijana wao kwenye mitandao ili wawapambe na kuwapigia campaign wakati muda bado....na aliendelea kusisitiza kuwa "kama chadema wanataka kuwajua CUF ngangari kwa vitendo wajaribu mizengwe".

Kwakweli wana Tanga walionekana wenye imani kubwa na Lipumba na walisisitiza kuwa ni wakati sasa Mchumi huyo kuiongoza nchi hii!

Karibuni wana jamvi!

mambo ya UKAWA yanakuhusu nini wewe mccm?
 
Ww mweu kweli kawe mtiifu ccm.mpuuzi ww uwezi tupangia mbona kabla awajaungana ukusema lipumba amie cdm.taira ww
Ukawa wana utaratibu wa kumteua mgombea wao wa urais kwa hiyo usituletee umbea wa mtaani. Yeyote watakayemleta ni wetu mradi awe mwadilifu,jasiri,mchapakazi. Kuhusu utaalamu sio kigezo muhimu kwani kuna maprofesa waliipewa vyeo vya siasa na hatukuona walichofanya km Kapuya, Sarungi, Msola na wengine wengi!
 
Slaa hawezi kwenda Zanzibar wakamsikiliza.

Alikwenda mara nyingi na kupokelewa kuliko rais wao kwani ana mvuto jasiri Wa kusema ukweli,mwadilifu na kwa taarifa yako anaheshimu dini zote kwani kwani dini nyingine ni mojawapo ya masomo ya upadre ndiyo maana huwezi kumsikia padre mkatoliki akikashifu dini nyingine.
 
Watakutukana sana umegusa sehemu ambayo huwa hawataki iguswe japo kwa kuangalia upeo wa mambo lipumba anaweza kuwa wa msaada zaidi kuliko slaa kwanza lipumba hana kisilani kama mzee slaa hata busara za lipumba ziko angalau kuliko dr slaa.
haa haa lipumba kagombea urais hivi mara ngapi vile..
 
Lumumba wamechanganyikiwa, wameamua kuleta vihoja vya kujaribu kuwachonganisha ukawa! Ukawa naomba msirudi nyuma ccm must go..
 
Kwa watanzania walivyo ichoka ccm wako tayari kumchagua kiongozi yeyote kutoka UKAWA.

Akipewa nafasi 2015, Lipumba atakuwa amegombea urais kwa kipindi cha miaka 25! Huko CUF hakuna watu wengine wanaofaa kugombea?
 
Huyu katumwa na ccm kuleta mvurugpo wa mawazo, na huko anakosema alipita alikuwa na issue nyingine au ndo utafiti wa kujilipa?. UKAWA ndiyo mpango mzima mipango inaendelea vizuri, wacha kukela watu.
 
Kuhusu elimu isiyotambulika na kwamba ni yakidini(Catholic), hapo umechapia pakubwa.

Unapaswa kufahamu jambo hili, "ELIMU WANAYOIPATA MAPADRI NI MARADUFU UKILINGANISHA NA ELIMU TUNAYOISOMEA KWENYE NORAMAL UNIVERSITIES""

Katika suala la elimu, hata kama Lipumba atakuwa na degree milioni za uchumi; bado kwa elimu aliyonayo SLAA, yupo juu ya Lipumba. Tena mbali mno.

Mengineyo niwakaribishe wadau waendelee kuchambua.

===============
Mnaona wakuu ndiyo maana nasema viongozi wa kidini kama slaa hawatufai kwani wanawadumaza waumini wao hadi mtu anaongea kwamba elimu ya mapadri ni bora kuliko yetu!!! how? kwamaana akiwa padre anamzidi daktari engineer and any specialist????? am sure unaumwa mhemko wa dini zaidi kama wafuasi wa kibwetere .....
Padre kaspecialize kenye kanon law na administration ya church .... anamzidi vipi specialist wa IT? or uchumi?

Mtu kama wewe ndio wanaosumbua Tanzania kwa ukosefu wa maarifa na maono.

LIPUMBA OK.
 
Back
Top Bottom